Story: Mahusiano



ALoyce: Kusema kweli Penny Anita nilimwonaga bank pale Posta.. nilikuwa naweka hela nilipomaliza kuweka nikaenda ATM kujua kama imeingia kweli.. nikakuta mlolongo mreeefu wa watu nikakosa pozi basi nikaamua kwenda reception kuulizia balance ndio namkuta mrembo Anita akanikaribisha vizuri sana maskini sauti nyororo ya upole anasauti nzuri ya kuvutia kama kindege
Alipomaliza kunihudumia nikamwomba namba ya simu akaniambia hana simu kwa sasa ... nikaondoka zangu saa 12 nipo mlangoni namwona anatoka anaenda Posta kupanda daladala nikamfuata mpaka na daladala zinapoenda kila daladala ikisimama na mie nasimama mbele ya daladala na gari yangu namwangalia kwa kioo cha nyuma anashuka au anaendelea
Nikamfukuzia akashuka bamaga akapanda la kwenda sinza akashuka kijiweni akaanza kutembea anaingia ndani ndani sasa huko gari haifiki
Kifupi nimemfuatilia mwenzi mzima kuna siku nimemchukua rafkiangu akawa anaendesha gari mimi nimekaa seat ya abiria aliposhuka kijiweni nikamfuata kwa nyuma hauwezi amini huyu Anita alienda kuingia kwenye kanisa moja kichafu kichafu cha udongoo kibayaaa doh nilichoka akakaa huko mpaka saa 1 usiku akatoka akaenda kupanda daladala mpaka mwenge akashuka akapanda la tegeta akashuka Tangibovu akaenda kwao
Sikuelewa kwanini alikuwa anajitesa lakini ni mtoto wa kishua na sijajua kwanini ameenda kwenye kanisa chafuchafu
Sasa Penny naomba uwe rafkiake kwa sasa akishakuamini utaachia ngazi mimi nitaingia kuendesha gari unasemaje?!
Money Penny: nikahisi Mungu ameamua kunitembelea kipekee nikamjibu kwa haraka natafuta tempo job shule imeshaisha nataka nikafanye katempo job mpaka nigraduate unaonaje ukinitafutia tempo anapofanya Anita hapo itakuwa rahisi kumzoea Anita
Aloyce: mmmh ngoja niongee na rafkiangu tuone cha kukusaidia
Money Penny: kingine kabla sijasahau... hela unanilipa ngap maana hii ajira no 2... nahitaji mshahara kila week sio unanimaliza nguvu tu hapa staki kuzeekea kwenye kazi yako pia ukimpata Anita au la sio shauriyangu ni wewe na udomo zege wako maana kwa maelezo yako huyu Anita haujawahi hata kuongea nae zaidi ya pale Benki
Sasa ukimkosa usinilaumu na chenji sirudishi na nikimaliza tempo field nataka ajira full staki ujinga
Aloyce: hamna shida Penny tupo pamoja akaingiza mkono mfukoni akanipa lakini 5 kafanye shopping na nauli ya kuanza Tempo kesho nakuja nikuelekeze upeleke barua ya maombi...akaondoka zake me nacheka kimoyomoyo sijui itakuwaje kama sijaja kuuwawa baaaas tena Mungu atakuwa amenisimamia sana
Kesho kweli akaja nyumbani akachukua barua yangu akaondoka nayo
Baada ya wiki 1 akaja Penny umeshapata field unatakiwa kesho saa 3 interview ndogo nenda benki ya Anita ... nikaelekezwa pale na lakini 5 ingine nikapewa hata ile ya Kwanzaa sijamaliza kuila
Kesho nikaondoka mzee dada kufika nakutana na warembo kibao wameshikilia makaratasi wanasoooma wenyewe wanaambiana hili swali lazima tuulizwe embu nielezee wanajazana ujinga na kuogopeshana
Pembeni yangu kulikuwa na mdada mwengine anaitwa Subira... mimi na yeye tulikuwa sawa tunawashangaa hawa mademu vepe mbona imani hawana?! Tukawa tunaangaliana tunaishia kucheka
Baada ya nusu saa wakaingia kwanza wale warembooo walipotoka wanasubiriana kuulizana mmeulizwa nini kumbe wanayoyasoma hamna hata waliloulizwa wanalalamika interview ngumu mshahara mdogo doh nikachokaaa
Akaja mdada akamwita subira nikabakia pekeyangu wa mwisho subira akakaa nusu saa hatoki uoga na shetani wakaandamana ndani ya akili yangu. .mara akaja kijana akaniuliza we ndio Penny nikamjibu ndio akaniambia nimfuate nikamfuata kuingia namwona subira amezungukwa na grup la mabosi kama 5 naulizwA maswali nikachokaaa
Nikaketi chini na yule kaka nikashangaa yeye ndio ananiuliza maswali ya interview... maswali yenyewe sasa bora yangekuwa maswali basi... nimeishia kuulizwA maswali ya kiboya unaitwa nani. .. unamchumba. . Umeolewa.. mbona mzuri sana.. kwenu mnahela ua.. unauhakika hauwezi iba hela ukakimbia utadhani nafanya interview ya ukahaba ... baada ya interview ya kikahaba nikapelekwa reception naambiwa hapa ndio utakuwa unafanya kazi kwa mwenzi huu mwenzi ujayo utahamishwa huyu hapa ndio mwenzio mtakuwa nae anaitwa Anita. .. kazi ndio imeanza mama kabla ya lunch uje Usain mkataba na mshahara
Kweli sikuielewa ile kazi lakini nikapotezea maana ajira yenyewe nimewekwaaa tu kwan tsh ngap?!
