Suluhisho la Joto la Dar ni kupanda mamilioni ya miti

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,433
7,055
Upandaji miti ndio njia ya haraka na uhakika zaidi.

Joto la Dar ni pasua kichwa mpaka imekuwa nembo ya jiji. Ni miaka na miaka jua limekuwa kali na kutafsirika kuwa ndio Jiji lilivyo. Notion ya ajabu sana!

Nimeona wazo hili la Aidan Eyakuze linafaa kupewa umuhimu. Kwamba; kupunguza pollution na kufanya jiji hili lenye watu wengi zaidi nchini lipumue, basi kampeni ya upandaji miti ifanyike kwa kuweka lengo la idadi ya miti milioni kadhaa.

"So, Dar has a population of approx. 3.5m permanent residents. What if we planted 7m new trees in the next 7 years to cool the city down and reduce pollution? Milan's mayor is planning to plant a "mere" 3m trees. Let's beat them! Any takers?"

Nakumbuka RC Makonda alianza vizuri kwenye kampeni yake ya #MtiWangu kipindi fulani. Turejee na ile plan tena kwa ukubwa wake.

Wananchi nao washirikishwe na ikibidi liwe ni zoezi la lazima tena lisimamiwe hata kwa viboko (sina uhakika kama natania hapa au la).

Upandaji miti uendane na utunzaji wa mazingira kwa sheria kali consistently.

Hapa naandika huku nasweat.
 
Yusuph Makamba aliongoza kampeni ya kupanda miti Dar na ilifanikiwa kwa kiasi fulani. Lakini baadhi ya miti ilingolewa kupisha upanuaji wa barabara.
 
Yusuph Makamba aliongoza kampeni ya kupanda miti Dar na ilifanikiwa kwa kiasi fulani. Lakini baadhi ya miti ilingolewa kupisha upanuaji wa barabara.
Hata Makonda naye. Nadhani kila RC aliwahi kujaribu na kukwama kutokana na sababu mbalimbali.

Jitihada zinahitajika kutokomeza hili joto. Labda kama lina economic importance kubwa zaidi likiwepo.

Maeneo yapimwe upya ili isitokee tena tukang'oa miti kupisha miradi fulani.

Kibwagizo: Wanaume wa Dar wakiambiwa joto linapunguza nguvu za kiume watapanda miti kwa juhudi kubwa. teh!
 
Na iwe sheria. kwamba kila mwenye kumiliki eneo la kiwanja kwa ajili ya makazi au biashara. Lazima awe na idadi ya miti kuendana na ukubwa wa eneo lake
. Hii itasaidia sana kila mtu kuwa jibika kwa kiasi chake
 
Njooni huku kwetu,hakuna magorofa marefu wala bahari lakini hali shwari,saa hizi baadhi yetu wamevaa makoti na usiku bila ya blanketi hulali, NA Ukimuona mtu ana handkerchief basi ujuwe ni kwaajili ya mafua na sio kufutia jasho.....
 
Exactly. Hiyo mbinu ni nzuri sana.

Jiji lina hali ya hewa nzito sana hili. Tunahitaji fresh air kwa kweli. Ni kama hakuna ventilation kabisa!

Hivi karibuni nilibahatika kuzurura mikoa mingi ya Tanzania baada ya muda mrefu. Nimeona kwa ujumla hali ya hewa ya nchi sio nzito hivi. Basi tu!
 
Njooni huku kwetu,hakuna magorofa marefu wala bahari lakini hali shwari,saa hizi baadhi yetu wamevaa makoti na usiku bila ya blanketi hulali, NA Ukimuona mtu ana handkerchief basi ujuwe ni kwaajili ya mafua na sio kufutia jasho.....
Wapi huko?

Kiukweli ndani ya nchi hii kuna sehemu nyingi ukifika ni kama umeenda ughaibuni.

Tunaweza kubalance hali ya hewa.

