Joseph Mbilinyi (Sugu) ni Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa ambaye amewahi pia kuwa mbunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la mbeya mjini.
Balozi
Humphrey Polepole ni wanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye amaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba
Madai
Julai 14, 2025 imeibuka Taarifa ikidai kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) amechapisha taarifa katika ukurasa wake wa X akieleza kuwa Polepole ni mnafki kwani aliyakalia kimya matukio mengi yaliyopita hivyo mtu huyo si shujaa bali ni mnafki wa kupuuzwa.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli.
Ufuatiliaji kwa njia ya maneno muhimu (Keywords search) JamiiCheck imebaini kuwa hakuna taarifa hiyo katika ukurasa wa wa X wa Sugu.
Linaloonekana kuwa ni andiko la Joseph Mbilinyi (Sugu) alilolichapisa katika ukuras awake wa X ni la kughushi na halijachapishwa na mwanasiasa huyo. Katika ukurasa wake wa X hadi kufiki ripoti hii inaandikwa Julai 14, 2025 Sugu hakuwa amechapisha taarifa yoyote inayomuhusu Balozi Humphrey Polepole.
Aidha JamiiCheck imebaini uwepo wa wimbi la Taarifa potoshi zinzomuhusu Balozi Polepole punde tu mara baada ya yeye kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya ubalozi wa Tanzania nchini Cuba Julai 13, 2025.