Sullivan: Serikali yawatapeli wananchi waziri afungiwa FFU wajimwaga

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Baada ya Serikali kupeleka wrong message kwa wananchi , hapa majuzi nimeona malalamiko makubwa lakini wafanya biashara toka mikoani waliambiwa walete mali zao na zitanunulika .Sijajua kama makubaliano ya wahudhuriaji wa Sullivan yalikuwa hayo na Serikali ama JK na serikali yake walitaka ku boost PR.

Habari ambazo zimenifikia muda huu ni kwamba juzi Mary Nagu alizuiwa na wananchi wamejawa na hasira wanalia na hasara kubwa na yeye akasema hana majibu ila malalamiko yao kama kawaida atayapeleka kwa wakubwa zake.
Wananchi walizidi kuchonga na akazuiwa kabisa kutoka nje hadi FFU walipo itwa na kuja kumwaga mtama kama kawaida yao bila ya kuuliza .

Wananchi wake wakaambiwa kwamba jana JK angalitokea kuja kusema nao lakini wamekaa hadi usiku JK akiwa kesha jikata mikoani na kuwaacha wakipiga miayo bure bila taarifa ya Rais kuingia ndani ya uwanja wa Nanenane ambako wamekusanywa huko .

Pinda pekee alitia timu siku ya pili ya mkutano na kama kawaoda yake aliingia kikulima na si kisiasa so hakusema lolote .

Jana watu walianza kufungasha maana wanalia na hasara na gharama kubwa waliyo ingia baada ya kupewa matumaini ya kuvuna mapesa.

My take ni kwamba Sullivan imeleta hasara na kama faida basi itakuwa kwa akina Rostam and the likes .Sullivan itakuwa imeongeza madhara makubwa badala ya ku heal majeraha .

Walio pata hasara wana wajibu sasa wa kuomba wananchi kuamua kwa kura zao majimboni na kwa rais ili kukomesha usanii na PR boosting .
 
Baada ya Serikali kupeleka wrong message kwa wananchi , hapa majuzi nimeona malalamiko makubwa lakini wafanya biashara toka mikoani waliambiwa walete mali zao na zitanunulika .Sijajua kama makubaliano ya wahudhuriaji wa Sullivan yalikuwa hayo na Serikali ama JK na serikali yake walitaka ku boost PR.

Habari ambazo zimenifikia muda huu ni kwamba juzi Mary Nagu alizuiwa na wananchi wamejawa na hasira wanalia na hasara kubwa na yeye akasema hana majibu ila malalamiko yao kama kawaida atayapeleka kwa wakubwa zake.
Wananchi walizidi kuchonga na akazuiwa kabisa kutoka nje hadi FFU walipo itwa na kuja kumwaga mtama kama kawaida yao bila ya kuuliza .

Wananchi wake wakaambiwa kwamba jana JK angalitokea kuja kusema nao lakini wamekaa hadi usiku JK akiwa kesha jikata mikoani na kuwaacha wakipiga miayo bure bila taarifa ya Rais kuingia ndani ya uwanja wa Nanenane ambako wamekusanywa huko .

Pinda pekee alitia timu siku ya pili ya mkutano na kama kawaoda yake aliingia kikulima na si kisiasa so hakusema lolote .

Jana watu walianza kufungasha maana wanalia na hasara na gharama kubwa waliyo ingia baada ya kupewa matumaini ya kuvuna mapesa.

My take ni kwamba Sullivan imeleta hasara na kama faida basi itakuwa kwa akina Rostam and the likes .Sullivan itakuwa imeongeza madhara makubwa badala ya ku heal majeraha .

Walio pata hasara wana wajibu sasa wa kuomba wananchi kuamua kwa kura zao majimboni na kwa rais ili kukomesha usanii na PR boosting
.

... your take is my take tooo....
Sisi tulio mbali tuliyaona ktk Chanel Ten ingawa ITV haiukuonesha ambapo huwa inaedit sana habari zake ila vyombo vya kizalendo hutoa kila kitu ili kuipa changamoto serikali.....
 
