Suala la mahari

Thread Starter

JF-Expert Member
Mar 16, 2017
1,370
1,032
Nimefuatilia sana hii mijadala ya usawa wa jinsia. Nimeona wanawake wakipinga vikali mila na desturi zote zinazo wadunisha kimaisha kama wanadamu na kuwafanya waonekane kama "vyombo" au "rasilimali".

Lakini hii desturi moja naona ikiepukwa na wanaharakati hawa, ulipaji wa Mahari. Japo mwanamke anataka aheshimiwe, asaidiwe kazi za nyumba sawia, awe na usemi wa maamuzi sawa na mume nyumbani na kadhalika.... Huyu mwanamke bado anafurahia na kuona ni jambo la sawa kununuliwa kwa Pesa au Mali.!!

Nilipohoji wengi wanasema mahari ni shukrani.... Je kama kweli mume na mke wako sawa, mbona ni mume pekee atoae shukrani wakati wa ndoa.?

Sijui maoni yenu yapi kwa suala hili?

(Samahani kwa kiswahili).
 
Tuheshimu mila lakini tuwe tayari kubadilika.

Ukimpenda mtu ukaambiwa toa mahari kadhaa toa. Bado sijaona ubaya wa kutoa mahari siku nikiona kuna haja ya kutokutoa nitahariri hii post.

ni kweli mkuu hakuna ubaya wa kutoa mahari

ila hawo wa upande wa pili wamegeuza mahari kama mtaji wa biashara

yaaani wao wanataja namba tu utasikia uku kimebhana pua nataka million 7 nyooooooooo
 
Nadhani ni ugumu wa maisha ndio unaochangia watu kuwa na mawazo hasi kwa kila jambo,

wala sio ugumu wa maisha rafiki

unadhani ukitaja mahari ambayo unaamini mpenzi wako anaimudu kunatatizo

hakuna tatizo ata ila nyie ndo mnafanya hili swala liwe gumu kwa kutaka mahari iwe ni thamani ya prado
 
Tuheshimu mila lakini tuwe tayari kubadilika.

Ukimpenda mtu ukaambiwa toa mahari kadhaa toa. Bado sijaona ubaya wa kutoa mahari siku nikiona kuna haja ya kutokutoa nitahariri hii post.
mda muingine hal ngum mkuu
 
Back
Top Bottom