Nikapewa Anita kama Supervisor wangu anifundishe kazi basi rohoni nacheka kweli kwa Mungu hakuna kubwaa ananifundisha sauti nyororo kama sololist wa kwaya
Kabla ya lunch nikaenda kusaini mkataba nashangaa kukuta mkataba wa internship na ni miezi 6 doh nilichoka. ..mshahara sasa doh sikuamini niliona kama nimependelewa kwakweli lkn unafanyaje sasa hakuna!
Kurudi namkuta mrembo Anita amekaa sikuhio wateja hamna basi tukaanza kuongea kufahamiana akaniuliza naishi wap nikamwambia naishi upanga mtaa wa lugalo akaniambia yeye anaishi kunduchi beach nikashtuka moyoni heee?!
Tukaongea mambo ya kawaida tu na mambo ya kazi na nini siku ikaisha. ..wiki ikaisha wiki ya 2 nipo na Anita, mchangamfu mwenyewe mrembo sana.. nikagundua vitu vingi kuhusu Anita
Moja wapo ni mdada msiri sana.. na usiri wake unamfanya aonekane wa mawazo moyoni
Siku moja pale kazini alikuja libaba limoja.. akaja mapokezi akamwambia atone nje kwa kumeamrisha
Anita akatoka akakaa kama dk 10 akarudi analia nikashangaa kulikoni anazidi tu kulia
nikambembeleza pale nikamwingiza ndani akawa analia sana.. baada ya dk 5 boss akaja kuna nini wateja wanasubiria sana nyie mko huku mmefiwa au?!
Penny nikamtetea kuwa anaumwa tumbo la siku ndio boss akapoaaa akamweka mtu mwengine mapokezi akaniambia mpeleke hospital kesho asije kazini apumzike siku 5
Tukaondoka mapemA wote kufika nje akachukua taxi akaniambia twende Penny nisindikize mahali nikajongea Taxini zamani ilikuwa hotcake kama sasa hivi useme Uber
Akamwelekeza DerevA Taxi iende upanga mtaa wa lugalo nikashtuka kujua Anita anakumbuka napoishi
Tukafika nyumbani kwetu uzuri wangu ni kwamba nilikuwa naishi na dada lkn nyumba ilikuwa ya wazee hawashindi hapo kabisa
Kufika Anita akaniambia Penny naomba nihamie kwako tafadhali. .. kumwuliza kwanini hataki kwenda kwao Kunduchi akafungukaaa
ANITHA: Penny ndugu yangu, mimi sina wazazi... wazee wangu wote walishakufaga kwenye ajali ya gari nikiwa nasoma sekondari form 4 nilipomaliza tu maisha ya kijijini yakanishinda nikauza mali zote za wazazi nikaja kuishi Dar pale Sinza Mori .. nikawa najisomesha kwa hela za wazee nikachukua certificate baadae nikajisomesha diploma
Katika soma soma yangu Darasani nikapendwa na lile libaba lililokuja leo ofisini.. mapenzi kolea akanihamisha sinza akanipeleka kwake Tangibovu nikawa naishi nae
Tulianza mapenzi yetu yalikuwa maziri sana akawa analipa ada zangu zote, ananipa hela ya matumizi akaninunulia usafiri wa gari nikawa sijui kuendesha akanipeleka Veta nikaenda kusoma mpaka nikaweza kuendesha gari...zile hela za wazee zikawa zimekaa tu kwenye sanduku ndio akanifundisha kuweka hela banki nikaziweka zile za wazee bank tena kwa siri asijue kwenye fixed deposite
Nilipomaliza shule akanitafutia ajira pale bank nikaanza
Money Penny: oh that's nice so tatizo lipo wapi?!
