Suala la CAG: Lugha, Siasa na Taaluma

Suala la CAG: Lugha, Siasa na Taaluma

uzeebusara

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
657
Reaction score
514
Habari wana jukwaa
1. Je adhabu iliyopitishwa ni stahiki?
2. Je kuna athari katika tasnia ya uhasibu?
3. Tunajifunza nin katika sakata hili

Note
Naona kuna shida katika kona za utetezi kuwa finyu sana kwa mshukiwa
Video hii pitia vema then jenga hoja
 
Hapa mkuu hakuna Weledi inaonekana ni kutaka kumshinikiza Seijii ajiuzuru so wanaqnza kumpush ili baadae Jiwe aseme "ajipime"
Then akiondoka ateue wake atakayemshika masikio
Kwa nini Mkuu unaona siasa zaidi imetawala katika suala hili? Kuna suala la kukomoana hapo? Kama yote swa je kwa manufaa ya nani hasaaa? Na kwa nini iwe hv?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa mkuu hakuna Weledi inaonekana ni kutaka kumshinikiza Seijii ajiuzuru so wanaqnza kumpush ili baadae Jiwe aseme "ajipime"
Then akiondoka ateue wake atakayemshika masikio

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna jambo kwa mimi nimelisikia kwa msisitizo wa kati lkn naona lina jambo nyuma yk kama utaipitia vema video ile. Suala la tuhuma ya uvunjifu wa maadili ya umma kwa CAG kutokana na kauli. Je hii hawezi kusukumiziwa kuwa sababu mojawapo ya msingi ya CAG kuondolewa jp mchakato wa kumuondoa ni mrefu lkn zipo njia fupi kama hz za maadili, magonjwa, vifo nk
 
Mkuu kale kavideo fanya kukaconvert hakasomi kwenye simu yangu ya kizamani
Kuna jambo kwa mimi nimelisikia kwa msisitizo wa kati lkn naona lina jambo nyuma yk kama utaipitia vema video ile. Suala la tuhuma ya uvunjifu wa maadili ya umma kwa CAG kutokana na kauli. Je hii hawezi kusukumiziwa kuwa sababu mojawapo ya msingi ya CAG kuondolewa jp mchakato wa kumuondoa ni mrefu lkn zipo njia fupi kama hz za maadili, magonjwa, vifo nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha

Hapo shortcut ni kifo
 
CAG hakusema kwamba bunge ni dhaifu, Bali alisema ni udhaifu wa bunge. Swali la kuuliza ni udhaifu wa bunge kwa muktadha upi! Na huo muktadha ndiyo aliyoukusudia CAG.

Huu ni mtego! Bunge wanajua. Kumbadilishia kibao wanasema amesema bunge ni dhaifu. Bunge limeridhia kutoshirikiana na CAG. Hii ni ajabu! Kwa hili, bunge hapa limeonesha udhaifu.

Halafu ajabu terminology za kitaaluma unazitafsiri kwa kutumia kamusi zilizobeba maana ki-jamii kuelewana kimazungumzo.
 
Ili tujue ukweli CAG apewe basi fursa ya kusema alikuwa anazungumzia udhaifu gani ili sisi Watanzania wote tujue. Bunge lisipofanya hivyo, tutajuaje kama sio kweli kwamba kuna udhaifu na kwamba kusema wanamkataa ni mbinu ya kumzuia asiwaambie Watanzania kuhusu huo udhaifu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani, wala tusitoe/kuvimbisha misuli ya shingo bure, 2020 ipo jirani mno. Tusubiri.

Nakumbuka tuliambiwa. Mh. Zitto alizungumza sana juu mkataba wa Buzwagi, wabunge wa ccm hawakumsikiliza hata chembe na walipopiga kura walishinda kwa uwingi na siyo busara.
Leo hii jambo lile lile limeibuka kama makinikia kila mmoja wao anasifia na kusahau jinsi alivyofifisha filimbi ya awali ya Mh. Zitto.

Nakumbuka tuliambiwa. Mh. Kafulila aliongea sana juu ya fedha za escrow, hadi kuitwa nyani na kutishiwa ngumi na Boxer Mkuu, na hata zamu ya kura ilipotimu, kama kawaida wabunge wa ccm wakakosa kutumia tena busara kuu na kushinda kura kwa uwingi wao mjengoni. Safari hii wakamhusisha na Mkulu wa enzi zile kutetea.
Leo hii tunawaona Habinder Sigh na Rugemalila wanavyopishana Mahakama ya Kisutu wakiandaliwa kupelekwa Ubungo kwa mafisadi.

Kwa mifano hii miwili mtu anaweza kuona tuna Bunge la jinsi gani katika kufanya uamuzi mgumu wa busara kwa manufaa ya Nchi na walipa kodi wake.
Wanayatenda hayo kwa masilahi ya kuilinda ccm (mie ni wanachama) isipokwe madaraka. Nk, nk, nk.
Atamwaga kupitia uwanja upi sasa!? Kwn taarifa tumekuwa tukipata kupitia Bunge! Na Bunge limeweka mpira kwapani na kutoa timu nje!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikiliza Hii Clip ya Taarifa ya Bunge

Kwa ufupi Mwenyekiti wa Kamati hii anapaswa kuliomba radhi Bunge kwa kulidhalilisha Bunge maana Ni aibu Na fedheha kwa Bunge

Mwanzo Mwisho Taarifa inanukuuu Maneno ya Kamusi kufasiri maana ya neno dhaifu badala ya Yeye kuonesha Bunge sio dhaifu

CAG alishawaambia hajutii kusema Bunge dhaifu na akaahidi Kuwa ataendelea kutumia Maneno hayo kwa Kuwa ndio lugha ya kitaaluma sasa ulikuwa wakati wao kuonesha Bunge sio dhaifu badala ya kumaliza Muda wote kunukuu Kamusi Za BAKITA kuhusu neno dhaifu

Aibu Sana Wallah daaah
 
Mkuu ni wewe ama hii ni Id ya taasisi, kuna mwingine kaitumia leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom