Nilipokuwa Jeshi ya Kujenga Taifa (JKT) karibu nibakwe na afande fulani (jina nahifadhi). Lazima niseme kuwa katika kipindi hicho wanaume wengi waliona makambi ya JKT kama ‘buffet' yawasichana.
Si maafande wa jeshi tu, bali hata viongozi wa serikali walikuwa wanapitia makambi ya JKT kula tani yao! Mimi nilikuwa Masange JKT, Tabora. Wakati huo huyo jamaa alikuwa ni Kepiteni wa JKT.
Nadhani alidhania kwa vile yeyeni kepiteni basi alikuwa na haki ya kutembea na yeyote aliyemtaka. Kwangu aligonga ukuta! Bila shaka alikuwa hajawahi ‘kunyimwa' mpaka siku hiyo alipokutana na mimi.
Miaka baada ya tukio nikiwanafanya kazi Daily News mara nyingi nilikuwa napishana naye Posta Mpya. Basi ananisemesha, na mimi namnunia halafu napitazangu kimya bila kumjibu kwa hasira.
Siku moja kanisimamisha kaniambia, "Chemi, naomba msamaha, nisemahe tafadhali, kweli nilikukosea!" Aliongeza kuwa miaka mingi imepita hivyo sina sababu ya kuwa na hasira naye! Na mimi nilimjibu,"Mshenzi sana wewe!" nikaendazangu.
Ikapita kama mwaka mwiingine. Jamaa anaendelea kunisalimia kila nikimpita njiani na mimi kwa uchungu bado nikashindwa kusema kitu. Basi nikafikiria alichoniambia Posta Mpya. Lakini niliona kama jambo hilo linamsumbua.
Na nikasema kama Bwana Yesu aliweza kusamehe watu kwa madhambi yao kwanin imimi nisimsamehe. Basi baada yahapo ikiwa nikimwona na akinisalimia naitika na naendelea zangu na nikaona kidogo hata yeye alikuwa na raha.
Lakini bado najiuliza kama kitendo chake kilimsumbua miaka na miaka kama ilivyonisumbua mimi. Unauliza ilikuaje mpaka nikajikuta kwenye situation ya kubakwa. Au mnasema nilitaka mwenyewe. Ngoja niwaelezee ilivyokuwa.
Nilikuwa mhudumu Officer's Mess, mpishi na msafishaji. Huyo jamaa alikuwa ni mgeni kutoka Makao Makuu ya JKT Dar esSalaam. Kwa kweli sikutaka kufanya kazi pale Mess lakini tulichaguliwa special na Matron, mimi kwa vile niijua kupika vyakula mbalimbali hasa za kizungu.
Lakini uzuri wa hiyo kazi ni kuwa uanambulia mabaki ya vyakula (leftovers), na mara nyingine kulikuwa hakuna. Basi huyo Afande alikaa kambini wiki kadhaa. Katika kumhudumia tukawa tunaongea na mimi nikawa namheshimu kama kaka vile.
Wala sikusikia mapenzi yoyote kwake. Basi jioni fulani,kanialika chumbani kwake kunywa soda na biskuti na kwa Maongezi zaidi. Sasa kama ulienda jeshi unajua njaa kali unayokuwa nayo. Nikaenda, kanikaribisha vizuri, nilipewa soda na tukawa tunaongea.
Basi nikaona mwenzangu anabadilika ghafla! Mara ananikumbatia kwa nguvu, na kunibusu na mengine.Nikajaribu kuaga lakini jamaa hakuniachia. Baada ya ku-plead naye aniachie, kaniachia.
Kaomba msamaha na kaniomba niendelee kukaa nimalize hizo soda alizoninulia. Kama mjinga nikamwamini, nikakaa nakunywa hizo soda.Tukaendelea na Maongezi, kukaa kidogo huyo kanirukia, najaribu kusimama huyo, kanivuta nakuniangusha kitandani!
Mimi saa hizo nikawa naogopa kabisa nia yake! Kaniambia eti, "ukipiga makelele najua nitasema nini! Nyamaza! Huna sababu yakunikatalia!" LOH! Kanizaba kibao!
Nikamwuliza kwa nini anaifanyia hivyo, na mimi nilikuwa namwona kama kaka yangu! Hapo sasa ikaniingia. Nabakwa! Loh! Nilimpiga mangumi na mateke lakini jamaa alikuwa na nguvu huyo kachana chupi yangu!
Baada ya hapo, jamaa kashika miguu yangu huko anafoka kwa sauti kama vile anatoa amri "panua miguu! PANUA MIGUU!" Huko katoa uume wake uliyosimama kwenye suruali! Basi kuona sipanui jamaa kaongeza makofi na kafanikiwa kupanua miguu yangu!