Mahesabu usishangae ndiyo ukweli huu .FFU walimwagwa kumuona waziri kufungiwa atoe maelezo kwa nini waliwadanganya .JK jana kila mtu alimtegemea kujimwaga aongee na wahanga wa Sullivan lakini akalala mbele na hali halisi ndiyo hiyo .Aliye bahatika ni Rostam na kundi lake na si akina mimi huku .

Ukiingia muda huu nane nane utajionea watu walivyo choka na wengine waliondoka jana kurudi mikaoni na wengine ndiyo wanafungasha sasa baada ya kujua kwamba Sullivan haikuwa yao .
 
Hii ndio Tanzainia bwana
Yaani shida zote, lakini utamkuta jamaa kila saa anakenua meno tu na kujichekesha mbele ya wenye naz, bila kufikilia kuwa hili 80% 75% ni maskini hawana lolote na wako katika hali mbaya ambayo haikumpasa kukaa akikenua meno kila wakati, Hii inadhihilisha kuwa anaona sawa tu waTz kukaa maskini

Kweli zaCommedy tumempata na kazi tunayo hapa

mkuu hii ni kali
 
huwezi kusema sullivan ina maslah kwa taifa kama wengine walivo dhani, mimi zamani niliita sulivan kama Jubilee au kongamano la kumkumbuka bwana suluvan ambayo target point ilikuwa ni kujijengea maslah na umarufu kwa kupitia kwa wanyonge afrika,kupata wanachama wa kudumu,wakiwa wenyewe ndo wadhamini ili k create xposure kwao km NMB,VODACOM lakini si mlima korosho MTWARA, AMBAO WENGI WAO WALDHANI NEEMA KUMBE........... MIMI NAFIKIRI KUNA KIONGOZI HASDA HAPA TZ ANATAKA KUWA`KAMA SULIVAN, YAN AKUMBUKWE KM MKOMBOZI WA SIFA AU KAMA RAIS WA AFRIKA Lakini asiye tambua kutandika kitanda vizuri asbh anapolala lkn aonekane nadhifu nje .NIPENI URAIS MIMI NTAANZA KUTANDIKA KITANDA CHANGU THEN NITAANZA KUVAA SUTI NIKITOKA
 
Madafa maneno yako machache lakini weighs heavy.Nimekuelewa na hil ndilo tatizo la viongozi kusema uongo kila kukicha na kujitafutia umaarufu .Sasa wacha tuje tuelezwe tumepata faida gani .Yaani hata waandishi wetu wao wanakimbilia kuandika tu kusifia bila ya kuhoji faida baada ya mkutano .Bush kaja hata nangoja kusikia tulifaidika nini ama hata kama Dunia imeweza kuelewa kwamba Tanzania ni Nchi mojawapo Duniani.Kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
jamani 2010 tujitahidi kuchagua viongozi siyo watawala la sivyo ya kimbari yakianza hakuna wa kulaumiwa. haya yanayotoea sasa hivi hayahitaji elimu ya juu hata mwenye akili ya kuzaliwa anaelewa la muhimu tujipande vyema.
 
Haya mambo tuliyaona tangu mwanzo,the summit is categorically designed to benefit the few ones,huyo Andrew Young mwenyewe anaonekana tapeli fulani hivi,pia hata ukitazama kwa undani malengo hasa hayakuwa kuwafikia sisi kina yakhe,wakufaidika ni kina Mengi (matangazo),RA na kundi lake na VodaCom,CRDB basi...hao wanyonge walitumiwa tu kuboost PR ya Sullivan ili next time Sullivan Summit ikienda Rwanda wapate samaki wengi...hebu jiulize tu watoto wa shule walikuwa wanatafuta nini?Interest yao ni nini katika Summit?Sullivan wala sion among the intl. orgs. chini ya UN system ambazo angalu hutoa misaada kwa watoto,chakula,afya etc.

Sullivan ni intl. ngo ya wajanja wachahche tu ambao wameona kuna nafasi ya kuinyonya Afrika kupitia viongozi wapenda PR kama JK...
 
