Hata Makonda naye. Nadhani kila RC aliwahi kujaribu na kukwama kutokana na sababu mbalimbali.Yusuph Makamba aliongoza kampeni ya kupanda miti Dar na ilifanikiwa kwa kiasi fulani. Lakini baadhi ya miti ilingolewa kupisha upanuaji wa barabara.
Exactly. Hiyo mbinu ni nzuri sana.Na iwe sheria. kwamba kila mwenye kumiliki eneo la kiwanja kwa ajili ya makazi au biashara. Lazima awe na idadi ya miti kuendana na ukubwa wa eneo lake
. Hii itasaidia sana kila mtu kuwa jibika kwa kiasi chake
Wapi huko?Njooni huku kwetu,hakuna magorofa marefu wala bahari lakini hali shwari,saa hizi baadhi yetu wamevaa makoti na usiku bila ya blanketi hulali, NA Ukimuona mtu ana handkerchief basi ujuwe ni kwaajili ya mafua na sio kufutia jasho.....
Uko sahihi kiongozi. Kuna changamoto kubwa ya maeneo mengi ya wazi kutwaliwa na kufanywa makazi. Maeneo haya yalipangwa makusudi kwa lengo la kutoa nafasi kwa miradi kama hii na uhifadhi."Failing to plan is planning to fail"! Hiyo miti Dar es Salaam unaipanda wapi, au angani!? Angalia hata viwanja vinavyopimwa 2000s bado havina space za kutosha kuweza kupanda miti ya kutosha. Angalia sehemu kama Oyster bay iliyo planned ina miti lakini mfano Kariakoo, Mnnyamani au Magomeni unapata wapi kichochoro cha kupanda miti kwa mfano!?
Hata maeneo yaliyoachwa kimkakati kama Mwembe Yanga au Mnanzi mmoja kuna nyumba zinaanza kujengwa na kuchukua maeneo ya miti!
Mkuu wazo ziri nakupongeza,
Nasikitika pia uzi huu muhimu kukosa wachangiaji wengi
Pambana nao hao unaohisi wanamtukana Rais, usiishie kulalamika tu bila kuchukua hatua.Mkuu wazo ziri nakupongeza,
Nasikitika pia uzi huu muhimu kukosa wachangiaji wengi kwa kua "mizwazwa" ipo vyumbani mwao ikitype kumponda Rais kila kukicha na kuacha mambo muhimu ya nchi yakienda na upepo
Mizwazwa hii kwa nahisi inalipwa kutekeleza kazi hii
coasta regions zote duniani,joto linawahusu..inategemea pepob za bahari zimavuma kwa joto kuelekea wapi,na mwinuko was eneo kutoka usawa bahari..Ingeanza kampeni walau kila mji ama mtaa walazimike kupanda idadi flani tutazoea
Km vile usafi
Shida Makonda anadeal na vitu petty sana; leo anadeal na ishu za mapenzi mfano aliehonga IST anaweza idai iwapo jini mkata kamba kaingilia mahusiano
coasta regions zote duniani,joto linawahusu..inategemea pepob za bahari zimavuma kwa joto kuelekea wapi,na mwinuko was eneo kutoka usawa bahari..
Wewe,Eyakuze hamjasoma CLIMATOLOGY!Upandaji miti ndio njia ya haraka na uhakika zaidi.
Joto la Dar ni pasua kichwa mpaka imekuwa nembo ya jiji. Ni miaka na miaka jua limekuwa kali na kutafsirika kuwa ndio Jiji lilivyo. Notion ya ajabu sana!
Nimeona wazo hili la Aidan Eyakuze linafaa kupewa umuhimu. Kwamba; kupunguza pollution na kufanya jiji hili lenye watu wengi zaidi nchini lipumue, basi kampeni ya upandaji miti ifanyike kwa kuweka lengo la idadi ya miti milioni kadhaa.
"So, Dar has a population of approx. 3.5m permanent residents. What if we planted 7m new trees in the next 7 years to cool the city down and reduce pollution? Milan's mayor is planning to plant a "mere" 3m trees. Let's beat them! Any takers?"
Nakumbuka RC Makonda alianza vizuri kwenye kampeni yake ya #MtiWangu kipindi fulani. Turejee na ile plan tena kwa ukubwa wake.
Wananchi nao washirikishwe na ikibidi liwe ni zoezi la lazima tena lisimamiwe hata kwa viboko (sina uhakika kama natania hapa au la).
Upandaji miti uendane na utunzaji wa mazingira kwa sheria kali consistently.
Hapa naandika huku nasweat.