Suala la Machinga, yafanyike haya

Kwani kipindi cha jk, mbona yaliwezekana?meko ndio aliwatia jeuri sana!!walikuwa wakijenga vibanda vinavunjwa, na ukikamtwa ni mahakamani kwani sheria si zipo?serikali ikiamua kwa dhati mbona watakubali tu, mfano kuna masoko yamejengwa yako tupu watu hawaendi huko, eti wanafuata wateja nje!!eti litajitatua lenyewe wakati kila siku ndio linazidi, watu wanajenga mabanda kabisa barabarani, ?!!
 
Jitu katili, think again

 
JPM aliwapa jeuri ipi?

Unajua kwamba wamachinga nao ni raia wa nchi hii?

Kama hijui usiongee, JPM alitoa maelekezo sahihi kabisa hata SSH anajua

Ila na wanaozibiwa maduka yao nao ni raia wa nchi hii, tena wenye mchango mkubwa sana kwa taifa hili kuliko hata huyo machinga!!na kwani kupitia kodi anayolipi ndio ina muhudumia huyo machinga, lakini machinga anapomfanya asifanye biashara yake vizuri nalo ni tatizo!!mfano nenda mbagala unakuta mtu amelipia fremu tena iko pembezoni mwa barabara kuu, lakini kwa mbele kuna kama kambi ya wavuvi ni maturubai tu hata chochoro la kuzifikia hizo fremi hakuna!!mwisho wa siku anafunga biashara tu,
 
Siyo kwamba hawaelewi.
waliingia mjini kwa mbio za mwemge na kuajiriwa kimkakati.
 
Biashara holela ni vurugu. Mama hajasema Machinga wafukuzwe bali wawekwe kwenye maeneo rasmi.
 
Machinga Complex ilijengwa kipindi cha JK na machinga hawakwenda kwa kifupi waligoma
 
Mimi najua maumivu ya maamuzi kama haya,nakumbuka miaka ile mkapa,naamka asubuhi nasikia redioni Mungai afanya kweli,kafuta masomo ya ufundi,wakati huo ndo masomo nayofundisha watoto wapate chakula
 
Machinga ni jini ambalo CCM walilitoa kwenye chupa halafu JPM akaliweka sebuleni kwao. Halitoki, halifi, halidhibitiki.
Bila kuzingatia misingi ya utawala bora na demokrasia CCM hawawezi kutatua hili tatizo.
The HALLMARKS of bad governance:
1. Arbitrariness
2. Ambiguity
3. Capriciousness
 
Your correct, muza nyanza bamia hoho atalipa kodi ipi? Isitoshe kilasiku anapanda daladala linalotumia mafuta yaliyolipiwa kodi, mwingine humu anatumia gari stk ambalo halilipi kodi wala bima
 
Chukua Kariakoo, hilo jengo maalum kufanyia biashara lijengwe mtaa gani? Tupe mfano.
Hayo masoko yaliyojengwa maeneo wanakoishi machinga hao na hawayataki, unataka wapelekewe watu wa aina gani ambao watanunua bidhaa zao.
Nini tofauti ya bidhaa za wamachinga na za wenye maduka?
Hao wamachinga siku zote wanao viongozi wao, hivyo hilo si jipya.
Kigezo cha eti wanatafuta riziki ndicho kinawajengea kiburi, kila mtu mzima mwenye nguvu hutafuta riziki ili aweze kuishi, mwenye duka hauzi sura dukani pake naye anatafuta riziki.
Siasa rahisirahisi ndizo zimetufikisha hapa na zitakuwa mbaya zaidi tuelekeako kwani idsdi yao inazidi kuongezeka kwenye eneo dogo.
 
Mtaa wa Kongo ulienda kutafuta nini? Nawewe ni mmoja wa waliosababisha idadi kubwa ya watu kariakoo
 
Wamachinga waliotapakaa ni raia wa wapi?
Kama ni wa Tanzania acha kuwaangalia wao kama tatizo, kaongee na viongozi walioshindwa kuwaongoza na kuwasimamia
Ikiwa tatizo la machinga halijakuathiri ni rahisi kuzungumza jinsi ambavyo unaweza, Lakini ukweli machinga na JPM wameiharibu inchi, Mamia ya biashara zilizokua rasmi zilifungwa kwa sababu ya kadhia hii machinga, Haiwezekani ulipie kodi za TRA,Vibali vya Halmashauri, Ulinzi shirikishi, tozo za usafi halafu mtu ackachonge tu meza ya mbao aiweke mbele ya Biashara yako, HUU NI UPUMBAVU ULIOPITILIZA.
 
Ulisha jiuliza kwanini machinga hawako masaki wala lugalo?
 

Wameharibu nchi kwa sababu wanaotakiwa kuwasimamia wamekaa maofisini bila kufanya mipango yoyote? Kwani kulikua na gharama gani wahusika kuwapangia sehemu zisizotakiwa kufanya biashara kama zile njia za waenda kwa miguu na kwingineko?

Wewe unashauri tuwapeleke wapi watakapoweza kuishi na kutunza familia zao ili nchi unayosema wameiharibu itengamae??

Kabla ya kuwaza juujuu na kuishia kuwaona machinga tatizo tafuteni mzizi wa tatizo
 
Ulisha jiuliza kwanini machinga hawako masaki wala lugalo?

Watu wavivu hawataki kutumia akiliza kufikiria kabisaaa, badala yake wanaishia kuwaona binadamu wenzao tatizo
 
Machinga haendi China, wenye madukq ndio huwapa bidhaa machinga wakauze jioni wapeleke hesabu, eti mtu hauzi mbona hafungi biashara na frem analipia 10m kila mwaka

Ulishawaji kutana na matangazo ya ajira chapchap hebu fuatilia ni ajira gani kama hautaishia kubebeshwa mabeseni vijiko pasi chupi sindiria soksi.
 
Watu wavivu hawataki kutumia akiliza kufikiria kabisaaa, badala yake wanaishia kuwaona binadamu wenzao tatizo
We Acha tu, huyohuyo anayelalamika jioni anapita hapohapo kuhemea nyanya bamia viazi mviringo, eti hamna sehemu za kutembea alijuaje kama hazipo sialipita akitembea alikuwa anatafuta nini kama sio kuhemea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…