.....wakuu nilikuwa pale kwenye pilika muda wote huu ..ndio kwanza nafungasha kurudi milimani kwetu...the fact ni kuwa mkutano ulikuwa mzuri kwenye upande wa kuibua hoja mpya juu ya ndugu zetu walio mbali na sisi...lakini kibiashara madhara au faida yake si rahisi kuonekana haraka.

nadhani serikali kuna kitu inashindwa kuwaambia wanaanchi ukweli...MAONYESHO YA BIASHARA NI KAMA MATANGAZO NA KWA NAMNA YOYOTE SIO MADUKA AMBAYO YATAWEZA KUMFANYA MJASIRIAMALI ARUDISHE PESA YAKE NDANI YA WIKI MOJA!! NO WAY...maonyesho ya biashara sio mahali pa kuuza na kununua...bali ni mahali pa kupata miadi ya kibiashara......hii mentality lazima iondolewe kwa wajasiriamali....kama hawana uwezo wa naweza kushauriwa kushiriki kama vikundi vya uzalishaji mali ili hata wakipata oda kubwa waweze kuzalisha...kwenye yale maonesho kuna mama alikuwa na nguo nzuri za asili..nilimuuliza nikihitaji nguo 2,000..ataweza kunipa kwa muda gani...alisema hataweza mpaka apate mtaji na hata akiwa na mtaji ana uwezo wa kuzalisha 5 kwa siku....ukweli ni kuwa huwezi kupata ODA ndogo kama utabahatika kupata oda ya marekani...watahitaji nyingi zenye kiwango sawa.

JANA SAA 9 HADI SAA 12 ..RAIS ALIPATA MUDA WA KUPITA KILA BANDA LA MJASIRIAMALI AKIWA NA NAGU.....TATIZO NI KUWA SIDHANI KAMA WAJASIRIAMALI WAMEPATA SULUHISHO JUST KWA KUWA WAMETEMBELEWA NA RAIS....BUSINESS PROBLEM NEED A BUSINESS SOLUTIONS...

UKUACHA TATIZO LA WAJASIRIAMALI ..MKUTANO WAS FAIR..NA HATA WAMAREKANI [IN DIASPORA]..WAMEKIRI KUFURAHIA MUDA WAO PALE ARUSHA ..WANAONDOKA NA POSITIVE ALTITUDE!
 
Phillemon... tulituma ujumbe wa wafanyabiashara alipokuja Rais NY what did we get from there? Tumeshikiri maonesho makubwa tu ya biashara Ujerumani, Ufaransa n.k Ni kwa kiasi gani tunapata marejesho mazuri? Kwa kuangalia kundi la watu waliokuwapo pale unaweza kusema walikuwa ni wawekezaji wanaoweza kuwekeza kwenye barabara, simu, teknolojia, sayansi n.k?

Na umesema kitu muhimu sana.. kama huu mkutano ulikuwa na lengo la kufanya contacts kwanini serikali iwashawishi hawa wahangaikaji toka Zenji na mikoano kuja huku na vitu vyao kana kwamba wamekuwa maonesho ya "Saba Saba"? Sasa wanapoondoka wakiwa disappointed (kidogo walichokuja nacho hawakukiuuza, na kikubwa walichatarajia kupata hawakupata) tutawalaumu kweli? Kwanini katika mambo haya ya kuinua wajasiriamali wetu tunaangalia nje ya nchi yetu zaidi wakati tuna soko la Afrika ya Mashariki la karibu watu milioni 120... ?

Hadi pale tutakapoweza kuconsume karibu asilimia 80 ya vile tuvizalishavyo ndivyo tutakavyokuwa na economic dependence and the flood of prosperity itakapofunguliwa kwetu...
 
...........mengi Pamoja Na Kuwa Moja Ya Wadhamini ..hakuwepo Kabisa ..hii Si Kawaida ..may Be Ana Matatizo Au Alikuwa Na Miadi Ya Maana Zaidi...

Mwakani Mkutano Rwanda ....other Notable Absentee Was Uganda ...uganda Ni Nchi Pekee Ya Jirani Ambayo Haikutuma Mwakilishi Wa Maana Kwenye Mkutano Ule...sidhani Hata Kama Yule Head Wa Delegation Ya Alikuwa Hata Balozi Wao Hapa ......nadhani Alikuwa Ni Afisa Tu....[?????????]
 
