Subtitles kwenye movie za Kibongo

Subtitles kwenye movie za Kibongo

Waajiri watu wa "kuwamwagia ung'eng'e".Kweli wanatia aibu "kimataifa".Huwa napotezeaaa... nakwama,dah!
 
Nimepaliwa wakati nikiwa nacheka. Kikohozi kimenianza. Mtoa mada kakimbilia wapi?
 
Kama wamejifunza chini ya mwembe basi wewe umejifunzia kwenye mwembe uliong'olewa likabaki shimo tupu ukaingia humo kujifunza! substitute!!!!!!!!? Ohooo sina mbavu!
mambo yakukosea yapo Sana katika cm hivyo sioni chakushangaza.kikubwa kaeleweka.pole yako ww unayependa ligi.
 
kidhunguuu! hii lugha tunaipenda lakini yenyewe wala haina khabari nasi. jamaa yangu huwa hakawii kusema kocha abadilishe information ya timu.
 
jamani mie huwa sielewi hizi movie za kibongo ni akina nani wale wanaozitafasiri kwa kiingireza. kweli wanaboa mno na kutia aibu

He kumbe kile sio ki inglishi sahihi, maana mi huwa nachukua baadhi ya vimaneno pale naviunganisha kupata sentensi
 
Bongo hakuna sanaa wala wasanii wa muvi, siku wasanii na ma director wakianza kufanya muvi wengi tutapenda. Waacheni hawa wa sasa wauze sura ili mapedeshee wanunue, na wakiume wawe punda wasukume maisha, anyway wanasaidia kuwa keep busy ma house gel
 
kiingereza chake ni zaidi ya mchemsho wa miguu ya kuku wapatikanao tandika davis kona au kwa lulenge na njia panda ya mwinyi.
 
Whatever! lakini mleta mada amegusa kero ya wengi!mi huwa naogopa jirani zetu wakiburudishwa na movie kutoka tz aibu!
 
Habari wakuu

Jamani mie huwa sielewi hizi movie za kibongo ni akina nani wale wanaozitafasiri kwa kiingireza. kweli wanaboa mno na kutia aibu

Na tatizo lao kubwa lipo kwenye kutaka kufanya tafsiri ya neno kwa neno. Waangalie movie za Yoruba. Nadhani wanatafsiri dhana sio neno kwa neno lakini ujumbe unafika kwa wanaongalia lakini hawajui ki Yoruba.

Hata hivyo ni kweli kwamba uwezo wa lugha wa hao wanaotafsiri ni mdogo mno. Ili kupata bidhaa bora, lazima watumie watu wenye uwezo wa kufanya kazi hizo. Ndio maana utakuta movie za kibongo - main character, director, script writer ni mtu huyo huyo. Hii ngumu "kumesa"
 
Back
Top Bottom