Story yenye funzo: Tayari ameolewa

Carnivora

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
3,651
5,980
Habari za Jumapili wakuu.

Niende kwenye mada. Kama kichwa cha thread kinavyosema, ni kweli yule bint ameolewa. Let me take you to the story behind. Ni kisa kinachonihusu mimi mwenyewe. Mimi ni mwanaume, mwezi ujao wa May nitatimiza miaka 30.

Ilikua ni Jumamosi, 22 October, 2016; nilipomwona kwa mara ya kwanza huyu bint. Nilisafiri Ijumaa tarehe 21 lakini nilifika jioni sana jijini Tanga kumfuata huyu bint nikitokea Dar es Salaam. Mwenyeji wangu, rafiki wa kiume, classmate wangu wa chuo akanipokea na kunipeleka mahali ambapo nitalala. Sikuweza kulala kwake sababu ya uhaba wa mahali anapoishi. Akanipeleka lodge nikalipia hapo. Lengo la safari yangu lilikua kukutana na bint ambaye nilitambulishwa kwake na rafiki yangu mwingine kuwa anafaa kuwa mke. Tukiwasiliana kwa siku kadhaa kama marafiki wa kawaida tu. Makazi yangu yalikua jijini Mwanza ila nilikuja Dar likizo basi nikatumia muda huo kwenda Tanga kumuona mhusika ili tuweze kuongea japo mawili matatu tukiwa ana kwa ana nami ikiwa kama utalii kufika Tanga kwa mara ya kwanza.

Jumamosi ya tarehe 22 tukaonana na bint, mwenyeji wangu pamoja na yule bint wakashauri twende Raskazone. Tukaenda beach kule. Jamaa akatuacha kidogo tukizungumza mawili matatu. Alionekana mwoga na mwenye aibu sana yule bint. Naomba nimuite jina la Maryam ingawa si jina lake halisi. Mariam alikuwa anaongea na mimi huku amegeukia upande wa pili. Ilinichukua sekunde chache kugundua kuwa ni msichana asiye na mambo mengi na anaonekana ni mgeni wa vitu vingi sana. Nilishangaa kwa umri wake wa miaka 21 wakati huo na amesoma hadi chuo (certificate) na mji aliopo wa Pwani, ni kitu cha nadra sana. Nilihisi ana act. Nilifanya juhudi ya fasta fasta anizoee ili mambo yaende. She was very anxious. Tukatambulishana vizuri na kuelezana historia za maisha yetu kwa undani. Mwisho nikamuuliza, unataka kuolewa, ukiwa kama mke matarajio yako kwa mume au kwenye ndoa ni nini? Hakujibu hili swali. Baadaye tukarudi mjini, nikachukua bus nikarudi Dar na kesho yake nikapaa na Precision back to Mwanza nilikokuwa natakiwa kureport kazini Jumatatu ya tarehe 24.

Mawasiliano yaliendelea na Maryam alionekana kakolea kweli kweli. Kila mara alisisitiza nimuoe. Hii nioe ilizidi mno mpaka nikawa napata wasi wasi huyu anataka ndoa kweli au kuna kitu anatafuta. Mwaka 2016 ukaisha na 2017 ikaanza yeye ajenda yake ikiwa ni hiyo hiyo. Nilimueleza mpango wangu wote. Kwamba mwaka huo wa 2017 ninataka kuacha kazi nijiajiri. Nikishajiajiri I'll need atleast six months nikae sawa. Then naweza kuoa. Alikubaliana nami. Mwezi June 2017 niliacha kazi, nikarudi Dar, nikaanza michakato yangu. Dar ndipo nlipokulia na familia yangu yote ipo hapa. Nilikomaa mpaka mwaka ukaisha 2017. Hali yangu haikuwa nzuri sana. Alitoka Tanga akaja Dar na akawa anaishi hapa. Nilimtimizia mahitaji yake kwa kadri alivyotaka. Nilimpa muda wangu mwingi, mara nyingi mimi ndio nilikua nataka tuonane maana yeye mpaka ajipange kutunga safari na halijui jiji vizuri. Kwa hiyo tulikua tunaonana mara kwa mara. Sikuwahi kumgusa hata mara 1, nilifanya hivyo makusudi ili ajiongeze. Ikiwa kweli mi namtaka kwa ajili ya ndoa basi ataona matendo yangu.

Mwaka 2018 ukaanza bado hali haijabalance vizuri. Kwa sababu mwezangu alikua anapush mno nimuoe. Nikasema ikifika March mwishoni ntaanza mchakato afe kipa, afe beki.

Mungu si Athumani wala sio John. Mwisho wa March kama nilivyopanga mambo yakawa yanaenda vizuri. Lakini nilianza kuona mabadiliko ya mwendendo wake. Kuna siku akaja home kwangu, tukiwa tunaongea nikambana sana akafunguka huku analia. Nilimwambia nataka kupeleka kwao posa, akashtuka na kuniuliza nikipeleka posa ntakaa muda gani ndipo nioe.? Nikamwambia sitakawia. Machozi yanamtoka. Eti nimsamehe, amefanya uamuzi wa kijinga. Na anajutia.

Ndipo nikataka kujua undani wa kilio chake. Akafunguka kuwa, baada ya kuona mimi nakawia kumuoa alishauriwa na rafiki zake anipige chini atafute mtu amuoe. Na pressure ya mama zake (familia) nao huko kijijini kuwa yuko mjini huku muda mrefu kwa nini haolewi (maana tangu amemaliza chuo mwaka 2015 yuko tu home Tanga na hapa Dar kwa ndugu). Rafiki zake walimshauri kuna ustaadhi anafanya kuunganisha watu walio single waowane kupitia group ya whatsapp. Naye akajiunga huko. Ustaadhi alipomuona akata kumuoa mke wa pili (mathna) akakataa. Ndipo akapatiwa jamaa mwingine mwalimu wa sekondari. Wakakutanishwa....jamaa akamind mzigo. Ustaadhi akapeleka posa mwenyewe. Mahari ikalipwa. Na mpaka siku tunaongea nami harusi ilishapangwa tarehe 22 mwezi April. Haya yote yamefanyika ndani ya mwezi 1.

