Wissman
JF-Expert Member
- Dec 12, 2014
- 1,012
- 1,284
Katika hali isiyo ya kawaida tangu mwezi huu wa nne uanze bei ya sukari imepanda ghafla kwa taarifa za kwamba sukari haipatikani. Katika hali ya kushangaza siku ya jumapili nimenunua sukari bei ikiwa kilo moja sh 2200 lakini leo hii nimeenda dukani sukari bei kilo moja ni sh 3000, nikadhani masihara ikabidi niende duka la pili na la tatu hiyo ndio bei. Ikabidi ninunue tuu maana wauzaji wanasema na itapanda zaidi ya hapo maana hakuna sukari kwa wauzaji na wasambazaji wakubwa. Hiyo ni huku Arusha. Vipi upande huo huko