Kwa bahati nzuri ardhi yetu imebarikiwa sana. Miti inaota. Hakuna gharama kubwa na hatuhitaji kabisa expensive artificial projects za kuwezesha kuwa na hali ya hewa nzuri. Ni suala la utashi na utayari tu!
 
"Failing to plan is planning to fail"! Hiyo miti Dar es Salaam unaipanda wapi, au angani!? Angalia hata viwanja vinavyopimwa 2000s bado havina space za kutosha kuweza kupanda miti ya kutosha. Angalia sehemu kama Oyster bay iliyo planned ina miti lakini mfano Kariakoo, Mnnyamani au Magomeni unapata wapi kichochoro cha kupanda miti kwa mfano!?
Hata maeneo yaliyoachwa kimkakati kama Mwembe Yanga au Mnanzi mmoja kuna nyumba zinaanza kujengwa na kuchukua maeneo ya miti!
 
Mkuu wazo ziri nakupongeza,

Nasikitika pia uzi huu muhimu kukosa wachangiaji wengi kwa kua "mizwazwa" ipo vyumbani mwao ikitype kumponda Rais kila kukicha na kuacha mambo muhimu ya nchi yakienda na upepo

Mizwazwa hii kwa nahisi inalipwa kutekeleza kazi hii
 
Uko sahihi kiongozi. Kuna changamoto kubwa ya maeneo mengi ya wazi kutwaliwa na kufanywa makazi. Maeneo haya yalipangwa makusudi kwa lengo la kutoa nafasi kwa miradi kama hii na uhifadhi.

Ukiritimba ndio umetufikisha hapa. Watu wameuziwa maeneo hayo kinyume cha sheria na wengine wamejisogeza tu kwa vile hakuna ufuatiliaji.

Mjadala huu ukasaidie kufufusha yote haya. Sheria si zipo? Zinasemaje? Najua athari inaweza kuwa kubwa kushughulikia watu lakini kuna busara pia. Itumike hiyo.

Kama tunaweza kubomoa makazi ya watu kupisha ujenzi wa barabara, hatuwezi kukosa la kufanya kupisha upandaji miti.

Faida za kuwa na hali ya hewa nzuri zinajulikana. Hasa kwa Jiji kubwa na mashuhuri kama hili.
 
Mkuu wazo ziri nakupongeza,
Nasikitika pia uzi huu muhimu kukosa wachangiaji wengi

Asante sana mkuu. Naamini kuna wachangiaji wengine hawajauona bado. Tuvute subira, watakuja tu.

Ifahamike tu kuwa maoni yanayotolewa hapa yanafuatiliwa kwa ukaribu na mamlaka husika.
 
Mkuu wazo ziri nakupongeza,

Nasikitika pia uzi huu muhimu kukosa wachangiaji wengi kwa kua "mizwazwa" ipo vyumbani mwao ikitype kumponda Rais kila kukicha na kuacha mambo muhimu ya nchi yakienda na upepo

Mizwazwa hii kwa nahisi inalipwa kutekeleza kazi hii
Pambana nao hao unaohisi wanamtukana Rais, usiishie kulalamika tu bila kuchukua hatua.

Sawa umeunga mkono hoja, nini maoni yako kuhusu hili? Miti ipandwe vipi Dar sehemu kama Kariakoo, Posta, Magomeni n.k huko ndiko joto lipo barabara ukilinganisha na maeneo ya pembezoni.
 
Penye nia pana njia kwani nchi nyingi sasa imekuwa ni kuvunja rekodi tu ya kupanda miti
Ethiopia wamejitahidi sana kwa kuipanda
Na kuna wakati walivunja rekodi kwa siku moja
Pembezoni mwa barabara zote miti ingepandwa na pembezoni kote ingepandwa hata millions of
Kwa joto lilivyo hapo kati wangezuia magari kuingia na kufanya sehemu friendly kwa waendesha baiskeli na watembea kwa miguu tu

Kila kitu kinawezekana ni maamuzi tu kuna kundi moja ulaya la watu 100 walipanda miti 50,000 kwa siku moja je sisi watu 10,000 tungepanda miti mingapi kwa siku tukiamua

Kila nchi imeamua kuhangaika kivyao kwanini sisi tushindwe?
 
