Baada ya Serikali kupeleka wrong message kwa wananchi , hapa majuzi nimeona malalamiko makubwa lakini wafanya biashara toka mikoani waliambiwa walete mali zao na zitanunulika .Sijajua kama makubaliano ya wahudhuriaji wa Sullivan yalikuwa hayo na Serikali ama JK na serikali yake walitaka ku boost PR.
Habari ambazo zimenifikia muda huu ni kwamba juzi Mary Nagu alizuiwa na wananchi wamejawa na hasira wanalia na hasara kubwa na yeye akasema hana majibu ila malalamiko yao kama kawaida atayapeleka kwa wakubwa zake.
Wananchi walizidi kuchonga na akazuiwa kabisa kutoka nje hadi FFU walipo itwa na kuja kumwaga mtama kama kawaida yao bila ya kuuliza .
Wananchi wake wakaambiwa kwamba jana JK angalitokea kuja kusema nao lakini wamekaa hadi usiku JK akiwa kesha jikata mikoani na kuwaacha wakipiga miayo bure bila taarifa ya Rais kuingia ndani ya uwanja wa Nanenane ambako wamekusanywa huko .
Pinda pekee alitia timu siku ya pili ya mkutano na kama kawaoda yake aliingia kikulima na si kisiasa so hakusema lolote .
Jana watu walianza kufungasha maana wanalia na hasara na gharama kubwa waliyo ingia baada ya kupewa matumaini ya kuvuna mapesa.
My take ni kwamba Sullivan imeleta hasara na kama faida basi itakuwa kwa akina Rostam and the likes .Sullivan itakuwa imeongeza madhara makubwa badala ya ku heal majeraha .
Walio pata hasara wana wajibu sasa wa kuomba wananchi kuamua kwa kura zao majimboni na kwa rais ili kukomesha usanii na PR boosting .
Hii ndio Tanzainia bwana
Yaani shida zote, lakini utamkuta jamaa kila saa anakenua meno tu na kujichekesha mbele ya wenye naz, bila kufikilia kuwa hili 80% 75% ni maskini hawana lolote na wako katika hali mbaya ambayo haikumpasa kukaa akikenua meno kila wakati, Hii inadhihilisha kuwa anaona sawa tu waTz kukaa maskini
Kweli zaCommedy tumempata na kazi tunayo hapa
............. ?
.....wakuu nilikuwa pale kwenye pilika muda wote huu ..ndio kwanza nafungasha kurudi milimani kwetu...the fact ni kuwa mkutano ulikuwa mzuri kwenye upande wa kuibua hoja mpya juu ya ndugu zetu walio mbali na sisi...lakini kibiashara madhara au faida yake si rahisi kuonekana haraka.
nadhani serikali kuna kitu inashindwa kuwaambia wanaanchi ukweli...MAONYESHO YA BIASHARA NI KAMA MATANGAZO NA KWA NAMNA YOYOTE SIO MADUKA AMBAYO YATAWEZA KUMFANYA MJASIRIAMALI ARUDISHE PESA YAKE NDANI YA WIKI MOJA!! NO WAY...maonyesho ya biashara sio mahali pa kuuza na kununua...bali ni mahali pa kupata miadi ya kibiashara......hii mentality lazima iondolewe kwa wajasiriamali....kama hawana uwezo wa naweza kushauriwa kushiriki kama vikundi vya uzalishaji mali ili hata wakipata oda kubwa waweze kuzalisha...kwenye yale maonesho kuna mama alikuwa na nguo nzuri za asili..nilimuuliza nikihitaji nguo 2,000..ataweza kunipa kwa muda gani...alisema hataweza mpaka apate mtaji na hata akiwa na mtaji ana uwezo wa kuzalisha 5 kwa siku....ukweli ni kuwa huwezi kupata ODA ndogo kama utabahatika kupata oda ya marekani...watahitaji nyingi zenye kiwango sawa.
JANA SAA 9 HADI SAA 12 ..RAIS ALIPATA MUDA WA KUPITA KILA BANDA LA MJASIRIAMALI AKIWA NA NAGU.....TATIZO NI KUWA SIDHANI KAMA WAJASIRIAMALI WAMEPATA SULUHISHO JUST KWA KUWA WAMETEMBELEWA NA RAIS....BUSINESS PROBLEM NEED A BUSINESS SOLUTIONS...
UKUACHA TATIZO LA WAJASIRIAMALI ..MKUTANO WAS FAIR..NA HATA WAMAREKANI [IN DIASPORA]..WAMEKIRI KUFURAHIA MUDA WAO PALE ARUSHA ..WANAONDOKA NA POSITIVE ALTITUDE!
........MWANAKIJIJI YOUR RIGHT ...kwenye ule mkutano nilipenda speech ya kibaki ..it was a straight forward speech..wale jamaa hata kama ni kwekeza ilionesha interest yao kuwa ni IT,ENERGY ,INFRASTRACTURE,na viwanda ...also TOURISM....sasa kibaki hotuba yake yote alitumia kuelezea maeneo nchini kwake yaliotayari kwa uwekezaji akielezea specific projects...mfano aliuombea kwa jina mradi wake wa EAST AFRICA OPTIC [UNDER SEA ] CABLE ...ambako utaboresha IT...ets...
we neeeded yale maonesho at least yangeshirikisaha watu kama TANZANIA SCIENCE COMMISSIONS[waje watangaze proposals zao]..watu kama TUME YA MAWASILIANO,TPDC ..TANESCO ets...serikali ingbeba jukumu la kuwa ku subsidize hawa wajasiriamali wote ...ambao ushiriki wao unhgekuwa na dhana ya ECOTOURISM.....kwa mfano kila mjasiriamali angetakiwa kulipwa kiasi cha pesa ili kumuwezesha ...kwa mfano kila mshiriki angepewa hata milioni moja ...hatungeshindwa kudhamini wajasiriamali 100 kama nchi kutoka tamaduni zote ..ili kuwaonesha wageni ddiversity ya bidhaa za utamaduni wetu!
Inawezekana watawala wetu wameshajua mahali pa kutugusa tukatulia ni kama unavyomkuna paka kichwani mpaka anasinzia. Kutoa ahadi zisizo na ukweli kisha kuwaingiza watu katika usumbufu na hasara ni ufisadi wa aina yake...Tatizo watu wetu hawayaoni haya 2010 hao hao utawaona na Green & Yellow eti namba 1....
bado tuko usingizini...
Lunyungu,
..wa-Tanzania kila kitu tunataka kulaumu serikali.
..hivi haiwezekani kwamba hizo bidhaa zimewadodea kwasababu ni mbovu?
..kuna mtu amejiuliza hao wananchi wenye malalamiko walikuwa wakiuza bidhaa gani, na za kiwango kipi?
..wakati mwingine kila mtu abebe msalaba wake.