Suala la watoto kupakatana kwenye magari ya shule naona si sahihi

Milonji

Senior Member
May 26, 2022
153
494
Salaam wapendwa.

Shule Sasa zinafunguliwa na Wazazi Sasa tunapeleka Watoto wetu Shule.

Sina shida na watoto wa Shule za Msingi za Serikali kwa sababu wanaenda Shule kwa Kutumia usafiri wa umma (Daladala) au kwa miguu.

Hapa nazungumzia watoto wa Shule za Msingi za Mchepuo wa Kiingereza (English Medium) na wanaotumia Usafiri wa Shule (School bus).

Hizi school bus zina mambo yake, naomba Wazazi na Mamlaka husika tufuatilie kwa umakini.

Yaani unakuta basi limejaa kupita Kiasi hadi watoto wamepakatana. Mbaya zaidi watoto wa Jinsia tofauti wanapakatana. Unakuta Kijana amempakata Binti. Hivi hapo watoto hatuwafundishi ufirauni kweli?

Mabasi mengine unakuta Mtoto Mkubwa wa Kiume amempakata Mtoto mdogo wa Kiume. Hivi huku siyo kufundisha watoto tabia za Kifirauni kweli?

Je, Sheria za Usalama barabarani zinaruhusu watoto kupakatana kwenye Mabasi? Wizara ya Elimu, mnaruhusu watoto kupakatana kwenye Mabasi? Wazazi, tunaruhusu watoto wetu wapakatane kwenye Mabasi?

Jamii, tumeruhusu watoto wapakatane kwenye Mabasi?

Kwa hili wadau naomba tupaze sauti zetu ili hatua zichukuliwe.

NB:
Naomba Kuanzia Sasa Wanajamii Forums wote tutakao ona Basi la Shule limebeba Wanafunzi na wamepakatana. Tupaze Sauti zetu kwa kutaja;

1. Jina la Shule

2. Namba ya Gari (Ukiweza)

3. Mkoa ilipo Shule.

4. Wilaya ilipo Shule.

Taarifa hizi zitasaidia Mamlaka husika kuchukua hatua stahiki.

"Change begins with us"
 
Siku hizi watu Wana fikra za ngono ngono tu, zamani ilikua kawaida kusema nampenda Abed Mziba, Mkapa, Pepe Kale nk, siku hizi ukisema hivyo utaitwa shoga, zamani hiyo kupakata watoto ilikuwepo tu, siku hizi tabu
 
Samaki mkunje........

Usipoziba ufa......


Nadhani Mkuu umenielewa. Miaka 10 ijayo na kuendelea tusije kulalamika ushoga umezidi.

Sikia nikwambie wewe sema unataka kuongelea ushoga sema unajificha kwa watoto

Af ushoga sio sifa kwamba kila siku uongelee wewe kama unapenda kufanya fanya sisi hata tukija sikia tutashangaa tu na kukuacha
 
Huku nje washaanza wanataka kuingiza hilo soma katika mitaala ya elimu na hao wa international school wajiandae

Screenshot_20230108-083742.png
 
Salaam wapendwa.

Shule Sasa zinafunguliwa na Wazazi Sasa tunapeleka Watoto wetu Shule...
Mimi nadhani wewe ndio firauni, unawaza ufirani.

Hivi wewe mwanaume mwenzio tu akikukalia miguuni tayari unawaza kumlawiti? Tena kwenye daladala?! Hivi mtu anaweza pata wapi muda wa kutoa dhakaru na kumvua mwenzie, kisha kumuingizia akiwa kwenye daladala? Tena unazungumzia watoto wadogo wa shule za msingi..

Achana hayo mawazo ya kifirauni firauni wewe!
 
Kama ni wavulana kupakata wasichana aaaahh! Mbona fresh tu! Ila wavulana kupakata wavulana ni BIG NO!

Ulaya na Marekani watoto wameshaanza kufundishwa Sodoma na Gomora angali bado wadogo kabisa maskeen... kwa mfano:-

"unawafundisha watoto wadogo maskeen wa miaka 8 kwamba to be a gay it's Okay!... kuwa na hisia na mwanaume wenzako t's very okay! Love is Love!..." WHAT THE https://jamii.app/JFUserGuide IS THAT?!

Au... unawafundisha watoto wadogo maskeen walio kwenye age hiyohiyo ya kujifunza kuanzia kwenye 8 na kuendelea eti "to be a Lesbian is very! Very! Okay!... yaan kupendana na binti/mwanamke mwenzio ni sawa, lakini abortion it's not right!"... Dunia inakwenda wapi?!


Mara kumi (10) wapakatane wajue nafasi zao na uwanamume wao uko wapi! Ni kheri upate kesi mwanao kamtia mimba mtoto wa mtu, kuliko kuitwa kwa kesi ya ushoga tena kabanduliwa au anashiriki kubandua wanaume wenzake... utajisikiaje kama mzazi?!... au uitwe shuleni uambiwe mwanao ana mimba ya mvulana anayedai ana hisia nae na anampenda kwa dhati... au ni bora uitwe na walimu wakushtakie kwamba mwanao kaanza kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja yaani USAGAJI?! Kipi bora wazazi wenzangu?!

Vina hasara ila tutafakari na faida zake.


#TAFAKARi
 
Back
Top Bottom