STRESS FREE: Vichekesho on fleak! Weka na cha kwako hapa tufurahi

Arabian queen

JF-Expert Member
Nov 23, 2016
2,591
2,000
MAPENZI NI MATAMU ILA ACHA KIHEREHERE..

Ama hakika mapenzi ni matamu sana ukimpata akupendaye mkashibana. Kumjali mpenzi wako ni jambo la msingi sana lakini ni vizuri kuepuka kuwa na kiherehe sana. Jamaa mmoja alijikuta taabani mara baada ya kumkurupukia mpenzi wake.

Jamaa mmoja alikuwa na demu wake ambaye alikuwa anamjali sana kwa kila kitu. Yule demu alikuwa kila anachotaka jamaa anatoa. Kwa ufupi jmaa alikuwa anamjali sana demu wake.

Siku moja kama kawaida jamaa aliamka asubuhi na kuchukua simu yake kisha akampigia mpenzi wake wa moyo.

Jamaa: Mambo baby umeamkaje?
Demu: Siko poa sana…
Jamaa: Nini mbaya mpenzi?
Demu: Nina mimba halafu sikupanga iwe sasa!
Jamaa: Khaaa! Mbona tulikuwa tunatumia kinga umepataje?
Demu: Kani nani kasema ya kwako?

Hivi navyooongea jamaa kakimbizwa Muhimbili kazimia kwa mshtuko! Kweli mapenzi ni matamu! Ungekuwa wewe ungefanyaje aisee?
 

Arabian queen

JF-Expert Member
Nov 23, 2016
2,591
2,000
 

Attachments

  • _20170412_121026.JPG
    File size
    103.8 KB
    Views
    430

Arabian queen

JF-Expert Member
Nov 23, 2016
2,591
2,000
Jamaa mmoja akiwa na mtutu wa kivita maarufu kama AK47 alivamia kanisa moja la kiroho na kukuta watu wanafanya ibada. Akiwa ameuelekeza mtutu wake juu jamaa alianza kupaza sauti huku akielekea madhabahuni.

“Nani ni mtoto wa mungu hapa?” Jamaa alihoji kwa ubabe. “Nauliza hivi, nani ni mtoto wa mungu hapa ili nimpeleke sasa hivi kwa baba yake mbinguni!”

Waumini wote walikaa kimya na jamaa akaongeza mkwara kwa kufyatua risasi tatu kwenye paa la kanisa. Waumini wote wakapaza sauti, “ni mchungaji. Kila siku huwa anasema yeye ni mtoto wa mungu.”

Kwa upole na unyenyekevu mwingi mchungaji akajibu, “mbona mnanisaliti wapendwa? Nyote nyie mnajua kwamba mimi ni mtoto wa Githinji. Sasa ninahusianaje na huyo mungu!”

Chezea safari ya mbinguni wewe!!!
 

Arabian queen

JF-Expert Member
Nov 23, 2016
2,591
2,000
ACHA MASWALI YASIYO YA MSINGI

Jamaa mmoja kwa kupenda vya kunyonga siku moja aliingia choo cha stendi bila kupenda. Tabia yake ya kuuliza maswali yasiyo na msingi ilimtokea puani na kumwacha mdogo kama kanyeshewa mvua ya mawe.

John: Cuzo, nasikia siku hizi unafanya kazi bakery.

Cuzo: Ndiyo, nafanya job kwa bakery bana.

John: Mbona hujawahi niletea mkate hata mmoja bana?

Cuzo: Dada yako yule anafanya kazi airport amewahi kuja na ndege kwa nyumba? Ehee! Wewe mwenyewe wafanya kazi mortuary, ushawahi kuja na maiti? Tafadhari usinikasirishe, sijalipwa mshahara mwezi wa tatu huu!
 

Arabian queen

JF-Expert Member
Nov 23, 2016
2,591
2,000
MSIKIE UYU MTOTO ANASEMA NINI

Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa.
Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto
wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika
akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na
manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi
kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa
manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo
wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao
 

Humble African

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
4,776
2,000
Jamaa kaingia Bar;

Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom