Suggested 3-Day Serengeti Camping Safari (Domestic)

Suggested 3-Day Serengeti Camping Safari (Domestic)

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
529
Reaction score
1,494
Day 1: Departure from Arusha (au karibu), kufika Serengeti kwa mchana, safari ya mchana (game drive), kulala campsite Serengeti.

Day 2: Siku nzima ya game drives ndani ya Serengeti—uwezekano wa kuona the Big Five, uhamaji mkubwa wa nyumbu na pundamilia (inapotokea), twiga, faru, chui, simba na ndege mbalimbali.

Day 3: Safari ya asubuhi, kisha kurudi Arusha kwa jioni au usiku.

Safari ya siku tatu ya camping Serengeti kwa Watanzania ni nafasi nzuri ya kushuhudia wanyama wakubwa, uhamaji wa nyumbu na pundamilia, simba, chui, tembo na mandhari ya savanna kwa bei nafuu ukilinganisha na wageni wa kigeni. Safari huanza Arusha kuelekea Serengeti, siku ya kwanza hufanyika game drive mchana na kulala kwenye kambi za umma. Siku ya pili hutumika kwa game drives siku nzima ndani ya Serengeti na siku ya tatu asubuhi mapema unapata game drive kabla ya kurejea Arusha. Bei za camping safari hizi kwa Watanzania huwa nafuu zaidi na kwa wastani unaweza kupata kati ya dola 600 hadi 700 kwa mtu kwa siku tatu ukiwa na kikundi, ikiwa ni pamoja na usafiri wa gari 4x4, dereva na mwongozo, chakula, ada za mbuga na kambi. Ukienda peke yako gharama huongezeka lakini ukijiunga na kikundi gharama hupungua sana. Usafiri wa ndani unashauriwa kwa sababu unaleta urahisi na kuokoa gharama. Hii ni nafasi ya kipekee kwa Watanzania kufanya utalii wa ndani na kufurahia urithi mkubwa wa taifa lao kwa gharama nafuu huku wakipata uzoefu wa kambi halisi katikati ya pori la Serengeti.
 

Attachments

  • 1756518625595.jpg
    1756518625595.jpg
    448.5 KB · Views: 34
  • 1756257738856.jpg
    1756257738856.jpg
    546.6 KB · Views: 35

Similar Discussions

Back
Top Bottom