Sumaye atema cheche; Alaani waliomshambulia Tundu Lissu

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye amelaani vikali watu waliomshambulia Rais wa chama cha sheria nchini TLS Tundu Lissu na kusema kamwe watu hao na wale waliowatuma hawatapata amani wala kufurahia maisha.

Akihutubia umati mkubwa wa watu wakati akimnadi mgombea udiwani wa Chadema Kata ya Mbweni DSM, Sumaye amewataka wakazi wa Mbweni kumpigia kura nyingi mgombea wa Chadema ili kuumgana na dunia kulaani kitendo alichofanyiwa Tundu Lissu.

Sumaye pia alishangazwa na hatua ya wala rushwa kupandishwa vyeo na kuonya hiyo ni aibu kubwa kwa CCM na serikali yake.

Mheshimiwa Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani na mjumbe wa Kamati Kuu amewataka wasimamizi wa uchaguzi huu kusimamia kwa haki vinginevyo kamwe Chadema haitakubali kuibiwa kura.

Sumaye ambaye alikuwa akishangiliwa kwa mayowe amesema kwa sasa Taifa liko katika hali mbaya kiuchumi na kusema CCM imeshindwa kutawala kwani maisha ya watu yamezidi kuwa magumu na kuonya Taifa linaelekea pabaya.

Maelfu ya watu waliohudhuria mkutano huo wameahidi kutoa kura nyingi kwa Chadema kiasi kwamba CCM wataona hata aibu kuiba kura.
 

Attachments

  • IMG-20171029-WA0051.jpg
    IMG-20171029-WA0051.jpg
    67 KB · Views: 64
  • IMG-20171029-WA0050.jpg
    IMG-20171029-WA0050.jpg
    83.3 KB · Views: 65
Labda Leo ndio kaipata Hiyo habari ya kushambuliwa kwa lisu. maana sio habari tena.
 
Mbona hakuna uhusiano kati ya udiwani na shambulizi la Lisu, sanasana nahisi harufu ya uchochezi, tume ya uchaguzi wasimamie maadili na kanuni za kampeni na uchaguzi,
 
Damu za Professor Nickas Mahinda aliepigwa Risasi Chumbani Kwake na wasiojulikana na Advocate Kapinga alieuawa pia na wasiojulikana wakati zero akiwa PM zimeanza kumpanda Kichwani !
 
Back
Top Bottom