Suala la tozo kuna makundi mawili yameibuka

Elisha Kigahe

New Member
Aug 16, 2022
3
4
Habari ndugu zangu watanzania na rafiki wa Tanzania. Kumekuwa na makundi mawili yameibuka katika suala hili la tozo. Binafsi naona kundi moja ni Lile la wanafiki na jingine ni Lile la ukweli. Kiuhalisia, kwa Sasa Hali ya maisha imekuwa ngumu kiasi chake. Fedha imekuwa ikipatikana kwa shida Sana na kutumika kirahisi Sana.

Suala la tozo sio baya Kama likiratibiwa vizuri Ila kwa namna hii ya Sasa Hali ni mbaya na inawafanya wananchi wengi kuichukia serikali Yao na viongozi wao.

Sisi ndio tunaishi mtaani, ukweli ni kwamba watu hawaridhishwi na suala la tozo na wanaiona serikali Kama imeshindwa kuwa na mbinu mbadala.

Mimi nadhani serikali itumie wataalamu wake wa Kodi na ushuru kuangalia njia mbadala ya tozo. Tozo zinaumiza jamani dah!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom