Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Yaani una miaka 22 unasimulia story ya maisha yako uko seriously kweli?

Duuh kweli mmegundua wanna jf wana hali ngumu Koo wanapenda story za kuwafariji na nyie mnawaletea story kila uchao

Sema me mtu anaekaa kwao hawezi akanipa story ya maisha yake
Asante kwa mchango wako nimeupokea
 
Inaendelea......

Hata baada ya kupata huo msala tabia yetu haikubadilikia bado tulikua tunaibaiba vitu vya watu.Ilifikia hatua tukawa tunaitwa chokoraa kwa sababu tulikua tunatembea mitaani kutafuta vyuma chakavu kisha tunaeenda kuviuza.Sehemu tuliyokua tunaviuzia ni pale karibu ofisi za mabasi ya kimotco

Katika uokotaji wetu machuma kunakipindi tulikua tunatoka kapa yaani hatupati kitu kwa sababu tulikua wengi waokotoji so ikawa ni mawaiano.Tulikua mtu tatu kwenye kundi langu mimi,huyo rafiki angu na jamaa mwingine tulikua tuko nae mtaa mmoja ila sio majirani.

Kuna siku nilipata kisanga kimoja tulipokua tunatafuta vyuma cku hyo tulienda mtaa wa Amri Abedi sasa huko tulikutana watoto wa nyasho nao walikua ni waokotoji vyuma.kulitokea kutokuelewana sisi pamoja na hao watoto alafu walikua wengi sisi tuko watatu,ugomvi ukaanza katika hizo harakati za ugomvi kuna dogo mmoja alinipiga Jiwe kwenye paji la uso walivyona damu zinanitiririka Waka run.....ok tuachane na hayo maana nilipata msaada kuna mbaba hivi alinipeleka despensary kuoshwa kidonda.

Baada ya vyuma kuwa adimu mtaani kuna cku niliwapa wazo wenzangu kuwa wanaonaje tukianza kuiba ile mifuniko ya masink ya choo ( chambers ) walikubali tukapanga tuwe tunaiiba usiku watu wakiwa wamelala

Na kweli ilipokuwa ikifika usiku midaa ya saa 8 au saa 9 tulikua tunafanya doria yetu kwenye masink ya watu.jamaa yetu yeye tulikua tunampitia kwao yeye ndo alikua anabeba ile mifuko ya kubebea hizo bidhaa ( gunia) tuliiba iba sana hyo mifuniko ya chamber ila kuna siku moja duh....hii cku ctaisahau cjui tungekamatwa ingekuaje.

Sikumbuki ilkua ni jumangp ila mwaka ni 2006 mwanzoni nikiwa darasa la nne tu.Siku hyo kama kawaida jamaa angu aliniamsha ilkua kwenye saa saba usiku twende kwenye mishe zetu.Tuli plan kwenda mitaa ya Kennedy lakin ilibidi tuanze kwanza kwenye mji mmoja hivi ni jirani na mtaa wetu.Tulifikapo fresh tu kuchora ramani tukaona kuko vzr tu wasiwasi hakua mkubwa sana

Nilichukua mfuniko wa Kwanza nikaweka kwenye mfuko sasa yule jamaa etu mwingne alipokua unachukua na yeye tulisikia sauti ya Mwanamke akipiga yowe weziii...wezii mara mlango ukafunguka anatoka baba wa kwenye huo kuanza kutufukuza,kila mtu alipita njia yake me binafsi nilitupa lile limfuniko nika kimbia niliamua kukimbilia maeneo ya kanisa la Wasabato sehemu ile kuna vimilima milima ndo ilkua pona pona yangu,wezangu hata ckujua walielekea wapi kwa muda huo nilikua na muomba Mungu anifikishe nyumbani salama.Na kweli nilivyoona hari imekua shwari nilitoka nduki kuelekea sehemu niliyokua nalala,nilmkuta huyo rafiki angu kumbe yeye alishakuja mapema alidhani nilishikwa.Basi tukalala kama vile hakuna msala tuliofanya kesho yake hao tukaenda shule.

Hilo tukio ndo lilisababisha me nafamilia yangu kuhama huo mtaa kwa sababu cku hyo ya tukio yule jamaa angu mwingne alionwa na yule mbaba alafu alikua anamjua so jamaa walimshikia kwao kubanwa kwa kipigo akatutaja tuliokua nawo.Nakumbukwa tulipigwa na mzee cku mpk leo nimebaki na alama karibu na nyusi jichoni.Mzee alinipiga na kisigino cha kiatu cha kike ( mzee wangu alikua ni mnyaama kwa kweli )

Mother ndo alimshauri mzee tuhame hapo kama ananitakia mema mimi na ndugu zangu mwanzoni alikua anakataa ila alivyoona nyumba tuliyokua tunakaa ilikua ndogo kwa familia aliamua kuhama baada ya kombe la dunia kuisha tukapata nyumba mitaa mwisenge na shule nilihama nikamfuata alipokuwa anafundisha.

Itaendelea....
 
Inaendelea


Kwanza samahani kwa kuchelewa kuleta muendelezo ni kutokana kutingwa na shughuli za kutafuta future's.

Haya tuendelee sasa

Baada ya kuhama kwenye nyumba mpya na mtaa mpya kiukweli maisha yalibadilika sana kwanzia mazingira na aina ya marafiki wapya nilio wapata hapo.Nyumba ilkua kubwa Vyumba 5,choo ni ndani kwa ndani.Lakini hapo tulipo hamia tulikumkuta jamaa mmoja ambae ni mtoto wa mwenye nyumba,alikua anakaa kwenye chumba kimoja vinne vilivyo baki tulkua tunakaa sisi.

Huyo mtoto wa mwenye nyumba kipindi hicho alikua amemaliza 4m 6 alkua anajiaanda kwenda chuo.Muda wa chuo ulivyofika akasepa zake chumba chake akaniachia niwe nalala.Jamaa alitokea sana kunikubali japokua nilikua bado yunk kuna vitu vyake vya siri alkua ananiambia.Tuachane nae kwanza huyu jamaa nitamuelezea mbele maana vitendo nilivyomfanyia tuliishia mwisho mbaya.

Mwaka 2008 nikiwa darasa la sita ckumbuki mwezi ila familia yangu iliyumba kiuchumi kidogo kutokana Baba yangu kusimamishwa kazi kwa muda kupisha uchunguzi ( alituhumiwa kutembea na wanafunzi kimapenzi ) ko hali ya kifedha ikawa chenga mama nae alikua kastop biashara yake tulkua tunaishi kwa kudra za mwenyezi Mungu tu.

Siku moja Mama aliniandika kibarua hivi na kutaka ni mpeleke binamu yangu ambae alikua anafanya kazi Garage ( hio garage ipo maeneo ya Mtaa wa Gandhi karibu na Mwigobero ) kwenye hicho kibarua alikua anataka msaada wa pesa tu.niliipeleka fresh tu na kweli nilipewa 20k siku hyo na maisha yakaenda.Me nilivyoona hivyo nikasema basi hapo ndo nitakua napata hela.Nilichokua nafanya nilkua naandika kabarua na kumpelekea huyo binamu yangu,yeye alikua anajua kinatoka kwa Mwana mother kumbe ni mimi muhuni ndo nilkua naratibu mambo 😄😄.Kweli pesa nilkua napata 20k,10k zilkua hazinikosi kwa huyo binamu.

Huo mchezo uliendelea hivyo hivyo Mama akiwa hajui nilifanyalo mpk nilivyofika form one 2010 ngoja nieleze nilivyonaswa.

Siku hyo nilkua sina Do ( pesa) nikimuomba Mama ananirusha Mzee ndo kabisaa nilikua cthubutu kabisa kumuomba nilikua na muogopa.Sasa cku hyo baada kuwaza sana nitapata wap hela ndo nikakumbuka kuwa kuna mkombozi wangu binamu.Nikaandika kabarua kama kawaida kesho yake nikakapeleka tena cku hyo niliomba nipewe 30k za Dawa ( nilkua nadanganya kuwa Mama ndo anataka ) basi midaa ya mchana baada kutoka shule nikala then nikaelekea garage,nilimkuta vizur tu nikampa kale ka ujumbe ni kamwambia Mama kanituma akakasoma.Alivyomaliza kukasoma nikawanaona mtu anajisachi,alikuwa hana hela siku hyo,akanambia nitangilie home yeye atakuja baada ya kutoka job.Nilivyockia hivyo moyo ulienda mbio kwa hofu nikawa najisemea moyoni kuwa leo nimeisha tamaa zangu zimeniponza.Nilienda home nikiwa nawaza sasa huyu akija itakuaje.Nilifika home nikamkuta Mama kalala zake kwenye sofa hana hata habar na Mtu nikatoka nje lengo ni kumsubir huyo binamu kama akina nimdanganye kuwa Mama hayupo.nilipokua nawaza hayo ghafla binamu huyo akaja na Pikipiki yake nilitetemeka vbya mno mpk jasho lilinitoka puani 🤣🤣🤣.Aliniuliza tu Shangazi yupo ndani badala ya kusema hayupo nikasema ndio yupo nadhani ni kutokana na hofu.Alivyoingia ndani nikaona isiwe kesi wala nini nikaamua kukimbia home kuepuka ile noma......

Nitarudi kukikucha.........
 
Musoma? kuna shule hapo kyabakari ilikuwa inaitwa Musoma Utalii. Mimi na mwanangu mmoja tulitoroka siku moja kwa kuruka fensi eee bwana eee tulikamatishwa na wahuni huko msituni simu ikaenda, viatu tukavulishwa mbaya zaidi na stori za kuwa tumekatwa mapanga zikawafikia wazazi. Ila hatukukoma kesho yake tulitoroka tena alfajiri tukasepa zetu Town. Shule ilikuwa ya kiboya sana ile.
 
