Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,441
- 7,780
Leo Rais Samia amepokea ripoti ya CAG Ikulu Dodoma na kuongelea mambo kadhaa ikiwemo suala la mafuta. Rais Samia amesema waziri husika aliondoa tozo ya Tsh 100 kwenye lita ya mafuta bila kuangalia upana wake ikiwemo tayari ilikuwemo kwenye bajeti ambayo ilipitishwa na Bunge hivyo Rais ameagiza irejeshwe.
Rais Samia ametaka wananchi kuambiwa ukweli kwamba nauli zitapanda na usafirishaji wa bidhaa umepanda, gharama ambazo zitaingizwa kwenye bei za vitu.
Kuhusu bei ya mafuta ya kula ameomba tathmini ya tozo iliyowekwa kwenye mafuta yanayotoka nje ili kulinda viwanda vya ndani itazamwe tena kwani viwanda hivyo vya ndani havizalishi.
========
Rais Samia: Bei zimepanda kwa bidhaa nyingi tunazoagiza kutoka nje lakini kuna upandaji wa bei za mafuta, mafuta yamekuwa yakipanda nadhani kutoka mwaka jana katikati ya mwaka.
Tukachukua hatua ya kupunguza tozo ndani ya mafuta kwa mara ya kwanza ili kushusha bei ya mafuta kwa wananchi lakini mafuta yameendelea kupanda.
Kipindi hiki cha pili mafuta yamepanda kwa 156 kwa lita, waziri akaona nikitoa shilingi mia yapande kwa shilingi 56 nitaleta unafuu ndani ya nchi lakini kwa bahati mbaya hakuangalia kwa upana zaidi ile ilikuwa tayari iko kwenye bajeti iliyopitishwa na bunge kwahiyo kulikuwa na utata kidogo, tumekaa kama Serikali tumerekebisha.
Ile shilingi iliyotoka, nimeagiza irudishwe na tathmini tuliyofanya hata kama ile shilingi tungeitoa, kwa mwenendo wa upandaji wa mafuta duniani, bado isingekuwa na impact ila tungejikosesha kile ambacho tunakifanya, kwahiyo tumeamua shilingi irudishwe.
Wabunge wenye maeneo yenu, mawaziri mnaosimamia sekta waambieni wananchi ukweli, vita ya Russia na Ukraine imepandisha sana bei ya mafuta na mafuta yanapopanda ndio kila kitu kinapanda.
Nauli zitapanda, usafirishaji wa bidhaa zitapanda. Sasa hivi kutoa kontena China ya bidhaa kuleta Tanzania walikuwa wanalipa kontena ya ft 40 dola 1500, sasa hivi ni dola 8,000-9,000. Hii inaenda kuingia kwenye bidhaa anazozileta kwahiyo waambieni wananchi ukweli, wasikae tu kulaumu Serikali haisemi kitu.
MAFUTA YA KULA
Rais Samia: Nakumbuka nilikuagiza waziri wa fedha kwamba katika bajeti yetu tunayoimaliza tuliingiza kitu katika mafuta ya kula nadhani na ya nyuma yake ili kulinda viwanda vya ndani nadhani kwenye uzalishaji lakini pamoja na kuongeza hiyo kitu kuzuia mafuta ya nje yasije, viwanda vya ndani ndio vimefungwa kabisa hata huo uzalishaji wenyewe, kwahiyo naomba litizameni tena.
Kama haitusaidii ondoeni ili mafuta ya nje yaingie angalau hata kama bei itakuwa kubwa lakini wananchi wana mafuta ya kutumia. Sasa mmezuia ya nje hayaingii, ndani hayazalishwi, wananchi wanapiga kelele bila shaka mafuta yatapanda bei kwa kiasi kikubwa, nendeni katazameni vipengele vitakavyoleta unafuu kwa wananchi.
=> Kwa mfano kwenye bei ya mafuta Afrika Mashariki na kati Tanzania ndio ina bei ya chini kabisa ya mafuta lakini wenye sekta hawasemi, wamekaa tu wanajifungia.
PIA, Soma=> Rais Samia aagiza tozo za mafuta kupunguzwa