Suala la CAG: Lugha, Siasa na Taaluma

Suala la CAG: Lugha, Siasa na Taaluma

Nimesikiliza Hii Clip ya Taarifa ya Bunge

Kwa ufupi Mwenyekiti wa Kamati hii anapaswa kuliomba radhi Bunge kwa kulidhalilisha Bunge maana Ni aibu Na fedheha kwa Bunge

Mwanzo Mwisho Taarifa inanukuuu Maneno ya Kamusi kufasiri maana ya neno dhaifu badala ya Yeye kuonesha Bunge sio dhaifu

CAG alishawaambia hajutii kusema Bunge dhaifu na akaahidi Kuwa ataendelea kutumia Maneno hayo kwa Kuwa ndio lugha ya kitaaluma sasa ulikuwa wakati wao kuonesha Bunge sio dhaifu badala ya kumaliza Muda wote kunukuu Kamusi Za BAKITA kuhusu neno dhaifu

Aibu Sana Wallah daaah
Je Mkuu Pohamba ukifanya rejea ile ya kikao kile cha Bunge na maamuzi yaliyotolewa je
1. Kuna umuhimu wa kuweka kigezo cha elimu katika nafasi ya Ubunge au uongozi wowote?
2. Uzalendo ni nini hasa? Kuweka maslahi ya Taifa mbele au maslahi ya chama mbele kwa vile ndiyo kimeunda serikali?
3. Mkanganyiko huu una athari gani kwetu sisi Watanzania?

Maendeleo hayana chama
 
1) Hakuna Umuhimu wa kuweka Kipaumbele Cha Elimu kwa Kuwa Bunge limeridhia lote sio Wabunge wa la Saba peke Yao, kina Palamagamba, Mwigulu, Ndalichako wote Hawa wameridhia Kama walivyoridhia kina Msukuma Na Lusinde

2) Uzalendo maana yake Ni kupigania maslahi ya Nchi yako kwa gharama yoyote ile
3) Mkanganyiko huu Ni Mtego kwa Mh. Rais Na namuombea kwa Allah ampe Maarifa Na Hekma avuke Salama

Rais analazimika kuchagua Kufanya Kazi Na CAG Au Na Bunge Na ikilazimu CAG atangazwe kajiuzulu Na kuteuliwa Mwingine maana yake Ofisi ya NAO imefanywa Kama Jumuiya Kama ya UWT, UVCCM Au Bavicha Yaan Kuwa Tarumbeta la Wanasiasa kitu ambacho Assad amekataa
 
Nashukuru Mkuu Pohamba kwa majibu yako.

Nina hili fafanua vema ukizingatia nawe ni mmoja wa wanaojya siasa za Tanzania. (interest zetu ktk vyama tuweke pembeni)

1. Ofisi ya CAG kama taasisi inaonyesha na imeonyesha kuwa ni Taasisi Huru inayoweza kusimama na kusimamia utaalam na taaluma halisi ya kinachotakiwa kufanyika kwa mujibu wa katiba. Kweli au si kweli? Kivipi
2. Kuna kuhusishwa kwa Mihimili miwili (Bunge na Mahakama) kumezwa na Mhimili (Serikali) mmoja, je hili kwa maoni yako ni kweli? Kama ni kweli nini madhara ya jambo hili kwa Taifa? Nini kifanyike sasa kuweka uhuru wa kila Mhimili uwe msimamizi wa mwingine?
3. Kuna umuhimu wa kuwa na Taasisi imara au viongozi imara? Kwa waliojaaliwa kuwepo enzi za Baba wa Taifa na Mwinyi, hili waliweza kulisimamisha vipi na sasa linashindikana vipi?
 
Binafsi napata mashaka Sana na hichi kizazi chetu, Bila kupepesa macho wacha na mimi niseme kuwa bunge letu ni kibogoyo, dhaifu, na nyondenyonde! Alichokisema CAG wakati akiulizwa swali BBC alisema ni "UDHAIFU WA BUNGE" na hakusema "BUNGE DHAIFU" kuna tofauti kubwa sana katika hz kauli mbili ila all in all Mzee huyu alikuwa anatafutiwa sababu tu kutokana na misimamo yake, soon ataeuliwa alieandaliwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naionea huruma sana, sana nchi yangu Tanzania nayoipenda. Kama maamuzi yetu kwenye bunge, mahakama na serikali yataendelea kuwa kama yalivyo sasa, baada ya miaka michache tu tutakuwa tumerudi nyuma miaka 20 au zaidi. Tunaona kwenye mahakama: unatolewa uamuzi na mahakama ya chini lakini ikikatwa rufaa mahakama ya juu inasema wazi kwamba maamuzi ya awali yalikuwa sio sahihi kabisa. Kwenye bunge yanatokea kama haya ya sasa hivi. Serikalini tunaona polisi wanabambika watu kesi. Tutafanya nini tutoke hapa tulipo? Ndio maana nasema naionea huruma sana nchi yangu Tanzania nayoipenda.

Tukirudi kwa CAG: kama aliona mapungufu kwenye mambo ambayo bunge lilipaswa kufanya lakini halikufanya (kwa mfano kama halikutendea kazi ripoti zake), akisema kuna mapungufu au udhaifu amekosea nini? Na je, kama bunge halitakti kufanya kazi na yeye, litafanyia kazi majibu yake ya ukaguzi au ukaguzi utaanza upya chini ya mtu ambaye "halidharau bunge"? Mambo haya yanasikitisha sana. Bunge litueleze sisi Watanzania (maana wao ni wawakilishi wetu), udhaifu ambao CAG aliousema ni upi. Kama hakuna udhaifu kweli, kwa hiyo CAG alisema uongo, basi na sisi wananchi tutamkataa kama bunge lilivyomkataa. Lakini kama Bunge lisipoweka wazi "maneno ya uongo" aliyosema CAG kwamba bunge ni dhaifu (kumbe sio kweli), sisi wananchi hatutawaelewa hawa wawakilishi wetu. Kwa hivyo wakikosa kura 2020 wajilaumu wenyewe.
 
Muulizeni Pascal Mayalla kwamba
ukiitwa kule unatakiwa kutoa maelezo na utetezi au maelezo na msimamo wako
KAMA KIONGOZI UNAWAITA VIONGOZI WENZAKO DHAIFU CAG NI TATIZO SANA KIUTENDAJI
ANGESEMA BUNGE HALIWAJIBIKI KIUTENDAJI MAANA YA DHAIFU NI HALI YA KIWANGO CHA CHINI SANA CHA MTU KUTOKUWA MAKINI
 
MakinikiA,wewe nimheshimiwa mbuge wa jimbo gani?nakuchana live mlicho kifanya siyo kizuri,siajabu kwenye kamati nawewe ulikuwemo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu MakinikiA hebu msome huyu jamaa anavyosema CAG kasema hivyo lakini mbona sentensi imegeuzwa? Kwa nini sentensi igeuzwe? Nini hasa lengo hilo kama ni kweli iligeuzwa!
 
Ila kuna mambo mengine ya ajabu sana...

Tunaacha kushughulikia mambo ya maana na yenye tija, tunaangaika na tafsiri za lugha...

Vingapi bunge letu limeshindwa kuvitolea maamuzi zaidi ya kufukuza fukuza na kamata kamata ya wabunge wanaonesha misimamo...

Cc: mahondaw
 
Watanzania kumbukeni zimebakia siku tano rais kuwasilisha ripoti ya CAG bungeni. Watanzania wote waheshimu sheria bila shuruti.
 
Pamoja na hilo lakini nadhani kuna wakati hata watu wa chama tawala wanakerwa na baadhi ya mambo ambayo msingi wake mkuu ni taaluma.
Mfuatlilie utaelewa, huyu atakuwa mkaguzi wa ndani mahali
 
Back
Top Bottom