SUMATRA fuatilieni utapeli huu AZAM MARINE

SUMATRA fuatilieni utapeli huu AZAM MARINE

Kweli vyuma vimekaza, buku 10 mtu anatoa povu la hatari khaaa
 
Pale Zenji ukitokea Ferry ni umbali wa kama Mlandizi tu,
Ilifaa tulipe Buku tu kama tunavyolipa kwenda Mlandizi
Usipende slope mtoto wakiumee wewe,kibaya Zaid mvulana wa dar, pole Sana Kwa kuingizwa mjin na mwanaume wa mkoani
 
hawa sumatra sijui wanafanya nini yaani toka Kilimanjaro mpk Dodoma nauli ni 23,000 ila tunakatiwa Kwa 28,000 alafu wao wanasimamisha tumbo zao huko barabara wakipewa ela ya kiwi na makonda wasifike kwenye gari
Kwa mabasi kuna nauli tatu tofauti kutegemea na daraja. Yapo madaraja matatu kama ifuatavyo 1. Daraja la kawaida 2. Daraja la uchumi 3. Daraja la biashara. Kwa kiingereza ni Ordinary class, economy class na business class. Nauli kwa kila daraja zinatofautiana mkuu.
 
mzee huyu hata ungemuweka kwenye injini kwa buku ten angekubali tu!
Mkuu
Mungu Ni Mwema Wakati Wote


Lalamiko Lako Ni La Msingi
Hutokea Hayo Lakini Ni Wizi Japo Ticket Huandikwa Bei Hiyo Hiyo
 
mkuu kama ticket imeandikwa bei hiyo unayolalamikia i.e 35000 ihifadhi na ikiwezekana hayo malalamiko yako yaweke katika maandishi na uyawasilishe SUMATRA (kama hutojali) unaweza kuwa mkombozi wa tatizo hilo kwa watapeliwaji wengi
SUMATRA na Zanzibar Maritime Authority (ZMA) kwa pamoja wakishirikiana kwa dhati wanaweza kuondoa tatizo hilo.

Niliwahi kusikia kuwa SUMATRA na ZMA huko nyuma walikuwa hawapikiki chungu kimoja hasa kutokana na jeuri ya ZMA hadi mwaka 2011 meli ya MV Spice Islanders ilipojaza abiria mara nne ya uwezo wake, ikapata ajali kwenye mkondo wa Nungwi na kuua mamia ya abiria wake. Baada ya hapo ndipo ZMA ikaona umuhimu wa kushirikiana kwa karibu na wenzao wa SUMATRA.
 
Pole sana. Siku nyingine kwea na pipa watakuwa wanakuona upo winguni tu.
 
Kwa mabasi kuna nauli tatu tofauti kutegemea na daraja. Yapo madaraja matatu kama ifuatavyo 1. Daraja la kawaida 2. Daraja la uchumi 3. Daraja la biashara. Kwa kiingereza ni Ordinary class, economy class na business class. Nauli kwa kila daraja zinatofautiana mkuu.
Ni wizi ticket unayopewa officen ukifika kweny bus wanakunyang'ang'a wanakupa yenye bei elekezi
 
Next time chelewa chelewa maana muda ukiisha halafu nafasi bado zipo inabidi wachukue tu hiyo hela!
 
Weka picha ya alokukatia tiketi tuanze nae kama mfano kwa wengine!!
 
Habarini wakuu!

Niende moja kwa moja juu ya utapeli unaofanywa na wakata tiketi wa boti za Azam. Mnamo siku ya Alhamis majira ya saa saba mchana nilifika bandarini nikiwa ni msafiri kwenda Zanzibar. Bajeti ya nauli niliyokuwa nayo ni 25,000 kwenda na kurudu nauli hio hio.

Sasa kufika pale nikaambiwa bei ni 35,000/- nikasema nataka ya 25, mkatishaji akasema labda ukate ya kesho asubuhi. Basi kwa shingo upande nikaongeza 10,000/- nikapewa hio ya elf 35.

Kinachoniuma zaidi ni pale jamaa yangu niliyekuwa nasafiri nae alifika bado robo saa tuanze kuingia melini alikata tiketi ya 25,000/-. Kabla hajafika nilimwambia awahi asijekuta na hizo za 35 zimeisha akaambulia za 50.

Hilo nikalimezea tu nikasema bas labda sio bahati yangu. Kilichoniuma zaidi na zaidi ni huko Zenji, nilifika saa moja kasoro asubuhi kukata tiketi na hapo pia naambiwa hakuna za elfu 25 kwenye boti ya saa tatu zipo za 35, 50 na 60 tu. Kwa shingo upande tena nikakata hio 35.

Jamaa yangu kama kawaida yake kachelewa chelewa badae anakuja bandarini ananipigia simu namwambia nipo humu VIP Lounge, anasema kwani sikupata za 25? Mbona yeye kakata sasa hivi kwa 25!

Kwa kweli nimeumia sana kwani bajeti yangu imeharibiwa na hawa wakata tiketi, hivyo naomba sana SUMATRA komesheni hii hali, yaani wanalazimisha kuuza za bei ya juu kwanza halafu ndio wauze economy. Na wanadanganya kwa kusema zimeisha. Sumatra tusaidieni kwa hili tafadhali.

Nawasilisha wakuu!
Bila shaka ww utakuwa msukuma, bonge la mshamba!
 
Umepigwa na vijana wa town. Wajinga ndio waliwao
 
mkuu kama ticket imeandikwa bei hiyo unayolalamikia i.e 35000 ihifadhi na ikiwezekana hayo malalamiko yako yaweke katika maandishi na uyawasilishe SUMATRA (kama hutojali) unaweza kuwa mkombozi wa tatizo hilo kwa watapeliwaji wengi
Sawa mkuu leo nataka kushughulikia hili suala
 
Back
Top Bottom