SUGU: Tutaendelea kutoka bungeni mpaka naibu spika aache udikteta

OGTV

JF-Expert Member
May 22, 2016
353
167
Akichangia Bungeni kwenye wizara ya mambo ya nje, Joseph Mbilinyi(Sugu) ameongelea kujichanganya kwa Tanzania kuhusu nchi ya Libya ilhali wizara ya mambo ya nje ni nyeti.

Pia Sugu ameongelea sakata linaondelea bungeni la upande wa upinzani kususia vikao vinavyoendeshwa na spika wa bunge, Tulia Ackson.Mwisho Mbilinyi ameongelea suala la uraia wa nchi mbili(Dual citizenship) na misiba inayotokea ughaibuni ikiwemo Andrew Sanga.

Kilichoibuka mitaani: VIJANA WAANZA KULNGANISHA UWEZO WA SUGU NA PROFESSA JAY BUNGENI.
 
Kutoka kwao hakujawahi kuwa na tija hata siku moja

Naomba mnitajie faida zilizopatikana kwa wao kutoka nje
 
Ni kweli kiti kinawaburuza lakini kutoka nje haijawahi kuwa suluhisho. Kutoka huku huku matokeo yake leo hatuna katiba mpya.
 
hizo ni kutuchanganya wananchi maana watawala ni nyie na wapinzani ni nyie pia..
 
hv wananchi wao waliwatuma kutoka nje ya Bunge, sheria ya bunge (130) ina mpa spika mamlaka ya kuhamua kadri anavyo ona inafaa, ukawa wasome sheria za bunge na wazielewe
 
Sasa watajua je udikiteta kaacha kama wanatoka nje? ha ha ha ha

Mie nashauri naibu spika aliongoze bunge kwa mda wote wa miaka 5.
 
Kwani alishakuwa Na mchango gani akiwa ndani.Sugu Ni miongoni kwa mifano mibaya mbali ya expectations kubwa waliyonayo wapiga kura kwa kupata mawazo tofauti Na mbadala matokeo yake wanaenda kuwa wafuasi wa mtu Na kushindwa kufikiri km individual.
 
Kutoka kwao hakujawahi kuwa na tija hata siku moja

Naomba mnitajie faida zilizopatikana kwa wao kutoka nje
Ni kama hivi wewe umejiuliza na umefuatilia kwanini wametoka nje, unakubali kimoyomoyo kuwa chama chetu kinafeli. Vyombo mbalimbali vya kimataifa vimetangaza habari hii kwa dunia na kuiweka nchi yako sehemu fulani kidemokrasia.
 
Kutoka kwao hakujawahi kuwa na tija hata siku moja

Naomba mnitajie faida zilizopatikana kwa wao kutoka nje
Watoke au waingie i do not see any added value, kwani kukaa kwao hutumia takribani tshs 126,720,000 kwa siku na hata wakitoka still wanatumia kiasi hicho hicho
 
hv wananchi wao waliwatuma kutoka nje ya Bunge, sheria ya bunge (130) ina mpa spika mamlaka ya kuhamua kadri anavyo ona inafaa, ukawa wasome sheria za bunge na wazielewe

wabunge pia wanayo mamlaka ya kutoka nje na ndio maana hakuna adhabu pale mbunge/wabunge wanapotoka nje pale wanapokuwa hawakubaliani na maamuzi ya kibabe nahizo sharia zote wabunge wanazijua zaidi unavyo fikiri
 
Back
Top Bottom