Suala la Airtel na TTCL inajulikana tokea 1998, na Serikali iliweka mabilioni na kuua TTCL

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Chanzo cha mpango huo kinatajwa kuwa ni uongozi wa juu wa TTCL uliotaka Serikali kudai haki zake za uwekezaji ndani ya Airtel ambako inaimiliki kwa ubia wa asilimia 40 kwa 60 na mwekezaji.

Dar es Salaam. Kutokana na uwekezaji mkubwa ilioufanya wakati wa uanzishaji wake, Serikali inataka kudai umiliki wa hisa zote za Kampuni ya Airtel Tanzania, imebainika.

Taarifa zilizolifikia Mwananchi zinabainisha kwamba hisa hizo zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kuendesha biashara za kampuni hiyo yenye wateja wengi zaidi nchini ikiwa nyuma ya Vodacom na Tigo.

Chanzo cha mpango huo kinatajwa kuwa ni uongozi wa juu wa TTCL uliotaka Serikali kudai haki zake za uwekezaji ndani ya Airtel ambako inaimiliki kwa ubia wa asilimia 40 kwa 60 na mwekezaji.

“Punde tu TTCL itamiliki hisa zote za Airtel Tanzania Limited. Tayari TTCL imewasilisha hoja ya kutaka kufanya hivyo baada ya kubaini kwamba Serikali ilipunjwa kwenye hesabu za uwekezaji,” kilisema chanzo chetu kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Hoja ya TTCL inaanzia Novemba 3, 1998 ilipoanzisha kampuni tanzu ya Cellnet ambayo ilifanya kazi mpaka Mei 7, 2001 ilipobadilishwa jina na kuitwa Celtel Tanzania huku umiliki wake ukiendelea kuwa chini ya shirika hilo kwa asilimia zote baada ya kuwekeza Dola milioni tano za Marekani (zaidi ya Sh11 bilioni sasa).

Lakini, Januari 31, 2002, Celtel ikiwa chini ya umiliki wa TTCL ilikopa kiasi cha Dola 82 milioni (zaidi ya Sh180.4 bilioni) ili kukuza mtaji wake.

Kwa kipindi hicho, TTCL iliyokuwa na thamani ya Dola 600 milioni (zaidi ya Sh1.32 trilioni) ilikuwa inamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na Kampuni ya Mobile System International (MSI) ya Uholanzi. Serikali ilikuwa inamiliki asilimia 65 ya hisa zote na mbia huyo asilimia 35 zilizosalia.

Agosti 5, 2005, mabadiliko yalifanywa kwenye bodi ya wakurugenzi wa Celtel kwa lengo la kuunda kampuni mbili tofauti; Celtel ikitenganishwa na TTCL. Kutokana na mabadiliko hayo, Celtel iliwekwa chini ya umiliki wa MSI ambayo Septemba 2007 iliuza hisa zake kwa Zain ambayo nayo ilikuja kuziuza kwa Bharti Airtel, Juni 8, 2010.

Imeelezwa kuwa TTCL inadai uwekezaji wake ilioufanya Celtel baadaye Airtel ambayo thamani yake imeongezeka maradufu sasa haulingani na inachokipata hivyo kutaka kusimamia biashara za kampuni hiyo ya mawasiliano. Hoja ya madai hayo ni namna umiliki wa hisa ulivyobadilishwa baada ya Celtel kutenganishwa na TTCL ambayo ilipewa hisa chache tofauti na ilivyostahili.

Hata hivyo, bado haieleweki kama Serikali imeshakamilisha taratibu za kudai umiliki huo kwani si uongozi wa TTCL wala waziri mwenye dhamana aliyepatikana kueleza hatua zilizofikiwa kwenye mchakato huo ambao utaleta mabadiliko kwenye sekta ya mawasiliano nchini.

Kwa sasa, Airtel Tanzania inamilikiwa na Serikali yenye asilimia 40 na Celtel Tanzania BV, kampuni tanzu ya Zain Africa BV ambayo ilinunuliwa na Bharti Airtel International, Novemba, 2010 ikiwa na asilimia 60.

Katika mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni, Serikali iliilipa Bharti Airtel Sh14.7 bilioni hivyo kuchukua asilimia 35 ya hisa ilizokuwa inamiliki na kuifanya imiliki asilimia zote za TTCL.

Sheria mpya iliyopitishwa hivi karibuni na Bunge imeibadili TTCL inayohudumia asilimia 0.82 ya soko kuwa shirika la umma la mawasiliano na kulipa jukumu kubwa katika sekta ya mawasiliano nchini.

