STUNTER: Breezy Swagger Boy Wa Facebook

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,570
2,000
Nakumbuka kuna kipindi nilikuwaga najiita BREEZY
SWAGER BOY kwenye profile yangu sikuweka picha
zangu niliweka picha za rafiki yangu wa huku
mtaani yeye Handsome ana mvuto ana swaga
balaa nikaona niwe nauza sura na picha zake
Nilikuwa Napenda sana sifa status zangu zote zilikuwa za kujisifia nilikuwa napenda sana kuchat
na Mademu wazuri nilikuwa napost sana kwenye
wall za mademu wazuri yani nilikuwa nna misifa
balaa kila demu mzuri nilikuwa namtongoza kule
facebook
Kuna siku nilimtongoza demu mmoja anaitwa RAHMA nilimdanganya vitu vingi sana hadi
akanikubalia
Aliniuliza naishi wapi nikamuambia naishi MASAKI
wazazi wangu ni wafanya biashara wakubwa
akaniuliza kazi ninayofanya nikamuambia mimi
nasoma chuo yeye akaniambia anaishi Kinondoni anasoma chuo Udsm
Tuliendelea kuchat kila siku na kupeana maneno
matamu tulikuwa tunapigiana sana simu mimi
nikawa namuita mke yeye akawa ananiita mume
Nikawa natupia sana picha zake facebook na
yeye akawa anatupia sana picha zangu bila kujua naweka picha za mtu sio zangu na aliamini mimi
naishi Masaki wakati nilikuwa naishi Manzese
nilimdanganya tu ili ajue mimi kweli wakishua
Tulikaa kama wiki tatu tukawa tunachat tu na
kupeana maneno matamu kwa njia ya simu mimi
nilikuwa nna hamu sana ya kumuona Rahma na yeye alikuwa na hamu sana ya kuniona mume
wake ila nilikuwa naogopa nikionana nae
nitaumbuka sababu ya picha nilizoweka
Kuna siku nikasema liwalo naliwe lazima
nikaonane na Rahma nilichoka kujitesa wakati
mrembo mwenyewe yupo hapa hapa Dar nikaona nimcheki hewani nimuambie tuonane
Nikampigia simu nikamuambia "Rahma mpenzi
naomba leo tuonane bby nna hamu sana ya
kukuona sio kila siku tunachat tu"
Akaniambia "usijali mpenzi wangu mimi mda huu
nipo chuo natoka saa kumi nikitoka nitakustua tuonane hapa Mliman city"
Nikamwambia "sawa mpenzi wangu usisahau
kunistua"
Nilianza kuwaza nikionana na Rahama
nitamuambiaje akiniona niko tofauti na kwenye
picha Alafu siku hyo nilikuwa na Buku mbili tu nikawa
nawaza itakuwaje pale wakati Rahma anajua mimi
mtoto wa kishua kwetu tuna mahela
Nilikaa kwa mawazo sana ile siku saa 9 ilifika
nikaenda kwa msela wangu kuazima nguo japo
nikaonekane niko poa nikakuta msela wangu hayupo
Nilichanganyikiwa sana ile siku nikaamua kuvaa tu
nguo zangu mwenyewe japo zilikuwa zimepauka
raba imechanika nikavaa hivyo hivyo kibishi
nikasema liwalo na liwe lazima nikaonana na
Rahma Rahma alinipigia simu akaniambia yupo Mliman city
na rafiki yake wananisubiri nikamuambia mimi
nipo kwenye Daladala nakuja aliguna akaniuliza
"umepanda daladala mbna uliniambiaga wewe
hupendi daladala kwenu mna magari mengi
unachaguaga utoke na lipi?? Nikamjibu "nakuja bby nitakuambia huko huko
kwann nimepanda daladala"
Akaniambia "basi poa mpenzi ukifika utanistua
nitakuambia tumekaa sehemu gani"
Nilifika Mlimani mwili wangu wote umelowa jasho
daladala niliyokuwa imepanda ilikuwa imejaa sana nilishukuru nilivyofika salama ila mawazo yalikuwa
juu ya Rahma nikawa nawaza nitamuambia nini
sababu kila kitu nilikuwa nimemdanganya
Nilichukua Tecno yangu nikampigia akanielekeza
alivyova na sehemu walipokaa nikaenda hadi pale
nikawakuta wadada wawili warembo balaa wamekaa wanakunywa Juice wa kwanza
kumtambua alikuwa ni Rahma sababu nilikuwa
nna picha zake nyingi sana nikawasalimia na mimi
nikakaa pale pale walibaki wananishangaa sababu
hawakujua mimi ni nani
Inaendelea
 
LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,131

Du iko poua.. shusha madini plz
 
STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,570
2,000
Ukiwa unadanganya, kaa ukijua kuwa unajidanganya mwenyewe. Na siku zote njia ya mwongo ni fupi mno. UWONGO UNAPOTEZA Uhuru wako MWENYEWE
Kuna wakati inafika hauna jinsi inabidi udanganye tu, wanasema ukitaka vya uvunguni usifunue kutanda , so kumpata demu wa kishua inabidi uende nae sawa
 
Infopaedia

JF-Expert Member
Oct 28, 2011
1,071
2,000
Kama nakuona vile mchizi wangu na handkerchief yako ya jeans. Huwa najiuliza.....huwa haiwachubui uso kweli!!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Thread starter Similar threads Forum Replies Date
N Kama vipi tembelea 'swagger' zake Mahusiano, mapenzi, urafiki 7

Similar threads

Top Bottom