SUMATRA kutangaza nauli wiki hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SUMATRA kutangaza nauli wiki hii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Giro, Mar 4, 2009.

 1. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Daily News; Tuesday,March 03, 2009 @20:14

  Hatma ya nauli ya mabasi kushuka inatarajiwa kufahamika baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kukamilisha mchakato wa kukokotoa hesabu. Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekirasa, alisema jana kuwa bado wanamalizia mchakato huo na siku yoyote wiki hii watatoa majibu juu ya mapendekezo ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na mamlaka hiyo, kutaka nauli ishuke kwa asilimia 25 baada ya bei ya mafuta kushuka.

  Katika kikao cha wadau wa usafiri kilichofanyika Januari 26 mwaka huu, mamlaka hiyo iliahidi kutoa majibu baada ya wiki mbili, kutokana na maoni ya wadau kuhusu mapendekezo hayo. Wakati huohuo, Sekirasa alisema vitendo vya uvamizi wa meli katika Bahari ya Hindi vinaongezeka kila mwaka, hivyo kutishia uchumi kwa meli za kimataifa kuogopa kutumia bandari za nchini kwa kuhofia usalama
   
 2. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yeah, hope it takes into account the increment rate when oil prices rose and the actual situation now for is ought to be a to way traffic here
   
Loading...