Sudan has 'declared war' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sudan has 'declared war'

Discussion in 'International Forum' started by MaxShimba, Apr 25, 2012.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160


  [​IMG]
  Soko lililoshambuliwa Sudan Kusini

  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema Jamuhuri ya Sudan imetangaza vita dhidi ya nchi yake kufuatia mapigano katika mpaka baina ya nchi mbili.
  Bw Kiir alisema haya wakati akiwa katika ziara rasmi nchini China ambayo ni mteja mkuu wa matufa kutoka nchi hizo.Huku haya yakiarifiwa, ndege za kijeshi za Sudan zimeendelea kudodosha mabomu kwenye maeneo ya mpaka mapema leo asubuhi.
  Taarifa zinazohusiana

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani mashambulio hayo ambapo mtu mmoja ameuawa na wengi kujeruhiwa.
  Mashambulio ya karibuni yametokea katika miji ya Panakwatch,Lalop na kituo cha mpakani cha Teshwin. Sudan Kusini ilipata uhuru wake mwaka jana kufuatia vita vya zaidi ya miongo miwili.

  Hata hivyo taharuki imeendelea kati ya pande mbili hususan tofauti dhidi ya raslimali za mafuta pamoja na mipaka kamili ya maeneo hayo.
  Matamshi ya rais Kiir yametokea wakati akikutana na mwenzake wa China Hu Jintao mjini Beijing ambapo anafanya ziara ya siku tano.
  Kiongozi huyo ametaja ziara yake kama muhimu akisema kwa maneno yake,''wakati jirani wetu Sudan ametangaza vita dhidi ya Sudan Kusini''.
  Kwa upande wake Rais wa China Hu Jintao ametaka pande zote kujizuia na vitendo vya kuhujumu usalama.

  Japo Sudan haijatangaza vita, wadadisi wanasema matamshi ya rais Omar Al bashir ya karibuni yanazua wasi wasi kuhusu kuendelea kwa mapigano.
  Rais Bashir amesema hakuna uwezekano wa kufanya mazungumzo na Sudan Kusini na kuapa kuendelea na harakati za kijeshi hadi pale wanajeshi wa Sudan Kusini na washirika wao waondoke kutoka arthi ya Sudan.


  Taarifa zinazohusiana

  BBC Swahili - Habari - Kiir,''Sudan imetangaza vita dhidi yetu''

   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na wenyewe wa kusini waharakishe waunde air force wasikubali manyanyaso ya Khartoum.
   
 4. Kabaridi

  Kabaridi JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 2,028
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kuna kilio kwa mataifa ya afrika katika kanda ya EA/IGAD kujaribu kutoa suluhisho maana AU na UN wamebaki watazamaji. Ninaona kuwa AU watabaki watazamaji mpaka vitu vitakavoaribika kabisa. Miongo ya vita isirejee tena Sudan Kusini.
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tanzania itasupport upande upi?. Ila JK anawapenda waislam.
   
 6. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haya maoni ya udini ni hatari kwa ustawi wetu tusiyape nafasi.
   
Loading...