Bharti Airtel inatakiwa kuorodhesha asilimia 25 ya hisa zake katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ili kukidhi vigezo vya sheria ya posta na mawasiliano ya mwaka 2010, lakini bado haijafanya hivyo.
 
Mh. Rais wetu JPM.. kashatoa amri kuu, kuwa hadi mwisho wa mwezi huu, kupitia Waziri wa Fedha, hisa zoooooooooooteeee za Airtel zichukuliwe na TTCL...!! Mwisho wa ufisadi Tanzania umefika, so few days naamini TTCL watatangaza rasmi umiliki wa 100% wa Airtel Tz... Na hii ndio sababu kuu wazalendo kama [HASHTAG]#Jay One[/HASHTAG] tunamsapoti kufa na kupona, from bottom of my biggest heart, any time 't' whenever, wherever, whatsoever.. tuko nawe Mh. Rais wetu.. ww ni kiongozi wetu, tuko pamoja nawe and we support you forever..!!

Mungu mbariki sana Rais wetu mpendwa Mh. JPM..!!
 
Mh. Rais wetu JPM.. kashatoa amri kuu, kuwa hadi mwisho wa mwezi huu, kupitia Waziri wa Fedha, hisa zoooooooooooteeee za Airtel zichukuliwe na TTCL...!! Mwisho wa ufisadi Tanzania umefika, so few days naamini TTCL watatangaza rasmi umiliki wa 100% wa Airtel Tz...

Mungu mbariki sana Rais wetu mpendwa Mh. JPM..!!
Ameagiza waziri afanye uchunguzi na sio akachukue hisa.Baada ya uchunguzi ndio itaeleweka,usichukulie kirahisi tu hilo suala.
 
Ikitokea wameichukuwa Gvt wakaweka management ya wazalendo ndio mwisho wa Airtel kama wataiendesha kama wanavyoendesha Ttcl
 
Ameagiza waziri afanye uchunguzi na sio akachukue hisa.Baada ya uchunguzi ndio itaeleweka,usichukulie kirahisi tu hilo suala.


Mh. Rais ana data tayari kasema kuwa Airtel ni mali ya TTCL kwa hisa zote.. So Waziri usifikirie hajui kitu anajua inside-out kuwa Airtel ni 100% mali ya TTCL, sio eti anaanza uchunguzi, ana data ni kuamuru tu when officially kutangaza..!! Usicheze na serikali inajua kila kitu na usione labda serikali ilikaa kimya haikujua kitu, so i hope few days Waziri wa fedha will come up with official announcement..
 
Mh. Rais ana data tayari kasema kuwa Airtel ni mali ya TTCL kwa hisa zote.. So Waziri usifikirie hajui kitu anajua inside-out kuwa Airtel ni 100% mali ya TTCL, sio eti anaanza uchunguzi, ana data ni kuamuru tu when officially kutangaza..!! Usicheze na serikali inajua kila kitu na usione labda serikali ilikaa kimya haikujua kitu, so i hope few days Waziri wa fedha will come up with official announcement..
Hata kwenye Makinikia walijua kila kitu kwamba tunaibiwa lakini kuna mambo ya sheria nk ndio maana mpk leo hayajaisha.
Usifikirie kwamba serikali itaita press conference iseme kuanzia leo Airtel ni yetu,kuna process flani zitapitiwa.Let's wait tusipige ramli
 
Mh. Rais wetu JPM.. kashatoa amri kuu, kuwa hadi mwisho wa mwezi huu, kupitia Waziri wa Fedha, hisa zoooooooooooteeee za Airtel zichukuliwe na TTCL...!! Mwisho wa ufisadi Tanzania umefika, so few days naamini TTCL watatangaza rasmi umiliki wa 100% wa Airtel Tz... Na hii ndio sababu kuu wazalendo kama [HASHTAG]#Jay One[/HASHTAG] tunamsapoti kufa na kupona, any time 't' whenever wherever.. Tuko nae Mh. Rais wetu.. Ww ni kiongozi wetu, tuko pamoja and support you forever..!!

Mungu mbariki sana Rais wetu mpendwa Mh. JPM..!!
Hii imekaa vizuri sana..
 
Mleta mada lengo lake ni JPM asipewe credit kwavile tu ni hoja ya mwaka 98! Tuache uchawi bana JPM kachukua hatua kwa hili tumpongeze! Penye sifa tuwe waungwana ili mkililia mtendewe uungwana muwe na benchmark hiyo ....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom