SUMATRA Kuratibu Mkutano wa TBC!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,428
113,432
Wanabodi,
Nikifuatilia Bunge live on TBC, matangazo yalikatika na TBC wakaanza kurun promo zao na matangazo mbalimbali. Nimeona Tangazo kuwa wiki hii, TBC itafanya mkutano mkubwa kwa watatarishaji vipindi vya elimu kwa umma mjini Dodoma.

Cha ajabu katika tangazo hilo, eti mkutano huo utaratibiwa na SUMATRA!.

TBC na SUMATRA wapi na wapi?.

Nadhani they ment TCRA na Sio Sumatra.

Nakumbuka miaka ya nyuma, mtangazaji mmoja (Jina nalihifadhi), alisoma habari na kuwa Serikali itatelekeza siasa ya ujamaa na kujitegemea wakati alipaswa kusema serikali haitatelekeza siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Mtangazaji yule alisimamishwa jumla kusoma habari, licha ya kujitetea hivyo ndivyo ilivyoandikwa, akaambiwa yeye kama mtangazaji wa habari alipaswa kufahamu!.

Ndivyo ilivyo kwa vituo vya utangazaji, naamini watangazaji wote wanapaswa kufahamu regulator wao ni nani. pia kujua SUMATRA inasimamia nini!?
 
Back
Top Bottom