Stricktly for ladies....Part I: UREMBO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stricktly for ladies....Part I: UREMBO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Oct 24, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Gents pia mnaruhusiwa kuchungulia...maana na nyie siku hizi hamshikiki kwenye kujiremba lol!

  Nimeshawishika kuandika mada hii na nyingine zitakazofuata kwa kuona jinsi wanawake tunavyodanganywa katika "kununua matumaini".Nimeona wanawake wa kipato kidogo sana wakitumia 90% ya rasilimali fedha walizo nazo katika kununua uzuri au urembo.Wapo akina kaka/baba ambao huchangia pia katika ununuzi wa urembo kwa wake zao na wapenzi wao.

  Nyingi ya vipodozi au urembo huu hasa wa bei poa ni short-lived au huleta madhara kwa mtumiaji au hata uzao wake.Inasikitisha kuona mama mjamzito au anayenyonyesha akijikoroga kwa vipodozi vyenye kemikali hatari kama zebaki n.k au mikorogo inayotengenezwa uchochoroni na wafanya biashara wasio na ethics ( biashara ni ushindani na mara nyingi ushindani hauna adabu!).

  Kwa sasa hivi, soko la vipodozi na urembo limevamiwa na wakongo na wanaijeria ambao huchanganya madawa makali na kuyafungasha katika vifungashio vya kuvutia na kuvipa majina ya kuvutia - extra light, super white etc.Wachina nao wameshanusa na kujua mwafrika anataka nini na hivyo kujibu kiu ya soko kwa bidhaa kadha wa kadha.

  Biashara yoyote yenye kulenga urembo wa mwanamke huuza.Kwanini? kwasababu kila mwanamke anapenda kujali muonekano wake.Amelelewa ( socialized) kutaka kuwa na ngozi nyororo isiyokuwa na mawaa, awe na nywele nzuri - ndefu, zenye kung'ara, awe na kucha zilizonakshiwa zikavutia, awe na umbo lililokaa vema - kutegemeana na mhusika anayotaka.Kuna wenye kupenda unene, wembamba nakadhalika.Wapo wenye kupenda kuonekana warefu zaidi, japo sijui kama wapo wenye kupenda ufupi n.k.Kuna wenye kupenda waonekane wamejaaliwa vifuani, kwenye makalio,hips na kadhalika.

  Tukitizama vigezo vyote hivi tutaona kuwa kuna biashara lukuki zenye kulenga maeneo hayo yote niliyoyaainisha.
  1. Nywele - dawa na mafuta ya kulainisha, kuviringisha, kubadili rangi, kuna kusuka, kukuza nywele, kujaza nywele n.k.
  2.Ngozi -dawa na mafuta ya kulainisha, kung;arisha, kufanya iwe na rangi ya kung'aa, kuifanye iwe nyeupe na kwa vile naangalia zaidi urembo wa kiafrika sijui kama kuna virembesho vya kuifanya iwe nyeusi! wazungu wanazo tans etc.Kuna mikorogo ya kienyeji n.k.
  3. Kucha - dawa za kurefusha, kubandika ziwe ndefu, kusafisha,kuna rangi n.k
  4.Maumbile - kuna mazoezi kupunguza au kujenga sehemu husika, kuna dawa siku hizi za kupaka na kumeza kuongeza au kupunguza, kuna upasuajia nk.Kuna nguo za kubana matumbo, makalio, kuna viatu kuongeza urefu
  5. Mvuto - kuna manukato, dawa za usafi zenye kulenga maeneo mbalimbali ya mwili wa mwanamke...

  Kwa kifupi UREMBO WA MWANAMKE NI BIASHARA KUBWA.kwavile inahusu kuuza na kununua matumaini...siku zote wenye kuifanya wana uhakika wa kutajirika.....There is always hope
  Je ladies..are you aware of how much u r contributing to enriching unscrupulous business men and women ?

  Kama mlengwa wa hizi biashara, unachukua hatua gani kuhakikisha hauingii kwenye mitego ya kukufukarisha badala ya kukupa tumaini unalolitazamia.?

  Are you aware kwamfano kuna njia nyingi salama na za bei nafuu za kukupa urembo wa ngozi yako na nywele?..Urembo wa ngozi na nywele zako unaweza kupatikana kwa kula chakula bora ,kunywa maji ya kutosha - mwili wa binadamu asilimia zaidi ya 70 ni maji! Huhitaji kutumia kemikali kusafisha ngozi yako auaweza kutumia matunda na mboga kusafisha ngozi yako kwa mfano ndimu au limao, huhitaji mikorogo bali waweza kujipaka mafuta unayoweza kutengeneza mwenye ( mwenye kutaka ani PMnimjuze)..Unweza kudumisha urembo wako kwa kujipa mawazo safi akilini mwako, kupumzisha akili na mwili wako, kufanya kila kitu kwa kiasi - kula, kunywa, na vingine ambavyo siyo vizuri kuvisema hapa.
  itaendelea......

   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mhhh.sorry kwa kuchungulia huku..

  Vera we anzisha idea ya kampuni ya vipodozi.....
  Halafu wanawake wenzio waje wanunue hisa...mjikomboe...
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Boss usione soo kuchungulia unaruhusiwa kabisa maana na wewe ni mdau - kama hautumii basi unatoa sponsorship kuvinunua.
  Kuhusu kuanzisha kampuni..... ni wazo zuri..let me sleep over it.....
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Whatever you do, do it in your privacy.Hamna kitu kinacho bore kama kumuona demu anajipodoa kwenye public transportation.Ni kama anaonyesha kuwa what you see is not the real me, it is just cosmetics.Halafu ina project kukosa confidence fulani, kama vile you have to constantly reapply make up just to reassure yourself that you are beautiful.

  That and taking every opportunity to look at any mirror-like object.The vanity!
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Lol! Nimecheka sana...
  Niliwahi kuona mwanamke akijipaka wanja huku anaendesha gari kwenye traffic jam...unachozungumzia ni etiquette ya kujipodoa...
  Kuna taratibu kabisa za wapi, vipi na lini kujipodoa
  1. Jipodoe kwenye faragha - chumbani kwako, washroom,.Kamwe usijipodoe mbele za watu kama kwenye mikutano, restaurant,kwenye gari inayoenda,ofisini etc
  2. Perfume - paka kabla hujatoka kwako..usiibebe mfukoni au kwenye kibeti chako.
  3.Mwanamke hapaswi kuanza kujipodoa mbele za wanawake wenzake labda kama anataka wamsaidie kuboresha au kumpa feed back.
  4.Kamwe usijipodoe mbele ya mume/mpenzi wako labda kama mko wote chumbani na unafanay hivyo kama utaratibu kabla hujatoka.
   
 6. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ........Da WoS kuna sehemu hapo umesema kuna mafuta unaweza kujitengenezea mwenyewe nyumbani, nina hamu ya kujua jinsi ya kutengeneza hayo mafuta.
  Kuhusu ndimu na limao mie mwenyewe nimehakikisha ni nzuri kwa kusafisha ngozi, na kuondoa spots.
  Hebu leteni mambo wanawake ili tuweze kujipodoa kwa kutumia vitu natural,itakuwa bora iwapo utaongelea kitu ambacho kweli umetumia na kimefanya matokeo mazuri.
   
 7. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2010
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,973
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  WoS, wewe si unataka kutupeperushia ndege wetu? Mikorogo yetu nani atanunua sasa?
  Ladies, mi nawatania tu kwa hilo. Mi mwenyewe mpenda natural.
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwakweli wazo zuri kama wadada wakiaamka na kuzingatia ushauri wako juu wa wanaigeri ninahakika nao sana kwani nimedili nao nimeona wanayofanya ni aibu yani nilisema kama pesa ndo hivi basi. jibu nilopewa nikwamba uoga wako ndo umasikini wako
   
 9. K

  Kekuye Senior Member

  #9
  Jan 21, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WoS umefanya jambo bora sana kuwakumbusha wanawake kuhusu urembo na vipodozi. Ila kiukweli mada hii inawahusu wanawake na wanaume kwa sababu mara nyingi wanawake hujiremba kulingana na jinsi wanavyosifiwa.
  Ningeomba pia kama utaweza uweke pia mada ya mavazi kwa sababu nayo ni sehemu ya urembo. Na kwa kiasi fulani wapo wanawake ambao hawafahamu kuhusu mavazi na mazingira ya kuyavaa.
   
 10. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani kama ulivyosema si vibaya kujipodoa/kujiremba kama unatumia vipodozi ambavyo haviumizi afya yako. It gives a good feeling to look beautiful and to know other people have noticed too lakini hawa wenzetu wanaofikia kabisa kujichubua ngozi zao na kujiangalia kwenye kila kioo wanachokutana nacho mpaka kwenye public transport may be its because they feel a little inferior and may be they think they dont have anything else to offer except beauty and thats really sad, because if you have reached a point where your "look" is the only thing you can give/show, then you are not living.
   
Loading...