STORY:KINDERE
EPISODE 02
*******
Siku hii ya Jumatano nilibakiwa na siku moja tu-Alhamisi, kbla ya siku ya kafara yangu ambyo ilikuwa Ijumaa saa 6 mchana. Pamoja na urembo aliokuwa nao Maanu, alikuwa anatokea kwenye familia ya maisha ya kawaida sana. Hivyo hata kama nitatumia KINDERE changu kumuomba pesa ya kununulia mbuzi wawili ambayo ilikuwa ni zaidi ya laki mbili, asingeweza kunipa.
Hapa ndipo nilipomfikiria Nei, demu niliyektana nae siku tan0 zilizopita. Licha ya kuwa alikuja hadi kwangu na kufanikiwa kumega tunda lake, alikataa kulala geto kwangu. Kilichofanya nimkumbuke ni kwa sabbu alitokea familia ya maisha bora. Laki mbili au tatu kwake halikuwa jambo kubwa sana. Niliamini tatizo langu limepata ufumbuzi. Kazi moja ndogo tu niliyokuwa nayo ni kutafuta namna ya kumuondoa Maanu hapa geto ambaye alishaahidi atakuwepo hadi Jumapili, ili kesho aje Nei nipate muda mzuri wa kumshawishi anipe pesa.
Kama maelezo ya mganga Chozzi yalivyosema kuwa muda sahihi wa kuomba kitu kwa mwanamke kupitia KINDERE ni pale ambapo nitakuwa 'nimeingiza kisu changu kwenye ala'. Hapo asingekuwa na namna yoyote ya kunikatalia. Hivyo, ilikuwa ni lazima Maanu aondoke ili Nei aje niweze kufanikisha zoezi langu ili niendelee kutumia KINDERE kwa muda mrefu. Niliamua kuchukua simu yangu na kumpigia Nei kutaka kujua kama naweza kukutana nae. Lakini kbla sijapiga simu, niliondoka pale kitandani na kwenda moja kwa moja hadi katika hifadhi yangu ya KINDERE na kukitoa. Ilikuwa ni hirizi ndogo tu na nyepesi ambyo usingeweza kudhania kama ina kazi kubwa kiasi hicho. Nikaelekea jikoni kwenda kukisemea vile ninavyohtaji. Baada ya hapo ndipo nikapiga simu.
"Haloo Nei, nimekumis dia wangu"
"Nimekumis pia Piza, natamani nikuone leo"
"Na mimi pia nilitamani hvyo mpenzi, tena nataka uje ulale kabisa leo" Nili0ngea na Nei kwa kujiamini kwani KINDERE hakijawahi kuniangusha. Na kwa jinsi nilivyokinuilia hapo jikoni, nilikuwa na uhakika juu ya Nei.
"Daaah sijui itawezekanaje Piza, ndo najiandaa hapa kuelekea Arusha, tumepata msiba na tutazika Ijumaa jioni, kwahyo hapa kurudi labda Jumapili" Nei alinijibu na kunipa kigugumizi, tumaini langu pekee lilikuwa ni yeye na nilibaki na siku moja tu. Mawazo juu ya hatma ya KINDERE changu baada ya Ijumaa kama sitofanya kafara yakawa makubwa. Niliduwaa kwa zaidi ya dakika tano hku Nei akiendlea kuniita bila mafanikio yoyote hadi alipoamua kukata simu. Utamu wa KINDERE ulishakolea. Lakini nilibaki na siku moja tu ya kesho Alhamisi kuweza kupata mbuzi wawili kwa ajili ya kafara ya KINDERE. Nilihisi kupagawa.
Itaendelea...
0718274130