Suala la Korosho: Mbunge Zitto anapotosha umma, JPM kafanya sawia kabisa

1. UZALISHAJI KUPUNGUA:

Uzalishaji ulipungua ulitokana na bad weather na sio vinginevyo. Taarifa ya wataalamu wa Kilimo wa kituo cha Utafiti Naliendele, taarifa ambayo Waziri Mkuu Kasim Majaliwa Majaliwa kaitoa leo mbele ya Mhe. Rais IKULU na Watanzania wengi tumeIsikia kupita vyombo vya habari.

2. ATHARI ZA KIMAPATO:

Waingereza wanasema to every cause there is effect… If we want to change the effect we should change the cause…Athari inaweza kushuka kwa Halmashauri kama taasisi, ila wananchi watapata hela nyingi kuliko halmshauri kama taasisi. Mzunguko wa fedha utakuwepo katika Halmashauri husika, kwani fedha ambazo kila mwananchi atauza korosho kwa Sh. 3,300/kg, fedha hizo zitanunua bidhaa na huduma katika wilaya/halmashauri hiyo hiyo na kwingineko ambako mwenye fedha atapenda.

Value chain ya korosho itafanyikia hapa kwa kutumia kiwanda cha jeshi (BUKO) ambacho leo wamepewa, unlike korosho ghafi ambayo huwa inakuwa exported kwenda India na Vietnam kuwatajirisha wenye viwanda vya huko na sio Tanzania. Kwa kuwa tutakuwa na finished product, export levy itapatikana wakati tunauza korosho iliyoengezwa thamani. Hoja yako pia iko dhaifu.


3. TADB HAINA FEDHA:

Rais sio kwamba hana uhakika wa uwepo wa 660 bilioni ambazo ametaka zitumike kwa ajili ya ununuzi wa Korosho toka TADB. ZZK acha kutuhadaa kuwa Serikali itawakopa wananchi. Korosho itanunuliwa kwa cash sawia na agizo la Rais JPM wewe kama kiongozi hutakiwa kutengeneza fitna na taharuki. Mbunge anakuwa entrusted na diplomatic passport, kwa hadhi hiyo unawajibika kutulia na kuacha executive branch ifanye kazi yake. Kama kwenye execution process utaona madhaifu, utakuwa na fursa ya kuja na hoja ya kokosoa na sio sasa.

Sidhani kama kuna uvunjwaji wa sheria utatokea. Ila kama itatokea ukiukwaji wa sheria, ZZK nenda mahakamani kufungua shauri la uvunjwaji wa sheria. Ikumbukwe, kuna sheria zingine ambazo huwa zina-govern a particlur land huwa ni mbaya; na kama sheria ni mbaya, ikitokea sheria zimekiukwa, sisi hatutakuwa wa kwanza duniani. Wakati wa utawala wa Farao huko Misri, kuna sheria ilipitishwa kuuwa watoto wa kiume kutoka jamii ya Kiyahudi. Familia ya Musa ilikiuka kwa kumficha mtoto Musa ndani kwa miezi 3. Hata baadae alipotupwa mto Nile na kuokotwa na binti Farao, alipata advatange ya kulelewa katika kasri la Farao kwa kukiuka sheria mbaya. Kama kuna fedha ya kununua korosho ipo ndani ya Tanzania, ni vema fedha itumike kwa kununua korosho bei ya sh. 3,300/kg. Hii thamani yake ni kubwa. Kwa kuwa tuna nafasi ya kuzibangua na kuwa na finished product, gharama ya finished product sokoni ni kubwa. Na kwa kuwa tutauza say kwa kg sh15,000; tutakuwa na fedha nyingi za ziada na mkopo utarejeshwa na riba kama ipo.

4. Magari ya Jeshi yatahitaji mafuta na uhakika wa posho na stahiki za wanajeshi wakiwa kwenye zoezi la korosho. Wanajeshi ni wazalendo na wana utayari kuwa sehemu ya zoezi hili lina thawabu kubwa kwa maslahi ya Taifa kuliko wangenunua madalali/walanguzi wengi ambao ni “Watanzania wa asili ya India”. Mwisho wa siku fedha huwa zinabaki kwenye account zao kama sio India au UK na fedha huwa zinakuja tu, msimu wa kununua korosho na sio vinginevyo. Baada ya manunuzi huwa zinabaki kujenga uchumi wa India ni sio Tanzania.

HITIMISHO:

ACT Wazalendo na ZZK walipinga manunuzi ya ndege kwa cash, wakitaka tufuate sheria ya umma manunuzi ambayo mchakato wake ungefanya gharama ya ndege kuwa kubwa zaidi. Ilitumika akili ya kawaida tu, kununua kwa cash. Prof. Kabudi alieleza vyema kuwa hata Mwl. Nyerere aliwahi kununua ndege Uholanzi kwa Cash.

ZZK, bila shaka wewe unaweza kuwa dalali au mtetezi wa madalali na walanguzi wa Koroshi kwa jina la Kongomba. Na bila shaka una hofu ya kutiwa mbaroni na “ma-MP” kwa kuwa una uzani mkubwa wa Korosho au madalali wana uzani mkubwa wa korosho huko kusini. Bila shaka hofu inaongezeka kwa uwoga wa kupoteza maana mkitakiwa kuthibitisha mashamba mnayolima na kuvuna korosho hayapo. Kuna uwezekano, korosho ikawa mali ya JWTZ by default kwa hao “kangomba” maana wakulima walishalipwa na madalali zamani kama wengine wanavyodai.

Ifikie tu wakati, Wizara ya vijana na ajira iwe na mkakati wa kufanya equipment financing kwa vijana na wawe trained kutengeneza finished products za Korosho zinazokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje. TADB na TIB Development bank zinaweza kuwapa mikopo vijana kwa udhamini wa Serikali na kutafuta consultants ambao watawa-guide kuzalisha final product yenye kukidhi global markets.

Mhe. Rais JPM, waamini vijana pia kwenye biashara na watafutie consultants ambao watacheza nafasi ya kuhakisha the processing of final product is made by Tanzania owned industries. Na tokea Tanzania, final product ikiuzika nje ya nchi, itaongeza liquidity na kuongeza fedha za kigeni nyingi tofauti na kuwategemea madalali toka India. Enough is enough

Aluta continua
Well said!!
 
Back
Top Bottom