Amicus Curiae
JF-Expert Member
- Sep 12, 2012
- 5,352
- 7,668
Wasalaam Aleykum wakuu.
Mimi ni mwanasheria wa kujitegemea, kwa kuzingatia kwamba nimefanya kazi hii ya sheria kwa vitendo kwa takribani miaka mitatu (3) sasa, nimebahatika kuandika kitabu chenye jina "DONDOO MUHIMU ZA NAMNA YA KUKABILIANA NA KESI ZA ARDHI, JINAI, MADAI, MIRATHI NA NDOA HASA KWA WASOMAJI WASIO WANASHERIA NA WANASHERIA WACHANGA (SOMO FUPI LA SHERIA KWA VITENDO)". Nilitamani kukigawa bure lakini kwasababu sina uwezo huo, nimeona nikiuze kwa bei nafuu kabisa ya shilingi za Kitanzania elfu kumi (10,000/=) ; ambayo itafidia gharama za uandaaji wake tu. Napatikana Dodoma ila mikoani natuma, lakini pia natazamia kuanza kukiuza online.
Turejee kwenye mada...
Uzoefu wangu kwenye kazi hii umenifanya nigundue kwamba zaidi ya asilima themanini (80%) ya wanawake wanaoomba talaka wanalenga zaidi mgawanyo wa mali. Sasa kuna kitu kimoja kinaitwa 'Marriage Prenup' au 'Prenuptial Agreement'. Haya ni makubaliano yanayofanyika baina ya wanandoa kabla ya ndoa, kuhusu mgawanyo wa mali ikitokea wameachana au mwanandoa mmoja amefariki. Huu utamaduni umezoeleka zaidi Nigeria ingawa hapa Tanzania bado Sheria zetu haujautambua.
Lakini mimi naamini hatujachelewa, kwasababu hata hii kitu inaitwa 'plea bargaining' inayofanyika Tanzania hivi sasa, haikuwepo before. Ulikuwa ni utamaduni wa America. Hii 'plea bargaining' ndiyo huu utaratibu wa mtuhumiwa wa kosa la jinai, kama hawa wenye makosa ya uhujumu uchumi, kukiri kosa na kuilipa fidia Serikali. Kabla ya utaratibu huu kutambulika Tanzania, Serikali imekuwa ikipata hasara, kwasababu kuendesha kesi za jinai ni gharama sana, kwa mfano; imagine kama kesi ipo Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma lkn shahidi/mashahidi kwenye kesi hiyo wanatoka Simiyu, inabidi Serikali iwalipie nauli, posho n.k, lakini muda ambao kesi inasikilizwa pia ni tatizo kwa Serikali, kwahiyo kama mtuhumiwa akikiri kosa mapema anaokoa muda wa Mahakama na rasilimali fedha za Serikali.
Ombi langu kwa Serikali ni kwamba 'Prenuptial Agreement' iwe incorporated kwenye SHERIA zetu halafu tuone kama migogoro ya ndoa haitapungua.
DISCLAIMER: Wapo mabinti ambao hawana tamaa ya mali. Hivyo wakiomba talaka wanakuwa wamechoshwa kweli na vituko vya wenza wao.
Karibuni mchangie wakuu.