Huyo aliyeandika haya maoni amekulia wapi? Alizawa na kukulia huko huko USA? Kama alizaliwa na kukuli huko nitamsamahe kwa haya aliyoandika. Lakini kama alikulia Tanzania nitashangaa kwani historia ya Tanzania ni somo tunalolisoma tangu shule za msingi na kuendelea. Mimi nikiwa primary school nakumbuka mambo kama vita vya majimaji, kuzaliwa kwa TAA na baadae TANU, harakati za uhuru na mambo mengi tulikuwa tunafundishwa.