Ingeanza kampeni walau kila mji ama mtaa walazimike kupanda idadi flani tutazoea
Km vile usafi

Shida Makonda anadeal na vitu petty sana; leo anadeal na ishu za mapenzi mfano aliehonga IST anaweza idai iwapo jini mkata kamba kaingilia mahusiano
 
Kwa upande wangu hili jiji bila ya joto hua halinogi kabisa.
Hata nikiwa nazurura kariakoo, kisutu na posta bila ya kukasikia kale ka harufu ka mitaro inayopitisha pilipili za wadosi hua sijifeel kama nimefika mjini.
 
Msingi wa tatizo ni mipango miji.
Kama jiji likipangwa vizuri, kwa kubomoa na kufanya marekebisho, hali itabadilika kwa kiasi kikubwa.
 
Ingeanza kampeni walau kila mji ama mtaa walazimike kupanda idadi flani tutazoea
Km vile usafi

Shida Makonda anadeal na vitu petty sana; leo anadeal na ishu za mapenzi mfano aliehonga IST anaweza idai iwapo jini mkata kamba kaingilia mahusiano
coasta regions zote duniani,joto linawahusu..inategemea pepob za bahari zimavuma kwa joto kuelekea wapi,na mwinuko was eneo kutoka usawa bahari..
 
Uko sahihi mkuu. Kwa kuongezea tu nadhani mleta mada alimaanisha tupande miti walau ipoze kidogo joyo kwa ile effect ya microclimate...kwamba pamoja na hizo natural factors, basi joto lingepungua kwa miti kupoza hewa joto kutoka baharini, kupunguza vumbi na kuchangia kupunguza kabonidayoksaidi kutoka angani. Pia miti ingepunguza makali ya jua kwa kuwepo vivuli sehemu nyingi.

Kwa hali ilivyo kukosekana kwa mipango miji ni janga kubwa.sehemu kama kariakoo hivi moto ukizuka watu watakimbili wapi?
coasta regions zote duniani,joto linawahusu..inategemea pepob za bahari zimavuma kwa joto kuelekea wapi,na mwinuko was eneo kutoka usawa bahari..
 
Upandaji miti ndio njia ya haraka na uhakika zaidi.

Joto la Dar ni pasua kichwa mpaka imekuwa nembo ya jiji. Ni miaka na miaka jua limekuwa kali na kutafsirika kuwa ndio Jiji lilivyo. Notion ya ajabu sana!

Nimeona wazo hili la Aidan Eyakuze linafaa kupewa umuhimu. Kwamba; kupunguza pollution na kufanya jiji hili lenye watu wengi zaidi nchini lipumue, basi kampeni ya upandaji miti ifanyike kwa kuweka lengo la idadi ya miti milioni kadhaa.

"So, Dar has a population of approx. 3.5m permanent residents. What if we planted 7m new trees in the next 7 years to cool the city down and reduce pollution? Milan's mayor is planning to plant a "mere" 3m trees. Let's beat them! Any takers?"

Nakumbuka RC Makonda alianza vizuri kwenye kampeni yake ya #MtiWangu kipindi fulani. Turejee na ile plan tena kwa ukubwa wake.

Wananchi nao washirikishwe na ikibidi liwe ni zoezi la lazima tena lisimamiwe hata kwa viboko (sina uhakika kama natania hapa au la).

Upandaji miti uendane na utunzaji wa mazingira kwa sheria kali consistently.

Hapa naandika huku nasweat.
Wewe,Eyakuze hamjasoma CLIMATOLOGY!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom