Student's unlimited freedom

Student's unlimited freedom

Walimu mnazidi kujidhihirisha jinsi gani mlivyo mambumbu hasa walimu wa shule za serikali. Kwanini tukio kama lile haliwezi kutokea kwenye shule binafsi?
Kwanini mambo ya ajabu tu yanatokea kwenye shule za serikali?
Hivi amuwezi kujiuliza ni kwanini yanatokea shule za serikali tu?
Kuna tofauti kubwa sana kati ya shule za binafsi na za serikali, aina ya watoto wanaosoma ktk shule hizo ni tofauti, hata uelewa wa wazazi nao ni tofauti hivyo kwa mwl kuwatreat wanafunzi wa serikali kama wanafunzi wa private itakuwa makosa mno! Amin. Huwezi fananisha malezi ya mtoto wa muuza karanga na na malezi ya mtoto wa mkurugenzi wa CRDB
 
Hata Scorpion pamoja alikamatwa kwa utaratibu na kuhojiwa kabla hajafikishwa mahakamani
 
Walimu mkifanya hivyo mtakwamisha Tanzania ya viwanda serikali ya awamu ya tano inawahitaji walimu sana
Sina hakika kama serikali inaona umuhimu wa mwalimu
 
Huo ushenzi uko wapi?
Ni lini umesikia suala la ajabu ajabu limetokea shule binafsi?
Tatizo lenu walimu wa serikali mnafanya kazi kwa mazoea
Na wewe nilini umefanya research ukagundua hakuna mambo ya ajabu shule za private? Maana usije ukawa unatumia hisia wakati hata shule hujenda.
 
Hiyo nini maana yake? Walimu mmeamua kususa/kununa? Unasema walimu wameamua? Walimu wa wapi hao? Idadi yao?

Ndugu usijaribu kuwakilisha mawazo ya walimu wote nchini utakuwa unajipotosha bure tu. Ngumu jambo hilo kufanikiwa. Mwalimu anayejua nini maana ya wajibu wake kwahakika atatimiza wajibu wake shule iwe sehemu salama kwa mwalimu na mwanafunzi pia. Migogoro itaendelea kuwepo na ufumbuzi utapatikana tu.....ndivyo ilivyo.
Uko sawa. Walimu watakaogoma ni wale wa whatsapp.
Hii itasaidia Sana walimu sasa watakuwa wanatoa adhabu Kwa kuzingatia utu.
Nafikiri tuangalie mitaala ya vyuo hawa walimu wa field walipotoka. Malezi sio kutumia viboko, na adhabu nyingiiiiiii. Malezi sio kutumia nguvu.
Kwa mfano mwanafunzi mtukutu darasani Inawezekana ni kwa sababu hana kazi aliyopewa.
Nafikiri ifuatiliwe pia chuo kilipokea taarifa gani ya walimu hawa wa field.
Maana tukumbuke tunawaita walimu, lakini nao bado ni wanafunzi wa chuo Cha ualimu. Mapendekezo yangu walimu wasihusishwe na hili. Cha muhimu utazamwe utaratibu Mpya wa vyuo vya ualimu, ikiwezekana viwe na shule zake, au wanafunzi wake wanapokuwa field wawe na walimu wao wanawasimamia.
Kama Inawezekana basi wawe chini ya walimu kamili, wasiruhusiwe kumchapa, wala kutoa adhabu yoyote pasipo ruhusa ya mwalimu maalum atakayekabidhiwa kwao shuleni
 
Unadhani mihemuko yako itasaidia? Eti waache kufuatilia wanafunzi wanaokosea? Kwasababu wewe "slimshedy" umezira? Hiyo haiwezekani mwalimu anayefahamu vema kazi yake/mkataba wake wa kazi atatimiza yote tu. Mark my words....siku zitajongea na walimu wataendelea kufanya kazi zao kama kawaida. Madai ya walimu wanataka kupiga kwa kudhalilisha wanafunzi hayana nguvu yatapotea kama moshi unavyopotelea angani.
unaijua sheria ilivyo anayepaswa kumchapa mwanafunzi ni mwalimu mkuu peke yake nasio mwalimu wa kawaida viboko visivyozidi vinne au ulifahamu ilo
 
SUBIRI MATOKEO KUNAWAKATI SEROKALI INASHIKA MPINI NAWALIMU WANASHIKA MAKALI LAKINI KWA HILI WALIMU WATAKUWA WAMESHIKA MPINI NA SERIKALI IMESHIKA MAKALI NASHAURI SERIKALI WAKAE PAMOJA NA WALIMU KULIWEKA SAWA SWALA MALEZI
 
Serikali na jamii mkae mkijua sisi walimu ni wanafiki sana! msifikiri tunavyowachekea ndo tumekubali tuuuu tunafanyaga action ambayo impact yake itaonekana miaka kadhaaa, hebu ona form form four wanamaliza hawajui kusoma wala kuandika ila darasa la saba wana B+, Msicheze na walimu nyie
 
Kama wanajipenda naamini hawatafanya mambo yaliyo nje ya mikataba walioingia na waajili wao. Kama Luna kipengele cha kutoa adhabu katika mikataba yao basi watekeleze tofauti na hapo yatakayowapata yanawastahili
Kwa maana iyo walimu sio walez ni wafanyakaz kama wafanyakaz wengine, ni marufuku kumuita Mwl ni mlez wa mwanao
 
Unadhani mihemuko yako itasaidia? Eti waache kufuatilia wanafunzi wanaokosea? Kwasababu wewe "slimshedy" umezira? Hiyo haiwezekani mwalimu anayefahamu vema kazi yake/mkataba wake wa kazi atatimiza yote tu. Mark my words....siku zitajongea na walimu wataendelea kufanya kazi zao kama kawaida. Madai ya walimu wanataka kupiga kwa kudhalilisha wanafunzi hayana nguvu yatapotea kama moshi unavyopotelea angani.
Kama unataka walimu waendelee kuwafuatilia wanafunzi basi,nashauri waendelee tu kuwatwanga mana hakuna namna sasa na wamechoka!!
 
Swala la kufundisha mwanafunzi aelewe hasielewe hilo lipo tangia zamani na wajue watakukuwa wanajenga mazingira ya kupigwa hadi vibao na wanafunzi wao wanadhani wanakomoa hawajui kuwa w anajikomoa wenyewe
 
Huo ushenzi uko wapi?
Ni lini umesikia suala la ajabu ajabu limetokea shule binafsi?
Tatizo lenu walimu wa serikali mnafanya kazi kwa mazoea
Peleka mtoto private huko watoto wanalelewa kama nyanya maana mwanafunzi ni mteja na elimu ni biashara, yaani wao hata watoto wakilawitiana wanafanya siri hawawachapi wanaogopa kumfukuza mteja, jiulize sasa kitakachokuja kutokea mbelen
 
Walimu mnazidi kujidhihirisha jinsi gani mlivyo mambumbu hasa walimu wa shule za serikali. Kwanini tukio kama lile haliwezi kutokea kwenye shule binafsi?
Kwanini mambo ya ajabu tu yanatokea kwenye shule za serikali?
Hivi amuwezi kujiuliza ni kwanini yanatokea shule za serikali tu?
Sababuni ni ngingi mambo ya ajabu unajifanya huzijui
Private elimu ni biashara
Government elimu ni huduma, jifikirie Mara mbili je neno huduma kwenye serikali linatawaliwa na changamoto zipi?
 
Kwa maana iyo walimu sio walez ni wafanyakaz kama wafanyakaz wengine, ni marufuku kumuita Mwl ni mlez wa mwanao
Kama mwalimu ni mlezi nikwa utashi wake,halipwi ili alee bali aelekeze. Sasa kama wakati anaelekeza kukitokea mambo yanayohitaji kuwa mlezi awe makini isimtokee puani.
 
Back
Top Bottom