Sukari iliyokamatwa itaanza kugawiwa BURE lini na wapi?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
11,126
39,267
Siku ya juzi Rais wa Tanzania, John Magufuli alisema uhaba wa sukari nchini unatokana na baadhi ya wafanyabiashara kuficha shehena ya sukari kwa makusudi ili waje waiuze kwa bei ya juu, na kuahidi kuwa Shehena hizo zikikamatwa tu, sukari hiyo itagawiwa BURE kwa watanzania
Mpaka kufikia jana, Rais amesema zaidi ya Tani 5000 zimekamatwa zikidaiwa kuwa zilikuwa zimefichwa kwa makusudi.

Sasa wananchi wanauliza ni lini na wapi sukari hiyo itaanza kugawiwa BURE ili wafaidike nayo?
Zipo taarifa zinadai kuwa, mara baada ya sukari hiyo kukamatwa, maafisa wa serikali walitoa amri sukari hiyo ianze kusambazwa madukani na kuuzwa tofauti kabisa na agizo la rais Magufuli.

M
 
Wewe una mikono miwili na Huna tatizo lolote la kuweza kuzalisha Mali, usipende vya dezo , Hiyo sukari itapelekwa kwa wazee, wasiojiweza na ma shuleni
 
Sukari iliyo ghalani kwa mfanyabiashara utasemaje imefichwa? Kigezo gani? Imelipiwa Ushuru utaitaifishaje? JPM apunguze jazba ban afauate sheria za nchi! Tutamchoka sasa hivi! Anaanza kuuz sukari atakuja mafuta then sembe lini atajenga viwanda??
 
Augunanifahamu16128415 said:
Wewe una mikono miwili na Huna tatizo lolote la kuweza kuzalisha Mali, usipende vya dezo , Hiyo sukari itapelekwa kwa wazee, wasiojiweza na ma shuleni
Kwani wewe unanifahamu?
Unajua matatizo yangu?
Unajua nawasemia wananchi gani hasa?

Hoja yangu ni kukumbusha Ahadi ya rais itekelezwe ipasavyo, maana hiyo sukari iliyokamatwa kuna wananchi wanasema kwa sasa wanauziwa, tena wanauziwa kwa bei ya juu, tena kutoka kwa wafanyabiashara wale wale waliokamatwa nayo.
 
Sukari iliyo ghalani kwa mfanyabiashara utasemaje imefichwa? Kigezo gani? Imelipiwa Ushuru utaitaifishaje? JPM apunguze jazba ban afauate sheria za nchi! Tutamchoka sasa hivi! Anaanza kuuz sukari atakuja mafuta then sembe lini atajenga viwanda??
Sukari siyo Biashara huria ndiyo maana si kila mtu atakayeenda kununua Kiwandani
 
Hakuna sukari itakayogawiwa bure kwenye zama hizi ambapo taifa halina hata kiwanda kimoja , may be if the government will imports sugar and provide it freely to her citizens otherwise this is a just drama and jokes . Reserve my words.
 
Kuficha na kuhifadhi kuna tofauti kubwa sana na Mahakama lazima itoe interpretation kuondoa hii ambiguity kwa kuangalia mischief behind creation of this law.
 
Siku ya juzi Rais wa Tanzania, John Magufuli alisema uhaba wa sukari nchini unatokana na baadhi ya wafanyabiashara kuficha shehena ya sukari kwa makusudi ili waje waiuze kwa bei ya juu, na kuahidi kuwa Shehena hizo zikikamatwa tu, sukari hiyo itagawiwa BURE kwa watanzania
Mpaka kufikia jana, Rais amesema zaidi ya Tani 5000 zimekamatwa zikidaiwa kuwa zilikuwa zimefichwa kwa makusudi.

Sasa wananchi wanauliza ni lini na wapi sukari hiyo itaanza kugawiwa BURE ili wafaidike nayo?
Zipo taarifa zinadai kuwa, mara baada ya sukari hiyo kukamatwa, maafisa wa serikali walitoa amri sukari hiyo ianze kusambazwa madukani na kuuzwa tofauti kabisa na agizo la rais Magufuli.

M

Taifa la wapenda vya bure,Mlizoea kupewa t-shirts,kofia,kanga,chumvi na viberiti vya bure wakati wa kampeni,huku mkikaririshwa kuimba na kututukana tuliokataa kuiunga mkono ccm,mliaminishwa kuwa ni wapinzani pekee watakaosomeshwa namba,nanyi mkasahau kuwa tumbo halina itikadi,sasa mnaanza kutamani vya watu.Endelea kusubiri,wajumbe wenu wa nyumba 10 watawapa taarifa ni lini mtaitwa kupewa sukari ya bure.
 
Kwani wewe unanifahamu?
Unajua matatizo yangu?
Unajua nawasemia wananchi gani hasa?

Hoja yangu ni kukumbusha Ahadi ya rais itekelezwe ipasavyo, maana hiyo sukari iliyokamatwa kuna wananchi wanasema kwa sasa wanauziwa, tena wanauziwa kwa bei ya juu, tena kutoka kwa wafanyabiashara wale wale waliokamatwa nayo.
Mkuu ni kweli hoja yako iko sawa kabisa, lakini kweli uliamini tutagawiwa sukari bure!! Mimi nitakuwa wa mwisho kuamini hivyo na nitakuwa wa mwisho kwenda kupanga foleni ya kusubiri sukari ya bure!!!!
 
Tumeshindwa kuwa na sera madhubuti halafu tunaishia kuwalaumu wafanyabiashara. Kuna siku nilisema, tulishindwa kusimamia rasilimali za nchi tukaishia kuwalaumu watumishi wa umma na kuwaita majina ya kuwadhalilisha ilimradi wanasiasa ndio waliosababisha yote haya kwa kuleta sera mbovu na ubabe wa kuingilia utendaji kazi wa watumishi wa umma.

Leo kuna maamuzi yalifanywa na mwanasiasa mmoja ila tunaishia kuwasema vibaya wafanyabiashara, hatutaki kusema ukweli. Dhambi hii itatumaliza watanzania, hakika nawaambieni.

Tukae chini tuangalie nyuma, wapi tulikosea then let's move on before it's too late to rescue the economy of our nation
 
Mkuu ni kweli hoja yako iko sawa kabisa, lakini kweli uliamini tutagawiwa sukari bure!! Mimi nitakuwa wa mwisho kuamini hivyo na nitakuwa wa mwisho kwenda kupanga foleni ya kusubiri sukari ya bure!!!!
Trust me, ukienda wa mwisho kupanga foleni lazima Ukose mgao, teh teh
 
Sitajali sana nikikosa, lakini angalau nitakuwa nimejiridhisha kwamba kuna mgawo wa bure wa sukari...!!! Siamini hizo porojo za jukwaani ndio maana yangu.
 
Back
Top Bottom