Katika uchaguzi wa demokrasia, mtu huchaguliwa kwa uwezo na kwa ajili yao kuwatumikia, katika demokrasia ya rushwa, fedha huwachagulia watu mwakilishi kwa ajili ya waliotoa fedha, kama nimetoa fedha kwa ajili yako, na wapiga kura wanakua wapiga mihuri.
Sasa imetoka mtu kuhonga achaguliwe, na sasa mtu anatoa rushwa kununua watu ili apate kujenga mtandao wake na sasa ni rushwa ya kimtandao ambayo ni hatari sana...
ni zaidi ya mary nagu walitoa rushwa nchi nzima isipokuwa kwa staili tofauti ndicho alichokisema PM mstaafu kuwa ccm wametumia rushwa na uchafu mwingine nchi nzima ktk uchaguzi wao wa ndani.
ccm mpoooo?poleni sana je 2015 itakuwaje?
tusubiri tuone!
hakika kwa staili hii ya kulielezea suala makini kimdhahamdhaha, naomba usioteshwe kuwa mgombea maana tutakula hasara kwa mara nyingine, ushauri wangu kwako PM Mstaafu kama haupo tayari kugeuka na kuipigania haki ya mtanzania ni vyema ukapumzika tu na kujilia pensheni yako taaratibu, tuachie wenye uchungu na nchi yetu tuijenge upya maana mmeibomoa vya kutosha!Sumaye:
Mambo ya Hanang, yalitokea nchi nzima... Na yalitokea kwa staili tofauti
Tatizo ni kubwa sana, maana nchi nzima mattumizi makubwa ya fedha... Tatizo ni kubwa na limeota mizizi
Nimewahi kuzungumzia mara kadhaa...
Nilisema nikiwa Same "Rushwa ni tatizo Barani na Tanzania pia... Kwetu sisi huwezi kushinda bila kutoa fedha"
Nilisema haya 2010:
"Kiongozi anayetoa rushwa anapata wapi kama si mwizi na mla rushwa... Hawezi kuwatendea haki maana wananchi ni kama bidhaa na hatawatumikia bali atatfuta za kihonga baadae"
kama hao waandishi walipewa bahasha basi itakuwa ni baada ya hiki kituko, other wise wangeondoka waka muacha peke yake kabla ya kumaliza. unaweza kudhani unaota
Na sisi ambao si waandishi na hizo bahasha hatuchukui? Katupotezea muda, hiki si kitu cha kuitisha mkutano na waandishi na kuongea. Hakuna jipya hapa. Natoka wakuu
Sumaye:
Rushwa inatengeneza wawakilishi wa mtu ama watu na si wawakilishi wa umma... Rushwa inadhalilisha watu na chama
Huyu jamaa hana jipya ni muoga sana
Ana hang over ya kukosa nafasi ccm huyu! Hivi kama angekuwa amepata angekuja kufanya press conference na kuongelea hayo anayo ongea?!
Sumaye:
Hanang'kulikuwa na matumizi makubwa ye fedha, uharamia wa kuhamisha watu... Sitokata rufaa wala sitolalamika chamani maana kila jambo lilikuwa hadharani na media ilitoa taarifa.
Siko CCM kwa ajili ya vyeo... Nchi nyingi zimeingia katika vurugu na kuhatarisha amani ktk uchaguzi,,, Tanzania tusichafue kwa kusababisha matatizo kwa kutimia vibaya umasikini wa Watanzania.
Najua si matamu kwa masikio ya wengine na tusiwanyamazishe wanaozungumzie kwa uwazi.
Mungu ibariki Tanzania
Kaongea zero mkuu! Hivi ulitegemea bangi itoe mchicha?CCM in mambo ya kipuuzi sana....na wanachama wake wapuuzi pia.
Sasa huyu zero kaongea nini....
Kama unataka biashara zako zifanikiwe peperusha bendera ya CCM "Sumaye"