........MWANAKIJIJI YOUR RIGHT ...kwenye ule mkutano nilipenda speech ya kibaki ..it was a straight forward speech..wale jamaa hata kama ni kwekeza ilionesha interest yao kuwa ni IT,ENERGY ,INFRASTRACTURE,na viwanda ...also TOURISM....sasa kibaki hotuba yake yote alitumia kuelezea maeneo nchini kwake yaliotayari kwa uwekezaji akielezea specific projects...mfano aliuombea kwa jina mradi wake wa EAST AFRICA OPTIC [UNDER SEA ] CABLE ...ambako utaboresha IT...ets...

we neeeded yale maonesho at least yangeshirikisaha watu kama TANZANIA SCIENCE COMMISSIONS[waje watangaze proposals zao]..watu kama TUME YA MAWASILIANO,TPDC ..TANESCO ets...serikali ingbeba jukumu la kuwa ku subsidize hawa wajasiriamali wote ...ambao ushiriki wao unhgekuwa na dhana ya ECOTOURISM.....kwa mfano kila mjasiriamali angetakiwa kulipwa kiasi cha pesa ili kumuwezesha ...kwa mfano kila mshiriki angepewa hata milioni moja ...hatungeshindwa kudhamini wajasiriamali 100 kama nchi kutoka tamaduni zote ..ili kuwaonesha wageni ddiversity ya bidhaa za utamaduni wetu!
 
Phillemon.. lakini tulijua juu ya uwepo wa Summit hii Arusha karibu mwaka mmoja kabla..... Nani alikuwa anashughulikia kuuandaa?
 
Inawezekana watawala wetu wameshajua mahali pa kutugusa tukatulia ni kama unavyomkuna paka kichwani mpaka anasinzia. Kutoa ahadi zisizo na ukweli kisha kuwaingiza watu katika usumbufu na hasara ni ufisadi wa aina yake...Tatizo watu wetu hawayaoni haya 2010 hao hao utawaona na Green & Yellow eti namba 1....

bado tuko usingizini...
 
bado tuko usingizini...Kwa maneno haya kula nane Kipanfa na 2 baadaye .Nani aliwaroga Watanzania ? Huu ni uharamia wa hali ya kuu kucheza na feeligs za watu mwishowe kwenye mali na maisha yao .
 
Lunyungu,

..wa-Tanzania kila kitu tunataka kulaumu serikali.

..hivi haiwezekani kwamba hizo bidhaa zimewadodea kwasababu ni mbovu?

..kuna mtu amejiuliza hao wananchi wenye malalamiko walikuwa wakiuza bidhaa gani, na za kiwango kipi?

..wakati mwingine kila mtu abebe msalaba wake.
 
JOka Kuu soma vyema kwa nini Serikali inaingia lawamani .Ni kwa taarifa za kusema pelekeni bidhaa lipieni mkauze wanakuja wawekezaji na bidhaa mtauza na si mkaonyeshe katika ubora na kutafuta contact for later treading .Hapa ndipo nasema Serikali inaingia lawama .Ukiwasikia wananchi wanasema na kulia ni kwamba they were told to bring for sale na si kuonyesha .Hebu rudi mtaani kama uko TZ utasikia then uje .

Lakini hata hivyo nauliza huyu Sullivan anakimbilia Africa means kuwasaidia weusi .Je kule US kafanya nini kwa weusi kabla hajalet magic zile zile Africa ?
 
PM alichokiongelea naona kama vile watanzania walikaa kwenye mbwembwe sana za kuandaa mkutano lakini dhana kamili ya Mkutano huo walikuwa hawakuielewa. Ndio maana naona umeona Kibaki ameweza kutoa speech nzuri hata zaidi ya waandaaji.

Nafikiri bado katika serikali yetu naona kila jambo linafanyika kisiasa siasa badala ya utaalamu.

Waandaaji wameweka sana nini watapata kutoka kwenye Mkutano huo kwa maslahi binafsi na siyo taifa kwa ujumla. Sasa angalia unawaleta watu wenye uwezo wa mitaji mikubwa halafu unamleta mjasiliamali ambaye hana uwezo hata wa ku-supply nguo 10, kweli hiyo planning ina maana gani?
 
Back
Top Bottom