Sugu agoma kusoma hotuba ya Upinzani katika Wizara ya Habari baada ya kukuta 80% ya maneno yameondolewa! Naibu Spika ataka isiwekwe kwenye kumbukumbu

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Msemaji wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni katika Wizara ya Habari Joseph Mbilinyi (Sugu) amegoma kuendelea kusoma hotuba yake Bungeni kwa madai kuwa zaidi ya 80% ya maneno yameondolewa katika hotuba yake kuhusu bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Sugu amelazimika kuchukua uamuzi huo leo Alhamisi Aprili 18, bungeni jijini Dodoma, baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kumtaka asisome baadhi ya maeneo yaliyoko katika hotuba yake.

Kwa mujibu wa Dk. Tulia, hotuba aliyotaka kusoma Sugu ilikuwa na mambo yaliyoondolewa baada ya kuonekana yanakiuka kanuni za kudumu za Bunge.

Kabla ya Sugu kuchukua uamuzi huo, alianza kusoma hotuba kupitia katika kitabu alichokuwa nacho lakini baada ya muda mfupi tangu alipoanza kusoma, Dk Tulia alimtaka asiisome bali asome kupitia kitabu kipya cha hotuba yake ambacho wabunge wote walikuwa wamegawiwa.

Kutokana na maelekezo hayo,Sugu alisema hawezi kufanya hivyo kwani kitabu kipya hakina maoni ya kambi yake na hivyo kulazimika kuondoka mbele ya Bunge na kurudi katika kiti chake.

Baada ya kusema hayo Naibu Spika aliruhusu mjadala wa bajeti hiyo uanze huku akisema hotuba ya Sugu isiingizwe katika kumbukumbu za Bunge kwa kuwa Sugu hakusema kama anataka iingizwe katika kumbukumbu hiyo.
 
Kwann serikal isiache watu waongee ili kupunguza ukal na maumivu ya moyo kwa sababu kumfanya mtu kutokuongea kuna mjengea chuki na husda ila lait serikali ingejua kumfanya mtu awe mtumwa mpe Uhuru wa kuongea kwa maana ataongea yote hadi moyo wake utakuwa sawa sawia na kuondoa ule ugonjwa wa sonona mana sonona humfanya mtu kuwa katili kwa kuona hana jipya hajaliwi wala athaminiwi
 
Sugu tuwekee hotuba hiyo mtandaoni. Hao puppets Tulia na ndugai hawawezi kwenda kinyume na matakwa ya puppet master wao ya kulifanya Bunge liwe Bunge DHAIFU/UOZO.
Hum watu wanataka vitu vya matusi na shutuma zisizo na maana ndio akina konki ndio hao na upuuzi wao. Hii nchi lazima maadili yalindwe sio kila MTU anataka aseme hata kama lina upuuzi ndani
 
Acha upuuzi wewe! Kuna maadili kwenye mtandao wa majizi unaongozwa na kubwa la majizi kuanzia Ikulu na kutambaa Serikalini, ccm hadi bungeni?

Wenye maadili wanakwapua trillions za walipa kodi na kisha kuzuia ukaguzi wa CAG Assad?

Acha UZWAZWA!

Hum watu wanataka vitu vya matusi na shutuma zisizo na maana ndio akina konki ndio hao na upuuzi wao. Hii nchi lazima maadili yalindwe sio kila MTU anataka aseme hata kama lina upuuzi ndani
 
Back
Top Bottom