Kuona kafanikiwa kupanua huyo kajaribu kupenya. Ilipogusa kwangu nilipiga kelelecha kufa! Nikasema,"Nakuufaaaa!"Heh! Ghafla jamaa kaniachia kaniambia niende.
Alisema,"Nimeigusa na ume wangu,unatosha!" Nenda zako! Naukimwambia mtu najua nitasemanini!"Loh nilikimbia bwenini nagiza lile la Masange huko nalia.
Wenzangu wananiuliza vipi, nikashindwa niseme nini! Kwanza niliona haya! Fikiria, niliona haya(shame)! Kesho yake nikaenda dispensary na kujiandikisha mgonjwa.
Sikwenda kazini Officer's Mess bali nililala bwenini. Siku iliyofuatia huyo Afande mshenzi kapita bwenini kwetu kaulizia hali yangu, na mimi huko natetemeka kwa woga nikashindwa niseme nini.
Alininunulia Orange squash nabiskuti na kuzileta bwenini. Sitasahau alivyonitazama! Ilikuwakama vile anapanga jinsi gani atanipata. Baada ya hapo alimwopoa msichana mwinginena huyo alimkubali kabisa.
Akawa analala kabisa huko Officer's Mess. Hakuna anayemsumbua wakijua ni bibi wa Afisa. Basi,siku za yule jamaa kukaa kambini zikaisha, na yule binti aliendanaye Tabora mjini kwa sikukadhaa. Halafu jamaa karudi zake DSM.
Yule binti karudi zake kambini! Kumbe alienda bila pass. Alidhania kwa vile yuko na mkubwa hana haja ya pass. Nayule Afande ndo kaondoka kimoja! Maafande waliobakia wacha wamtese huyo binti alivyorudi kambini!
Walimtesa kwa Extra drill na mengine mpaka ikabidi Military Police waombe wakuu wamsamehe la sivyo atakufa. Raha yake iliishia kwasuluba! Sijui yule binti alidhania jamaa atamwoa! Kwa nini alimkubali yule mshenzi.
Anyway, kila mtu na vyake. Alivyotoka kwenye suluba tulimwuguza! Siku haizi kupita na mimi nilitolewa kazi Officer'sMess na kupelekwa kwenye kikosicha Ujenzi na lazima niseme hapo nilifurahi sana.
Basi miaka ilipita. Mimi nilikuwa mwandishi wa habari Daily News, tena nilijenga jina. Sasa nikawa napishana na yule jamaa huko kapandishwa cheo na yuko JWTZ. Jamaa anajaribu kunisalimia namimi napita zangu kimya, namnunia kabisa.
Nilimwona mshenzi, mnyama, nakila kitu kibaya ndo ilikuwa yeye! Angefanikiwa kuingiza nakunimwagia uchafu wake ningejiona mchafu mpaka leo! Miaka kama 20 imepita sasa nabado nina uchungu naye. Jamani nyie wanaume nawaambia kubaka kunaathari zake kwa wanawake.
Unataka raha ya dakika na unamwachia mwenzio na uchungu wa maisha! Wengine mpaka wanakuwa wagonjwa wa akili. Kwa nini nimeamua kuzungumzia kubakwa kwangu hapa, ni kwasababu naona wasichana wengi wa nabakwa, halafu wanaamua kunyamaza kimya.
Kisa wakienda polisi na hospitali wanahofia kuambiwa ni Malaya au walitaka wenyewe! Hata mwamanke mwenzako anaweza kukufokea kuwa ulitaka mwenyewe.Tanzania, wanaume walikuwa na usemi wao kuhusu wanawake na ngono.
Walisema eti ukimwomba mwanamke halafu akijibu ndiyo,manake ndiyo atafanya. Akisema labda, manake atafanya, akisema hapana, manake hapana. Lakini jamani tendo si inakuwa tamu kama wote mmekubali? Na kama angefanikiwa kuingiza si angeniumiza sana! Wengine wanasema ningemshitaki.
Je, ningemshitaki ingekuaje? Kwanza jeshini mimi ningepewa Extra Drill mpakaniumie au kufungwa jela ya jeshi iliyojaa maji na mbu kusudi niteswe. Kumbuka ilikuwaTanzania na yule alikuwa ni Kepiteni wakati huo na mimi nilikuwa Private.
Hakuna ambaye angekuwa tayari kunisikia zaidi ya wenzangu ma Private, na yeye alijua hivyo. SHENZI TAIPU!