Deadbody
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 4,274
- 6,632
WALIMU WETU NA ELIMU KUANZIA OKTOBA 06, 2016
Binafsi sikutaka kabisa kuzungumzia suala la walimu wa mafunzo /Field wakiongozwa na Frank Msigwa kumtesa mwanafunzi Sebastian katika shule ya Sekondari ya kutwa ya Mbeya (Mbeya Day). Watu mbalimbali wakiwepo walimu na marafiki zangu kunitaka kuzungumzia jambo hili.
Lakini pia katika makundi ya whatasaap ya CHADEMA, makundi ya walimu ya whatasaap na hata Facebook nimona mawazo ya watu mbalimbali wengine wakiunga mkono adhabu hiyo na kutetea walimu kwamba ni halali adhabu hiyo kali na walimu wameonewa kufukuzwa vyuo.
Wengine wameonekana kukerwa sana na adhabu hiyo ya kikatili kwa mwanafunzi na wengine wameeleza kwamba kama Sebastian angekua mwana wao wangewamaliza walimu katika kundi hili Walimu wametukanwa kila aina ya tusi ikiwa ni Pamoja na kuitwa "MSHETANI" "HAWAIJUI LEBA / CHUMBA CHA KUJIFUNGULIA", "MAJAMBAZI ", " WAUAJI "," VILAZA WALIOFELI ", na matusi mengine mengi sana ya aibu mengine yakiwa ya nguoni.
Baada ya kujiridhisha maoni ya watu wa pande mbili nimegundua kwamba kwa sasa elimu yetu itaonekana upya na itaanza upya katika suala la uhusiano wa walimu, wanafunzi na wazazi. Walimu wameonesha kueleza kwamba wameonewa Sana kupewa adhabu ya kufutwa vyuo na kufunguliwa mashtaka.
Walimu wanadai, madaktari wamefanya operation na kusahu nyembe katika mwili, wamesahahu sindano au vitu vingine lakini hawajafukuzwa Kazi nk. Wamehoji mateso aliyoyapata mwananchi mmoja huko Mlowo Mbozi kwa udhururaji kwa kipigo cha mbwa mwizi na Polisi na kufariki hali iliyopelekea wananchi kuandamana kukataa kuzika.
Madhaifu ya wazi na sirini yamejitokeza katika taaluma za uhandisi, jeshi la polisi, Udaktari nk. Lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yao. Ghorofa lililoanguka na kuua watanzania Dar Es Salaam mwaka 2012 na 2013 mpaka leo hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahandisi...
Nimeona walimu wameamua kuanzisha uhusiano mpya ili kulinda vibarua vyao. Walimu wanasema kwamba kuanzia sasa kazi ya mwalimu itakua ni kufundisha tu. Walimu wengi wanasema kwamba mwanafunzi aje shule asije hatafuatiliwa. Mwanafunzi avute bangi asivute hakuna wa kujihusisha naye. Mwanafunzi akiwa na uhusiano wa kimapenzi asiwe na uhusiano hakuna kumfuatilia.
Mwalimu akitoa kazi mwanafunzi afanye asifanye hakuna wa kumfuatilia. Mwanafunzi alewe asilewe hakuna wa kumfuatilia. Mwanafunzi achelewe shule, atukane walimu, wanafunzi wagombane, wanafunzi wakifanya chochote wataachwa huru. Mwalimu atafundisha na kuondoka. Hakuna adhabu yoyote kwa mwanafunzi yeyote labda mwanafunzi akipata mimba au kuacha shule mwenyewe lakini walimu watajiondoa kuwa walezi /wazazi wa wanafunzi.
Hii ni kuepusha uhasama wa wanafunzi na wazazi wao dhidi ya walimu. Walimu Kazi wanayosema wamebaki nayo ni kufundisha tu basi. Mengine ni kazi ya mzazi. Uhusiano huu wa wazazi na wanafunzi dhidi ya walimu utawapa uhuru usio na mipaka wanafunzi (Student's unlimited freedom) na matokeo yake yanakuja wazazi, walimu, wanafunzi na serikali tujiandaye kupokea matunda na matokeo ya uhusiano huu mpya wa STUDENT'S UNLIMITED FREEDOM.