Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imeifungia daladala inayofanya safari zake Kimara hadi Kariakoo kwa siku 30 kutokana na kuwatoza abiria nauli ya Sh. 800 tofauti na iliyopangwa na mamlaka hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Michael Kisaka, daladala hilo lenye namba za usajili T 276 AYT linalofanya safari zake Kimara-Kariakoo lilikamatwa kwa kosa la kutoza nauli zaidi ya kiwango kilichoridhiwa na mamlaka hiyo. Taarifa hiyo ilieleza kuwa abiria walitozwa nauli ya Sh. 800 badala ya Sh. 500 kwa safari ya ruti hiyo.
"Huo ni ukiukwaji wa Kanuni namba 34 na 35 ya Kanuni za Leseni ya Usafirishaji kwa Magari ya Abiria ya mwaka 2007," alieleza. Mamlaka inatoa adhabu ya kufungia basi hilo T 276 AYT lenye leseni namba A2A044023 kwa muda wa siku 30 kwa njia zote za Tanzania Bara na kwamba adhabu hii itaanza leo.
Aidha, mmiliki alitakiwa kuwasilisha barua yenye maelezo na vielelezo kuhusu hatua zilizochukua dhidi ya dereva na kondakta wa gari lako kwa kosa hilo.
CHANZO: NIPASHE
Tena SUMATRA inabidi waangalie uwezekano wa kushusha nauli zote za mabasi kwani mafuta yameshuka bei.
Tena SUMATRA inabidi waangalie uwezekano wa kushusha nauli zote za mabasi kwani mafuta yameshuka bei.
Nchi yetu suala la usimamizi, uwajibikaji ni masuala sugu yaliyokosa dawa stahiki...
Route nyingi usiku na asubuhi nauli zinapaishwa watu wa gongo la mboto mpaka chanika wameshazoea hii hali
toka zako
hahaha!!! itakuwa ni yule wanamuita 'osama'.kuna dala dala huwa inafanya route zake toka kariakoo mpaka kimara hutoza 1000, na abiria wengi wanaifahamu kwani huwawahisha na kuwaepusha na adha za foleni, dereva wake huwa ni mjanja mjanja kukwepa foleni, wengi wa abiria wazoefu huwa na mawasiliano na dereva mhusika kabla ya kufika kituoni, nadhani itakua ndio hilo basi kama sijakosea
3500,000 + 250,000 + 150,000 + 250,000 + 100,000 = 4,250,000.... kwa taarifa tu, kama wewe unatabia ya kupakia abiria kwenye kigari chako wakati wa kwenda na kurudi kazi, summatra wakikushika adhabu yao ni shilingi 1,100,000/= mchanganua kama ifuatavyo
Kubeba abiria bila kibali cha kutoka summatra 3500,000/=
kutoza naluli kubwa kuliko kiwango 250,000/=
kuto kuwa na tiketi 150,000/=
kuto kuwa na sare 250,000/=
kukatisha ruti 100,000/=
Tahadhari kwa wenye HOHA mitaa ya mbagala yasikukute !!!
Tena SUMATRA inabidi waangalie uwezekano wa kushusha nauli zote za mabasi kwani mafuta yameshuka bei.
Kuna mda mwingine unaandika vitu vya msingi kweli. Lakini ukianza kuchangia thread za CCM akili inaenda likizo.
Nisome vizuri utafaidika na mengi sana.
Unakosea Dada faiza nauli ya daladala haipandi kwasababu ya mafuta tu, jaribu kuulizia spea uone zilivyo panda biashara ya daladala nishiida tu hakuna faida ya kutisha.