Sumaye alipua watawala Afrika

Hivi yeye ana nyumba ngapi? Na pato lake lilikua ngapi?

Ni gazeti gani lile ambalo lilizitaja mpaka trilion zake huko nje ya nchi halafu walipoulizwa mahakamani wakabaki wakijikanyagakanyaga tu. mara ooh! tuliambiwa , mara tulisikia nk.
Kama unazijua zitaje hapa jamvini tujadili.
 
huyu jamaa inaonekana amechoswa na serikali ya jk,amesema magamba ni hatari kwa chama yasipovuka yatakiondoa chama madalakani
 
mi siungani mkono na wale wanaosema kuwa hakufanya kitu, infact kama hua mara flani mnasifia utawala wa mkapa basi automatic sumaye nae anaingia humo, yeye anasema watoto wake na familia yake inajulikana ilivo toka hajawa waziri mkuu mpaka anatoka uwaziri mkuu, hakuna mtoto wake aliejilimbikizia mali....hapo alikua anapiga dongo kwa familia ya baba riz.
 
amekuwa waziri mkuu kwa miaka mingi alifanya nini la kukumbukwa na watz?huyu mzee mnafiki sana halafu ni mwizi
Wakati wake tulishuhudia mfumuko wa bei ukidhibitiwa kwa kiwango kikubwa na hivyo kuleta nafuu kwa raia, mabaya pia yalikuwepo
 
amekuwa waziri mkuu kwa miaka mingi alifanya nini la kukumbukwa na watz?huyu mzee mnafiki sana halafu ni mwizi
Kama alikuwa mwivi sawa, lkn ndo asifanye mashambulizi kwa wenzake? Akae kimya tu ndo furaha yako? Au na WEWE ni mmoja wao?
 
Naomba niijadili hoja ya Sumaye, na sio Sumaye mwenyewe. Nakubaliana naye kwamba mchawi wa maendeleo katika jamii yetu ya Tanzania ni rushwa, waweza iita ufisadi. hatuwezi kuendelea kwa kauli mbiu za kilimo kwanza. Natoa ushauri kwa watawala, sijui kama wananisoma na kama wananisoma sijui kama wanajali,kwamba wabadilishe kauli mbiu. Sasa tuanze kuimba "mapambano dhidi ya rushwa kwanza". Uwekwe utaratibu ambamo kila mtanzania akijihusisha na vitendo vya rushwa akamatike. Tukizuia wizi wa raslimali za umma, tutakuwa na uwezo wa kuzielekeza raslimali za umma kwenye miradi itakayozalisha mali kwa wingi na hivyo kuwa na ajira nyingi, mali ikizalishwa, mfumuko wa bei nao utashuka. Kilimo hakiwezi kufanikiwa kama ruzuku ya pembejeo inaliwa na walio na mamlaka na raslimali za taifa zinaelekezwa kwenye miradi ambayo ni rahisi kwa wenye mamlaka kutuibia.

Lingine ni kuhusu urais. Sumaye amesema atapima kama ataona ana ubavu wa kuibuka mshindi ndipo atutangazie kwamba anautaka urais. Kwangu mimi uwezo wa mtu kuwa rais (uwezo wa kuongoza) ni muhimu zaidi kuliko uwezo wa mtu wa kushinda katika kinyang'anyiro cha kuupata urais. ningeridhika kama Sumaye angetwambia atajitathmini na akijiona ana uwezo wa kuwa rais (uwezo wa kuongoza) atatutangazia nia yake ya kuwa rais. Wala ile kuangalia kama wananchi wanapenda uwe rais ndipo utangaze nia, sikubaliani nayo. Unaweza ukawa na mvuto kwa wananchi na ukachaguliwa kwa kishindo kwa zaidi ya asilimia 80, kumbe masikini huna uwezo wa kuwa rais (uwezo wa kuongoza), huna msimamo na uwezo wa kukisimamia unachokiamini kikawa.Hii haitatusidia.
 
wadau achen unafiki inamaana hamjui kipindi cha sumaye nchi uchumi ulipanda mno, kamanda kura yangu umepata
 
kwanza ana kashfa ya shs. billion 3 kwa wakati ni pesa nyingi,na hata sasa. Akakimbilia marekani kujifanya anasoma
ili mambo yatulie. Hana mchaango wowote wa maaana katika taifa hili na alikuwa amewekwa tu kama mtu wa kusema 'ndiyo' na kwa
ujumla alikuwa hana hadhi ya kuwa waziri mkuu. Tunamkumbuka Lowasa, The true prime minister.
 
magazeti yalimponda akaenda mahakamani akashinda, mtendaji mkuu wa serikali ni waziri mkuu. je hilo halitambui ukweli utawatoa kifungoni, je hamjui serikali ya sasa inayumba kwa nini kwa kuwa mtendaji wake mkuu ni mtu wa kulalamika sana, na kushangaa, pinda anapwaya. mpeni heshima yake waziri mkuu aliyeupaisha uchumi, sina tatizo na lowasa
 
na huyu naye ni wa kutajwa.kwa waislamu ni muovu kama au kuliko sumaye.wote ni makada wa mfumo kristo.wakirudi kuomba urais wataingia madarakani kama akina jonathan wa nigeria kwa vile wana kazi waliyoazimiwa kuitekeleza lakini si kwa kura zetu.
 
Jaza methali ifuatayo; vita ya panzi..................................................................................................................
 
na huyu naye ni wa kutajwa.kwa waislamu ni muovu kama au kuliko sumaye.wote ni makada wa mfumo kristo.wakirudi kuomba urais wataingia madarakani kama akina jonathan wa nigeria kwa vile wana kazi waliyoazimiwa kuitekeleza lakini si kwa kura zetu.

Confronted with religious ideology. Huna jipya wewe.
 
Yaani mie bongoland inaniacha hoi bin taabani, mtu akitoka kwa madaraka ndo utasikia eti viongozi walioko madarakani wanatumia vibaya madaraka yao..

Yeye alitumiaje?..mbona hasemi pato lake kwa mwezi lilikuwa kiasi gani na hayo majumba aliyonayo kayajengaje?.....siasa za bongo majitaka kwelikweli.......watu ni kuchafuana tuu....sitashangaa Baba riz1 akimaliza awamu yake na kuchaguliwa mwingine na yeye ataanza kulaamu uongozi uliopo kwamba haufanyi maamuzi magumu...tehetehe........
 
na huyu naye ni wa kutajwa.kwa waislamu ni muovu kama au kuliko sumaye.wote ni makada wa mfumo kristo.wakirudi kuomba urais wataingia madarakani kama akina jonathan wa nigeria kwa vile wana kazi waliyoazimiwa kuitekeleza lakini si kwa kura zetu.

nyie mtalaum mpaka kiama, punguzeni kuongea bila vitendo...action speak louder than plain words, sasa hvi mna raisi mslam, makam mslam, raisi wa znz na makam wake nao waslam lakini bado mnapiga mayowe...hivi nyie mnadhani kuna miujiza kwenye maendeleo, fanyeni kazi, wapelekeni watoto wenu shuleni....sio mnajazana kwenye vijiwe na kulalama kila siku.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…