Uko sawa. Walimu watakaogoma ni wale wa whatsapp.
Hii itasaidia Sana walimu sasa watakuwa wanatoa adhabu Kwa kuzingatia utu.
Nafikiri tuangalie mitaala ya vyuo hawa walimu wa field walipotoka. Malezi sio kutumia viboko, na adhabu nyingiiiiiii. Malezi sio kutumia nguvu.
Kwa mfano mwanafunzi mtukutu darasani Inawezekana ni kwa sababu hana kazi aliyopewa.
Nafikiri ifuatiliwe pia chuo kilipokea taarifa gani ya walimu hawa wa field.
Maana tukumbuke tunawaita walimu, lakini nao bado ni wanafunzi wa chuo Cha ualimu. Mapendekezo yangu walimu wasihusishwe na hili. Cha muhimu utazamwe utaratibu Mpya wa vyuo vya ualimu, ikiwezekana viwe na shule zake, au wanafunzi wake wanapokuwa field wawe na walimu wao wanawasimamia.
Kama Inawezekana basi wawe chini ya walimu kamili, wasiruhusiwe kumchapa, wala kutoa adhabu yoyote pasipo ruhusa ya mwalimu maalum atakayekabidhiwa kwao shuleni