Suala la Msumbiji; Umoja Ndani ya Nchi Ukitoweka Jirani Anakuonea

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,335
72,800
Baada ya Uhuru wa Msumbiji 1975 raia wa Tanzania kwa jinsi walivyokuwa wakiheshimika Msumbiji waliweza kuingia na kutoka huko kwa kutumia kadi ya TANU na baadae CCM.
Hii inatokana na juhudi zetu na kujitoa kwa hali na mali kuwasaidia wapigania uhuru wa Frelimo dhidi ya Mreno na umoja na kuheshimiana kwetu ndani ya nchi. Lakini mitafaruku na kubaguana kuliko shika kasi ndani ya nchi yetu kwa sasa na kutufanya sio wamoja kumefanya jirani zetu watudharau na kuwaona Watanzania kama taka taka hata kuwafukuza kama wanyama waharibufu kwani wanajua kwetu hicho hakita shtua wakubwa kwani hakihusiani na kukomoana kwetu. Na ndivyo ilivyo, hakuna anayejali serikalini hata Naibu waziri mambo ya Nje ameonekana kama anaunga mkono kiaina.
Leo ni Msumbiji, kesho yaweza kuwa Kenya,Zambiaau Uganda. Kwa nini? Kwwa vile heshima yetu awamu hii imepotea ndio maana mkuu anasema huko nje hata ukinyongwa shauri yako!
 
Hii ya Msumbiji na ya madawa ziko sawa. Wazamia unga Hongkong au Afghanistan wanajitafutia maisha yao wanajua hatari yake. Yakiwapata walishajitayarisha kunyongwa psychologically; hawahitaji wala hawategemei huruma yetu. Wa Msumbiji nao walienda njia za panya bila kutuaga, wakapeleka madawavya kulevya na petty crimes. Wasitegemee urafiki wavnchi mbili tutakubali uuawe na vibaka kwa kuvuruga nchi za watu. Heshima huzaa heshima, ujambazi hujaa ujambazi, wala wasijilinganishe na mashujaa waliosaidiana na Frelimo kwa vile hawa hawakwenda kumsaidia mtu wameemda kujitafutia maisha kwa njia zisizo halali. Leo tumewaona kwenye TV walo ng'ambo hii wanasora kwenye mahema. Kama huku kweli ni nyumbani kwao na waliaga vizuri wakawa wanarejeshavutajiri baada ya kuchuma kwa nini kila mtu asuende kwake straightbkwenye hekalu?
 
Nakumbuka tulikuwa na TAMOFA (Tz and Mzbq Friendship Association) ilikuwa na ofisi zake pale Mtaa wa Nkrumah (opposite Immigration Club na CoCabs kwa siku hizo). Sijui yenyewe ipo au imeishia wapi. Mwenye taarifa atujuze. Kama sikosei Kuna wakati Mh. Mkuchika alikuwa mmoja wa viongozi wake, nae anaweza kutusaidia.
 
Kuporomoka kwa kasi soko la ajira na ajira pamoja na hali tete ya kimaisha mtaani,kuwaona maadui wafanyabiashara, kuwasingizia kila tatizo wanaleta wao (sukari kupanda bei,kuficha hela,njaa na ukame n.k) na kuwalaani wafanyabiashara ambao wengi ndio waajiri na wawekezaji kumewafanya wananchi wengi wa TZ wakimbilie huko vichakani na mwisho wake wanafukuzwa kwa aibu huku waziri Maige anasubiri maelekezo ya neno la kusema toka kwa mkuu.
 
Upo sahihi Chakaza ndio maana umesikia Waziri Mahiga anawaponda wale kuwa hawana document yeyote hata kujua kuwa ni Watanzania ana majibu mepesi kwenye Jambo zito kwa kuwa hakuna ushirikiano na Raia wake..
 
Anataka document ipi tena huyo mtu? Wahanga wanakwambia kuwa walipokuwa wanakutwa ndo hapo hapo unakamatwa na kutiwa pingu kisha kwenye gari unapandishwa na kupelekwa mahabusu kisha unasafirishwa mpaka mpakani mwa mchi yako.. na kutupwa hapo. Hapo ni kwa wale wenye bahati zao. Wengine walipigwa na akina mama kubakwa.. sasa kwa hali kama hiyo unapata wapi muda wa kukusanya documents zako? Alafu wapuuzi fulani humu wanalichukulia swala kama hili au wanalihusisha na madawa ya kulevya!!! Si ni upuuzi uliyovuka mipaka ya kibinadamu huyo!!? Pu....mba...aaaaaaaaa......vu... kabisa.. watu kama hao. Ukweli ndo huo, kama hauna mshikamano ndani yako basi adui hutumia mwanya huo kukunyanyasa.. Hapa Tz wapo raia wa Msumbiji kibao hasa mikoa ya kusini huko, vipi raia wetu wakisema kama mbwai na iwe mbwai? Patakalika hapo?
 
Uko sahihi mkuu, bado ukweli unabaki kuwa hapa ndani ya nchi hatusaminiani wenyewe na majirani wamegundua hivyo nao hawatuthamini.
Kwani Msumbiji hawajui kuwa Wamakonde wamejaa tele hapa na huko Kenya wanachonga vinyago?mbona wasitumie mbinu za kihamiaji kudili na hao wahamiaji haramu badala ya kutumia uhuni na ukatili?
Hizo ni dharau kwa rais Magufuli na serikali yetu
 
Wamejjua sana kuw nchi imevurugwa na hatuna umoja wala hatuna vision tena kama nchi!!! Wamejua aliepo sasa ana kazi moja tu ya visasi hana mtazamo wa mbali sana wanajua kuwa lolote wafanyalo hana uwezo nalo wala hajui diplomasia inasemaje kwa hilo! Ni dharau sababu Wamejua hatuna umoja tena
 
Kwani kwenye kuomba kuchaguliwa nilisema wanaoishi malawi ntawasaidia japo kwa diplomasia? Nilisema? Kama mmefukuzwa mi niapokee mizigo yenu mpakani?.

Ndiyo sababu tunataka viongozi wenye sifa za uongozi, wanaojua maana ya kuwa viongozi wa kitaifa, wenye moyo wa uongozi na wanaojali. Uongozi siyo ushereheshaji. Kwa manatiki hii, ni dhahiri Tanzania muda si mrefu kitakuwa kitu kingine. Uongozi ni uzazi. Lazima viongozi walinde haki na maslahi ya Watanzania kokote kule duniani waliko. Wanatumia kodi zetu na wanapashwa kuliheshimu hilo.
 
Anataka document ipi tena huyo mtu? Wahanga wanakwambia kuwa walipokuwa wanakutwa ndo hapo hapo unakamatwa na kutiwa pingu kisha kwenye gari unapandishwa na kupelekwa mahabusu kisha unasafirishwa mpaka mpakani mwa mchi yako.. na kutupwa hapo. Hapo ni kwa wale wenye bahati zao. Wengine walipigwa na akina mama kubakwa.. sasa kwa hali kama hiyo unapata wapi muda wa kukusanya documents zako? Alafu wapuuzi fulani humu wanalichukulia swala kama hili au wanalihusisha na madawa ya kulevya!!! Si ni upuuzi uliyovuka mipaka ya kibinadamu huyo!!? Pu....mba...aaaaaaaaa......vu... kabisa.. watu kama hao. Ukweli ndo huo, kama hauna mshikamano ndani yako basi adui hutumia mwanya huo kukunyanyasa.. Hapa Tz wapo raia wa Msumbiji kibao hasa mikoa ya kusini huko, vipi raia wetu wakisema kama mbwai na iwe mbwai? Patakalika hapo?
Safi sana mi naona tuanze tu make kuna wa Malawi wengi hapa Tz na wengine hadi Kwenye taasisi za serikali
Japo nakumbuka na WanayaRwanda tuliwafanyia hivi hivi!
 
Mimi mpaka muda huu niko huku huku Montepuez -Mozambique
Ishu iko hivi sisi wengi wetu tulio baki Tuko huku kabla hata huo MGODI wa Madini hauja anza yaani tulikuwa tulikuwa tunafanya biashara kama kawaida
Hao waliorudishwa walikuwa wanashughurika na Ishu ya Madini.
Lile eneo la MGODI lipo chini ya mwekezaji. Wao walikuwa wanaingia eneo hilo hilo Kwani huko Tanzania hakuna migodi ambayo ipo chini ya wawekezaji? Ifike hatua tuwe tunaeleza ukweli siyo kuropoka na kueleza vitu visivyo sahihi
IMG-20170219-WA0002.jpg
Hao nao watailend-wazungu wa mawe pia wamerudishwa. Mbona kuna migodi kibao ya dhahabu ambayo haiko mikononi mwa wawekezaji Watu wanachimba hasa wa Tanzania
Hao walikuwa eneo ambalo linapatikana RUBY dini lenye thamani zaidi
 
Mimi mpaka muda huu niko huku huku Montepuez -Mozambique
Ishu iko hivi sisi wengi wetu tulio baki Tuko huku kabla hata huo MGODI wa Madini hauja anza yaani tulikuwa tulikuwa tunafanya biashara kama kawaida
Hao waliorudishwa walikuwa wanashughurika na Ishu ya Madini.
Lile eneo la MGODI lipo chini ya mwekezaji. Wao walikuwa wanaingia eneo hilo hilo Kwani huko Tanzania hakuna migodi ambayo ipo chini ya wawekezaji? Ifike hatua tuwe tunaeleza ukweli siyo kuropoka na kueleza vitu visivyo sahihi
View attachment 473519Hao nao watailend-wazungu wa mawe pia wamerudishwa. Mbona kuna migodi kibao ya dhahabu ambayo haiko mikononi mwa wawekezaji Watu wanachimba hasa wa Tanzania
Hao walikuwa eneo ambalo linapatikana RUBY dini lenye thamani zaidi

Repatriation ni jambo la kawaida sana kama ilivyo suala la watu kuhamia sehemu bila kuzingatia taratibu zote. Tatizo letu lililopo ni kule kuwaua, kuwabaka, kuwachomea nyaraka, kuwanyang'anya mali zao halali, ni kipengele gani cha sheria za kimataifa ama za Mozambique, ama za Tanzania, ama za nchi yoyte ya binadaam (ukiondoa urarabuni ambako ni ushetanini), zinazoidhinisha adhabu hizi kwa binadamu?