Nilisikitika. Nikanywa maji ya baridi kwanza. Nikamuangalia akijiliza. Nikamhoji mambo mawili matatu nikamwacha akaenda. Ila nikamwambia ntafanya kitu hiyo ndoa haitafungwa. Kesho yake hakupokea simu yangu akidai anaogopa nitambwatukia. Hivyo anataka tuchat tu.

Kesho yake hiyo akaniambia Meraki mahari imeanza kugawanywa hadi kijijini imetumwa. Na mama yake anakuja Dar tarh 15 mwezi April. Hajui afanye nini. Aanaogopa mi nikilianzisha atatia aibu kwa familia na ukoo wao sababu wale watu, ustaadh na muowaji aliwaambia mwenyewe wapeleke posa. Na siku hiyo ndo ustaadhi aliwaruhusu waanze kuwasiliana kwa simu. All the way long hawakuwahi kuwasiliana. I was in a shock. Nikakumbuka wimbo wa Kassim Mganga, harusi. Usijeitaka harusi kwa pupa. Yaani inaonekana alitaka tu kuolewa. Nikajiwazia, bint wa miaka 22 anaona anachelewa? Ila poa ndio maisha na kila mtu anayadefine atakavyo.

Niseme tu mimi ni sikuwahi kufahamika kwa nduguze hapa Dar japo yeye nilimtambulisha kwa baadhi ya watu wangu. Kiufupi sikufahamika kwao lakini dadake alikua anajua kuwa huwa anakuja kwangu.
Na pia mimi ni mtu wa imani kidogo. So nikamwamchia Mungu na kushukuru. Nikaswali rakaa 2 sunnati shukr kumshukuru Mungu kwa yote kisha nikafunga kitabu chake moyoni mwangu. Niseme ukweli hili suala halijaniumiza sana ila limeniongezea funzo kuwa usiwaamini sana wanawake hata yule usiyemdhania. Niliwahi kuumizwa na mapenzi huko nyuma nikaapa sitaki tena mapenzi yanitese namna ile. Nadhani hili limenisaidia kuvuka hiki kiunzi.

Nikashukuru Mungu nikasema Mungu amenipa muda wa kufocus na biashara zangu. Na mwezi wote huu wa April umekuwa busy mno na kama vile imekuwa take off yangu maana deal zimekuwa poa sana mpaka nakosa muda wa kufanya mambo mengine. I just move on. Ndio kwanza nina miaka 30 next month. Now I will marry when I want.

Story ni kama funzo kwa wengine. Sorry kwa uzi mrefu.

Jumapili njema.
 
hapo nilipoona Tanga tuu..nkajua yale yale, yakhee kule wote wameolewa mkuu
 
Kosa kubwa zaidi ulilofanya ni kutomtafuna.

Binti hana kosa, kosa liko kwako, huwezi kua na mwanamke kwenye mahusiano miaka 2 hujamtafuna, huo ni uzwazwa.

Kama mwenyekiti wa chama cha wanaume nakuwekea red color, naangalia mwenendo wako, hali hii ikiendelea unahamishiwa upande mwingine.
 
Nimekimbuka kale kawimbo ka dreams kanaimba hivi
Kamwambie mbona amechelewa, amechelwaa
Kidonda cha mapenzi alichonipa nimeshaponaa
Kamwambie mbona ye aliolewa, aliolewaaa
Na kidonda cha mapenzi alichonipa nimeshapona
 
Ndo ujue kwamba Bongo kwetu Wanawake huwa hawa fall in love na Wanaume bali huwa na maslahi tu, kwa akifupi hakukupenda, chukua kama fundisho na ukumbuke hilo maisha yako yote jamii yetu hatulelewi na kufundishwa maana ya ku.fall in love hayo ni mambo ya kigeni tuliletewa tu,

Mwanamke ni swala la muda ukifika na Mwanaume gani yupo tayari kwa wakati huo na huyo ndiyo atakayeolewa naye, jifunze, hapo Mwanamke wa Kibongo ha fall in love hata siku moja bali ana maslahi tu!
 
Kosa kubwa zaidi ulilofanya ni kutomtafuna.

Binti hana kosa, kosa liko kwako, huwezi kua na mwanamke kwenye mahusiano miaka 2 hujamtafuna, huo ni uzwazwa.

Kama mwenyekiti wa chama cha wanaume nakuwekea red color, naangalia mwenendo wako, hali hii ikiendelea unahamishiwa upande mwingine.
Wala sijutii uamuzi wangu. Nishafanya sana mapenzi na wanawake wengi hivyo sikuona sababu ya wala jipya ntakalopata kwake.
 
Kifupi huyu binti atajutia. Ramli yangu Zogwale ni kwamba binti ameingia chaka na haitapita muda mrefu atakukumbuka na atalia machozi ya damu. Nayaona mateso na vilio kwenye ndoa ya muda mfupi kiasi hicho. Mungu akutie nguvu mkuu usonge mbele na mke mwema utampata.
 
Pole ustadh,jua mlango wako haujafunguliwa,au umefungua mlango usio sahihi. Subiri mtu sahihi utampa na utaoa kwa amani zote.
Lakini next time ujifunze Ku authorities mahusiano kwa ndugu wa pande zote mbili hasa kama una nia ya kweli ya kuoa.
 
Similar Discussions

22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom