Sudan: Viongozi wa Jeshi wakubaliana na Wananchi kuunda Serikali ya Mseto


Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
6,041
Points
2,000
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
6,041 2,000
Viongozi wa kijeshi nchini Sudan na viongozi wa waandamanaji wamekubaliana kuunda serikali ya mpito, itakayo kuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu, na hatimaye madaraka kukabidhiwa kikamilifu kwa uongozi wa kiraia.


Makubaliano haya yamekuja, baada ya mazungumzo yaliyoanza mwishoni mwa wiki iliyopita kuonekana kuzaa matunda, kutokana na waandamanaji kuendelea kushinikiza kuwa wanataka jeshi liachie madaraka baada ya zaidi ya miaka 30.

Jeshi kupitia Jenerali Yasser al-Atta limesema kuwa makubaliano hayo yatatiwa saini na pande zote mbili ndani ya saa 24 zijazo ili kuanza kutekelezwa.

Aidha, amewahakikishia wananchi wa Sudan kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa kikamilifu ili kufikia matamanio ya raia wa taifa hilo.

Miongoni mwa makubaliano yaliyoafikiwa ni pamoja na bunge kuwa na wabunge 300 huku asilimia 67 wakitoka kwenye vuguvugu la waandamanaji, linalofahamika kama Alliance for Freedom and Change.

Maelfu ya waandamanaji kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa wameendelea kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi, hata baada ya kuondoka madarakani kwa rais wa zamani Omar Al Bashir, wakishinikiza ni lazima wanajeshi waache kutawala.
 
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Messages
3,547
Points
2,000
Age
55
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2013
3,547 2,000
Sawa, lkn akina Bashir na genge lake lazima wafikishwe mbele ya mahakama.
 

Forum statistics

Threads 1,295,680
Members 498,336
Posts 31,219,473
Top