Sumatra kuanzisha huduma za usafiri

Prodigal Son

JF-Expert Member
Dec 9, 2009
1,067
697
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), inakusudia kuanzisha utaratibu wa kutoa huduma za usafiri wa umma kupitia kampuni au ushirika wa wasafirishaji.

Utaratibu huo unakusudiwa kuanza katika majiji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya lengo ni kuwawezesha wasafirishaji kupata mikopo kwenye benki na mashirika mbalimbali kupitia kampuni zitakazoanzishwa.

Hayo yalisemwa jana mkoani hapa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Israel Serikasa wakati akizungumza na wadau wa usafirishaji na kujadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wasafirishaji hao.

Sekirasa alisema lengo la kuanzisha usafiri wa kampuni ni kurahisisha udhibiti wa utoaji huduma ya usafiri kwani kila kampuni au ushirika utawajibika kuwa na wakaguzi wake wa ndani.

Alisema pia utaratibu huo utapunguza msongamano wa magari hususan kwenye miji mikubwa ambayo hutokana na kuwepo kwa idadi ya magari yasiyoendana na mahitaji pamoja na miundombinu iliyopo.


CHANZO; Habari Leo
 
Naamini matatizo ya usafiri katika miji hususani DSM, Arusha, Mwanza, ni miundombinu na si kingine, na suluhisho litapatikana kwa miundombinu kuboreshwa na si kila siku kuja na hekaya ambazo utekelezaji wake ni ndoto, Umefika wakati ufumbuzi wa haya matatizo waachiwe wataalamu husika na sio wanasiasa,Ni juzi tu Ngugu Raisi katoa agizo Dar kujengwe madaraja ya juu ( Fly over), huyu leo kaja na lake, kesho na mkuu wa mkoa atakuja na lake ili mradi siku zinakwenda,
 
sijuia nani atakua mamlaka na nani atakuwa vendor hapa... thinking like kids!!!:(
 
Back
Top Bottom