Sheria zimempa nani mamlaka ya ku execute hizi hukumu?

Ukimya wa serikali ya Mozambique ni endorsement ya haya mambo?

Ukimya wa seriakl ya Tanzania ni kuafiki na hali hii kwa Wananchi wake walio ugenini?

Kama Tanzania na Mozambique zimeafikiana kuwa persecute Watanzania, bila shaka Watanzania wanapashwa kujua kwamba hawana serikali nahivyo wanapashwa kujilinda. Nini kinachofuata?

Huwezi kutetea unyama dhidi ya binadamu na ukabaki kuw abinadamu kamili.
 
Africa neno Uzalendo lina tafsiri nyingine kabisa ambayo dunia nzima inajua. Uzalendo kwa Africa ni wananchi kuwa royal kwa Serikali tu

Wakati uzalendo ni two way traffic kwamba wananchi anakuwa royal kwa serikali na serikali inakuwa royal wa wananchi mfano hayawezi kuwa mapenzi wakati ww unampenda yeye hakupendi hyo inaitwa ubwege lakini mapenzi ni muunganiko wa upendo kutoka sehemu mbili ndio yanaitwa mapenzi

Leo wenzetu nchi za weupe wapo tayali kutetea raia wao hata kama wamefanya makosa nchi nyingine wako tayali kuongea na nchi hyo ukatumikie kifungo chako ndani ya nchi yako si ugenini

Kwani wanaamini kuwa wakati watu hawatendi uharifu kwa kuwa wenyewe ni waharifu NO wakati mwingine mazingira yanaweza kukulazimisha kutenda uharifu

Haiwezekeni hata siku moja siku serikali ikipata matatizo mnaambiwa wananchi muwe wavumilivu lakini siku wananchi wakipata matatizo Serikali inawambia mtajijua wenyewe hv hapo uzalendo unatoka wapi?

Africa haiwezi kuwa na wananchi wenye uzalendo na nchi zao ndio maana nacheka sana tunapocheza ngoma ya uzalendo kwa kufata midundo wakati hatujui kinachoimbwa wanaojua wanalia machozi kwani nyimbo zile zinatukana mama zetu na vizazi vyetu
 
Baada ya Uhuru wa Msumbiji 1975 raia wa Tanzania kwa jinsi walivyokuwa wakiheshimika Msumbiji waliweza kuingia na kutoka huko kwa kutumia kadi ya TANU na baadae CCM.
Hii inatokana na juhudi zetu na kujitoa kwa hali na mali kuwasaidia wapigania uhuru wa Frelimo dhidi ya Mreno na umoja na kuheshimiana kwetu ndani ya nchi. Lakini mitafaruku na kubaguana kuliko shika kasi ndani ya nchi yetu kwa sasa na kutufanya sio wamoja kumefanya jirani zetu watudharau na kuwaona Watanzania kama taka taka hata kuwafukuza kama wanyama waharibufu kwani wanajua kwetu hicho hakita shtua wakubwa kwani hakihusiani na kukomoana kwetu. Na ndivyo ilivyo, hakuna anayejali serikalini hata Naibu waziri mambo ya Nje ameonekana kama anaunga mkono kiaina.
Leo ni Msumbiji, kesho yaweza kuwa Kenya,Zambiaau Uganda. Kwa nini? Kwwa vile heshima yetu awamu hii imepotea ndio maana mkuu anasema huko nje hata ukinyongwa shauri yako!
kuna ka ukweli fulani.

utaifa na uzalendo nchi hii umekuwa compromised sana kutokana na kuendekeza siasa za kibaguzi.

tuna wasiwasi adui akivamia sasa kanchi kamasikini kama ketu ambako kuna such an unprecedented "political polarization" ni rahisi sana kupata mamluki (wa Kitanzania) wa kutuangamiza sisi wenyewe.
 
Ni kweli kabisa. Hali tuliyokuwa nayo 1979 wakati wa vita ya Kagera dhidi ya Amini sasa hivi haiko kabisa hivyo yale yaliyosababisa kumpiga Amini kwa kupata msaada wa ndani ya Uganda yaweza kutokea hapa kwetu kwa baadhi yetu kumpa ushirikiano adui.
Hili yapaswa kuliangalia sana kama taifakwani sasa hivi sio lazima iwe vita ya silaha tuu bali hata vita vya kiuchumi
 
Back
Top Bottom