Sudan Kusini kutumia sarafu yake rasmi

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
Siku tatu baada ya kujipatia uhuru wake, serikali ya Sudan Kusini imesema itaanza kutumia sarafu yake mpya kuanzia wiki ijayo.
Kwa mujibu wa waziri wa fedha wa taifa hilo jipya, sarafu ya nchi hiyo ni pauni ambapo itakuwa na picha ya hayati John Garang, aliyeongoza harakati za kupigania uhuru wa nchi hiyo.
Sarafu mpya zinatarajiwa kufikishwa nchi humo katika siku chache zijazo.


Sarafu hiyo itakuwa na thamani sawa na sarafu ya Sudan.
Licha ya kuwa na mafuta mengi, Sudn kusini ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani hususan baada ya vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe.
 
Nina imani fedha zao hazikupelekwa kutengenezwa kwenye kiwanda kilichotengeneza fedha za TZ zinazotoa rangi!
 
Back
Top Bottom