Hayo ni makosa na si hilo tu kuna maneno kama maalumu, maskani, wataalamu, maskini magazeti na watu wasiolewa msingi wa lugha ya Kiswahili huyaandika: maalum, maskan, wataalam, maskin, na kadhalika. Kukosoa na kuwekana sawa ndiyo njia ya kuelimishana.
wewe utakuwa ni yule mpambe wake BaloziWana JF hivi mmeona kwenye taarifa ya habari itv jinsi mbunge wa mbeya mjini alivyojaza mtu kwenye mkutano na wapiga kura wake.?
Wabaya wa sugu mtachonga sana lakini Sugu ni level nyingine. Hata kama watu hawampendi ama wanaona hafai, but anapendwa sana na kuaminiwa sana na wapiga kura wake thats enough. Sugu moto chiniii..
Hivi unajua ni kwa nini hii mikoa ina vurugu? ni kwa sababu wabunge wake nao ni vurugu, hawana busara na zaidi ni VILAZA kwa hiyo bila kufanya hivyo CDM itawatema mwaka 2015. Hujiulizi kwa nini ROMBO, DAR, KIGOMA na kwingine ambako kuna wabunge wa CDMA hakuna vurugu? Hawa ni watu ambao wamekotwa mitaani kwenda kuwa wabunge, so itachukua muda wananchi wa mikoa hiyo kupata maendeleo kwa vile VILAZA wao wanatafuta umaarufu ilil waweze kurudi tena mwaka 2015. Waulize wananchi wa maeneo hayo mpaka sasa LEMA, WENJE NA SUGU wamefanya nini katika majimbo yao mbali na migomo na maandamano.
Nini kushangiliwa, MREMA alisukumwa mwaka 1995 sembuse kushangiliwa. Walimshangilia kama Msanii wa Kizazi kipya siyo kama Mbunge. Wana Mbeya walishamsoma SUGU kuwa ni mpenda sifa , hivyo ni lazima wampe haki yake. Wanajua wazi kwamba pale hawana Mbunge bali msanii
upo akiliKimsingi hii ndo sababu wamemkataa asiwasikilize kwani wao hawakumtuma aongoze MBY bali JK.Kiongozi wanayeona ana uhalali wa kisiasa kujibu na kushughulikia kero zao ni SUGU kwani ndo wana mkataba naye juu ya mustakabali wa maisha na maendeleo yao.KANDORO HANA CHAKE AKAMSIKILIZE JK ALIMTUMA KUFANYA NINI MBY?Kwa kitendo hicho wamechangia dai mojawapo ktk katiba mpya ambalo ni wakuu wa mikoa au majimbo wachaguliwe ili wawajibike kwao.
Mbona unajikanyaga hivyo? mara mmeona alivyokusanya watu, mara wabaya wa SUGU mtachonga, mara hawampendi wanaona hafai. Kumbe hata wewe unajua hafai unawatupia watu mpira. SUGU anajua nini , kukusanya watu siyo kigezo cha kuweza, tulishaona ona wanasiasa wengi wakikusanya watu wakiwemo akina SLAA , lakini ndo kama hivyo wanaweza nini? siasa za hasira, majungu, kashfa majukwaani na kelele za njaa ndiyo kuweza. Halafu ukumbuke kuwa SUGU ni msanii , Watu wengi wanaweza kuwa na Shauku ya kwenda kumuona Msanii na siyo Mbunge.
Nimegundua wengi wanaomponda sugu wanawivu wa kimama, mbona hawakutumwa wengine kama nao walikuwa wanaweza kuwatuliza wananchi
hapo ndipo utaona tafauti ya cdm na ccm ,sugu kaongea na wananchi kwa ujumla ,kandoro kaenda kuongea na waandishi wa habari