Lady of Destiny1
JF-Expert Member
- Feb 4, 2019
- 588
- 869
Naomba ushauri wako, mimi nina miaka 37, naweza kusema kuwa sijaoa, lakini nilikua naishi na mwanamke ambaye ni kama mke wangu kwa miaka 10, hatukuwahi kufunga ndoa na nilikua sijawahi kukanyaga kwao. Kila wakati nilikua nasema kuwa nitaenda nitaenda lakini mambo yanabana. Mwaka jana tuligombana sana, alikua ananitishia kuwa kama mimi simuoi basi ananiacha, kwakua nilijua kuwa hawezi kuniacha nilichukua vitu vyangu nikaondoka, nilikua naishi kwake kwani yeye ana nyumba kubwa tu na ana kazi nzuri, ni mfanyakazi wa serikali ana cheo kikubwa tu.
Niliondoka na kwenda kuishi kwa rafiki yangu kwa muda, kweli baada ya kuona niko siriasi basi alinitafuta na kuniomba msamaha. Nilimsamehe na kurudiana naye, lakini niliona kama ni mtu kabadilika, pesa ya matumizi hatoi kama zamani, anakua ni mtu wa hasira tu na wakati mwingine hata kupiga watoto. Nilimuambia kama ataendelea na tabia hiyo basi mimi nitamuacha, alijiahidi kubadilika lakini ni ile unaona kabisa kuwa mtu analazimishia. Mwaka huu alipata uhamisho, alihamishiwa Doddoma, ilikua ni mwaka huu mwanzoni, kwakua watoto wanasoma basi tuliamua mimi nibaki huku kwanza kuangalia watoto kisha tukishapata uhamisho basi tuhamie kule.
Hiyo ilikua ni mwezi wa pili, lakini kila siku nikimuambia mwenzangu kuhusu uhamisho alikua ananipiga chenga, huwezi amini kuanzia mwezi wa pili mpaka sasa hivi hajaenda hata shule kufuatilia. Kibaya zaidi hataki niende kujua alipohamia, kila nikimuambia mara yuko bize, mara hiki mara kile, amebadilika sana. Baada ya kuona kabadilika nikahisi kuna kitu, nikaamua kwenda mpaka kazini kwao, kufika nikamuulizia na kutaja kuwa mimi ni mume wake, kila mtu alishangaa kwani kumbe alikua na mwanaume mwingine. Niliambiwa kasafiri na mume wake kwenda honeymoon.
Nilishangaa lakini nilipomtafuta na kumuambia nipo Dodoma akaniambia kuwa ameolewa na mwanaume mwingine tena ndoa ya kanisani. Yaani hapa nimechanganyikiwa, amefunga ndoa kimya kimya kashirikisha ndugu zake tu, mimi hata sijui chochote. Hata watoto wake hakuwaalika, nashindwa kujua nifanye nini, kuna mali ambazo tulichuma pamoja, zina majina yake sasa nawaza kisheria nikoje maana ana mume wa ndoa, na watoto hata hazungumziia maana simu zangu hapokei tena, naomba ushauri nijue wapi pakuanzia.
Sent using Jamii Forums mobile app