sumatra na upandaji wa nauli

Rukiko

Senior Member
May 5, 2009
195
57
kati ya maswali ambayo huwa najiuliza na sipati jibu ni-kwanza,vipi sumatra wanashindwa kudhibiti daladala kujipandishia nauli kiholela- hasa jijini dar? pili; hivi wakati wa mwaibula hakukuwa na upandaji wa bei za mafuta huko yanakotoka? tatu, inakuwaje mwaibula alionekana kufanya kazi nzuri kuliko sumatra-ukizingatia uwingi wao?

sasa, jana nimepanda gari moja kwenda goms toka kariakoo, ikionyesha kuwa nauli yake ni sh 350 kuanzia mchana huo wa jana,na ticket ndio ilivyosomeka(nimeambatanisha ticket). Lakini watu walilalamika sana, inakuwaje asubuhi tumelipa mia tatu sasa mnasema mia tatu na hamsini. pamoja na kulalamika kwao waliishia kulipa-nafikiri baada ya kuona hawana pa kupeleka malalamiko yao-pengine. wasiwasi wangu ni kuwa ni lini sumatra imetoa tamko jingine baada ya lile lililoanza kutumika march 10,2011 kuhusu upandaji wa nauli tena. je hii haionyeshi kuwa ndani ya kipindi kifupi tu kila maeneo yatakuwa yanajipandishia nauli tu ili mradi yameweza kuchapisha ticket?
kama kuna mtu wa sumatra humu anisaidie
goms.jpg
 
Back
Top Bottom