Musoma? kuna shule hapo kyabakari ilikuwa inaitwa Musoma Utalii. Mimi na mwanangu mmoja tulitoroka siku moja kwa kuruka fensi eee bwana eee tulikamatishwa na wahuni huko msituni simu ikaenda, viatu tukavulishwa mbaya zaidi na stori za kuwa tumekatwa mapanga zikawafikia wazazi. Ila hatukukoma kesho yake tulitoroka tena alfajiri tukasepa zetu Town. Shule ilikuwa ya kiboya sana ile.
😂😂😂 pole mkuu ila kuwa pamoja nami nitakusimulia nivyokua nateka watu simu hususani ni wanafunzi na mabishoo plus masista duuh...
 
Inaendelea


Kwanza samahani kwa kuchelewa kuleta muendelezo ni kutokana kutingwa na shughuli za kutafuta future's.

Haya tuendelee sasa

Baada ya kuhama kwenye nyumba mpya na mtaa mpya kiukweli maisha yalibadilika sana kwanzia mazingira na aina ya marafiki wapya nilio wapata hapo.Nyumba ilkua kubwa Vyumba 5,choo ni ndani kwa ndani.Lakini hapo tulipo hamia tulikumkuta jamaa mmoja ambae ni mtoto wa mwenye nyumba,alikua anakaa kwenye chumba kimoja vinne vilivyo baki tulkua tunakaa sisi.

Huyo mtoto wa mwenye nyumba kipindi hicho alikua amemaliza 4m 6 alkua anajiaanda kwenda chuo.Muda wa chuo ulivyofika akasepa zake chumba chake akaniachia niwe nalala.Jamaa alitokea sana kunikubali japokua nilikua bado yunk kuna vitu vyake vya siri alkua ananiambia.Tuachane nae kwanza huyu jamaa nitamuelezea mbele maana vitendo nilivyomfanyia tuliishia mwisho mbaya.

Mwaka 2008 nikiwa darasa la sita ckumbuki mwezi ila familia yangu iliyumba kiuchumi kidogo kutokana Baba yangu kusimamishwa kazi kwa muda kupisha uchunguzi ( alituhumiwa kutembea na wanafunzi kimapenzi ) ko hali ya kifedha ikawa chenga mama nae alikua kastop biashara yake tulkua tunaishi kwa kudra za mwenyezi Mungu tu.

Siku moja Mama aliniandika kibarua hivi na kutaka ni mpeleke binamu yangu ambae alikua anafanya kazi Garage ( hio garage ipo maeneo ya Mtaa wa Gandhi karibu na Mwigobero ) kwenye hicho kibarua alikua anataka msaada wa pesa tu.niliipeleka fresh tu na kweli nilipewa 20k siku hyo na maisha yakaenda.Me nilivyoona hivyo nikasema basi hapo ndo nitakua napata hela.Nilichokua nafanya nilkua naandika kabarua na kumpelekea huyo binamu yangu,yeye alikua anajua kinatoka kwa Mwana mother kumbe ni mimi muhuni ndo nilkua naratibu mambo .Kweli pesa nilkua napata 20k,10k zilkua hazinikosi kwa huyo binamu.

Huo mchezo uliendelea hivyo hivyo Mama akiwa hajui nilifanyalo mpk nilivyofika form one 2010 ngoja nieleze nilivyonaswa.

Siku hyo nilkua sina Do ( pesa) nikimuomba Mama ananirusha Mzee ndo kabisaa nilikua cthubutu kabisa kumuomba nilikua na muogopa.Sasa cku hyo baada kuwaza sana nitapata wap hela ndo nikakumbuka kuwa kuna mkombozi wangu binamu.Nikaandika kabarua kama kawaida kesho yake nikakapeleka tena cku hyo niliomba nipewe 30k za Dawa ( nilkua nadanganya kuwa Mama ndo anataka ) basi midaa ya mchana baada kutoka shule nikala then nikaelekea garage,nilimkuta vizur tu nikampa kale ka ujumbe ni kamwambia Mama kanituma akakasoma.Alivyomaliza kukasoma nikawanaona mtu anajisachi,alikuwa hana hela siku hyo,akanambia nitangilie home yeye atakuja baada ya kutoka job.Nilivyockia hivyo moyo ulienda mbio kwa hofu nikawa najisemea moyoni kuwa leo nimeisha tamaa zangu zimeniponza.Nilienda home nikiwa nawaza sasa huyu akija itakuaje.Nilifika home nikamkuta Mama kalala zake kwenye sofa hana hata habar na Mtu nikatoka nje lengo ni kumsubir huyo binamu kama akina nimdanganye kuwa Mama hayupo.nilipokua nawaza hayo ghafla binamu huyo akaja na Pikipiki yake nilitetemeka vbya mno mpk jasho lilinitoka puani .Aliniuliza tu Shangazi yupo ndani badala ya kusema hayupo nikasema ndio yupo nadhani ni kutokana na hofu.Alivyoingia ndani nikaona isiwe kesi wala nini nikaamua kukimbia home kuepuka ile noma......

Nitarudi kukikucha.........
kumekucha aisee
 
Back
Top Bottom