DOKEZO Sukari inauzwa madukani Tukuyu ikiwa haina maandiko yoyote, haija ‘expire date’ wala utambulisho kuwa inatoka wapi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yaani hata Mimi nimeshangaa Sana, issue sensitive kama hii alaf watu wanajibu kwa dhihaka, kwa akili za namna hii ndio maana serikali inafanya inavyotaka na hakuna hatua zozote zitachukuliwa

Hii mada ingekuwa ya namna ya kumfikisha mwanamke kileleni au namna ya kuunganisha mabao bila kupumzika ungeona namna watu wanavyotiririka humu

So sad 😢
et wanavyotiririka humu , mkuu umenifurahisha.
 
Huyu atakua katoka daslm sisi tushazoe kutumia Sukari kutoka Malawi miaka nenda rudi wanatoa Malawi ikiwa kwenye viroba inakuja kufungwa kwenye mifuko ukiinunua kwa hiyo unataka Sukari ya Tukuyu itoke Morogoro muda mwingine utasikia sijui wameficha sukari hicho kitendo Tukuyu au Kyela hakuna braza ukifika sehemu nenda na beat ya muziki...
Je, unafahamu kwamba Serikali ya Tz na Serikali ya Malawi Zina mgogoro wa mpaka ktk Ziwa Nyasa/Ziwa Malawi?Vipi kama Malawi itaamua kuanzisha Opereshenie ya Siri na ya kimya kimya ktk kutatua mgogoro huo 'kwa kutumia mbinu za medani' huku 'sukari' hiyo ikitumika kama silaha yake??? Je, wananchi watawezaje kuepushwa na janga la namma hii ikiwa sukari yenyewe inaingizwa kwa magendo kwa kupitia 'njia za panya???????
 
Je, unafahamu kwamba Serikali ya Tz na Serikali ya Malawi Zina mgogoro wa mpaka ktk Ziwa Nyasa/Ziwa Malawi?Vipi kama Malawi itaamua kuanzisha Opereshenie ya Siri na ya kimya kimya ktk kutatua mgogoro huo 'kwa kutumia mbinu za medani' huku 'sukari' hiyo ikitumika kama silaha yake??? Je, wananchi watawezaje kuepushwa na janga la namma hii ikiwa sukari yenyewe inaingizwa kwa magendo kwa kupitia 'njia za pants.'??????
Daah aisee Wanasiasa hao hapo Karonga Watanzania wamejaa hapo na wanaongea kinyakyusa tu...
 
Ishu sio kukolea ishu usalama wako kiafya. Acha kufakamia. Sheria za usalama wa bidhaa ziko wazi utajua vipi tarehe ya ku expire kama haijaandikwa chochote? Tafakari
Kwanza 'ingredients' au 'components' zilizopo kwenye hiyo sukari wanazijua????Hiyo sukari ni ya aina gani kwanza?Kwa sababu zipo sukari za aina nyingi sana hapa duniani.
TBS inapaswa ku-intervene haraka sana huko mpakani ili kunusuru afya za watu ktk nchi hii.
 
Poleni na hatari sana...


Cc: Mahondaw
Yeah ni hatari sana hio.
Hivi hata za madukani wabongo tuna muda wa kukagua lebo zao kweli????? Au zile za kupima tu tukishapimiwa hatuna habariiiiiiii sie haoooo🚶🏻‍♀️🚶🏻‍♀️🚶🏻‍♀️ kutumia hatuna habariiiiiii!😊😊
Ni hatari lo
 
Back
Top Bottom