Anita: mmh we acha tu tatizo yule baba simwelewi unajua ukiishi na mtu ndio unajua kila kitu chake
Yule Baba nilikuja kumkuta ni mvuta bangi mkubwa. .. anakikundi cha vijana majambazi wanafanya na utapeli wanaibia watu kuna siku waliweka kikao pale Tangibovu nikiwa nimelala alfajiri saa 10
Kushtushwa na kelele zao nawsikia wanapanga maovu ya kuvamia watu huku wanavuta vitu vyeupee ...niliishiwa usingizi mpaka leo pale Tangibovu nakuona pachungu
Vile vikao havikuisha wale vijana wa yule baba wakawa wananitaka kimapenzi wakilewa wanafanya fujo zilishawahi pigwa risasi mule ndani baada ya yule baba kunifumania nimeshikwa kiuno na kijana wake mmoja asikwambie mtu sijui niliponaje
Baada ya miaka 3 kupita nikaenda bank kuangalia hela yangu nikakuta imeongezeka ... na kwasababu maisha ya pale Tangibovu yalishanishinda nikachukua hela nikanunua kiwanja kunduchi beach
Nikawa najenga mdogo mdogo kwa siri sana na kujiiba sana... mpaka leo nyumba imeshasha ina vyumba 3.. master room 1 na vyumba vya kawaida 2 ..kuna jiko na choo na bafu na sebule.. nyumba ya mlinzi na garage bila yule baba kujua na mpaka hapa nakuambia hajui kitu
Nyumba ilipoisha nikaipangisha kwa muda wa miaka 2 sasa. . Hela naweka bank na wapangaji risiti wananiletea hapa kukiwa na shida wanakuja pale kazini naenda kurekebisha haya ndio maisha yangu Penny
Sasa ugomvi mkubwa ulitokea miezi 6 iliopita. ..mwanaume akawa mbogo analeta wanawake ndani haniheshimu tena wakati yeye ndio alinibikiri nikamuonya na kumsihi aache tabia yake mbaya lkn hakusikia
Nikaja kuchukua hela aliziweka kwenye droo nikaenda kupanga mtaa wa 5 Tangibovu akanitafuta sana lkn hakujua napoishi baadae vijana wake wakamtonya nilipo akaja kunichukua rudi rudi kibaoo
Maisha na yule bwana yakanishinda siku nimekaa kituoni naskia watu wanahubiri habari za Yesu wadada wazuri kweli wakanipa kipeperushi wananikaribisha kwenye semina nikaenda
Kufika kwenye seminar neno la Mungu likanijaaa nikaokokaa wakanikaribisha kanisani kwao sinza tandale ndani ndani
Nikawa kila week nikitoka kazini naenda kanisani hata kama hamna seminar naenda tu ilimradi nipoteze mawazo siwezi kwenda baa wala night club maana nimeokoka na nyumbani yule bwana simwelewi kawa kama amechanganyikiwa nalala na mabastola masigara mabangi yani kama nipo kuzimu
So nikitoka tu kazini naenda kanisani narudi Tangibovu kwa yule bwana maana kule nilipopanga alinihamisha kwa nguvu nikifika namkuta hayupo naingia kuoga nalala
Akija analala kalewaaa alfajiri naamsha popo nawahi kazini
Sasa Jana jumamosi nikashinda kanisani Kurudi tumegombana anagomba sana ananiambia wewe naskia umeokoka sikuhizi vipi umechanganyikiwa?! acha ujinga
Nikamtemea cheche zangu kuwa simpendi tena nataka kuondoka kwenye maisha yake akanitishia kuniua nikakimbia nikaenda kujifungia stoo akaja akanipiga sana mateke na mangumi... ona hapa kwenye kifua nimekuwa mwekundu ona mbavu zangu hazifai hata hivyo nimejikaza sana kuja kazini leo
Alivyonipiga vile mimi nakohoa damu akaondoka nikakaa sana pale chini kuja kushtuka ni j2 asbh saa 10 alfajiri...uzuri nilikuwa na namba ya taxi dreva nikakusanya kila kitu changu nikaondoka kwenda kanisani sinza akanipokea Pastor Papaa kuona nakohoa damu akanipeleka hospital pamoja na shemasi wa kike yeye akarudi kuendelea na ibada
Nikakaa hospital mpaka mchana nikarudi kanisani ibada imeshaisha nikaongea na mchgj Papaa akaniambia hamna shida uwe unalala kanisani
Jana nimelala kanisani... asbh nikasema nijikaze nije kazini lile libaba lililonipiga ndio limekuja pale linaniambia nirudi nyumbani la sivyo ataniachisha kazi sijui nitaenda wap kazi ndio kila kitu kwangu ni kweli ni yeye akanitafutia lkn Kurudi Tangibovu sirudi Penny naomba niishi hapa kwako mpaka akili ikae sawa
Money Penny nikamhurumia sana Anita.. ila sikuwahi na uhakika sana na ukweli wa maneno yake si unanijua me Penny nilivyokuwa mbishi mpaka nichunguze mwenyewe ndio niamini
Nikamkaribisha kwa mikono 2 nikamwelekeza pa kulala nikamwambia kanisani asiende kwanza tutatafuta simu ya pastor Papaa tumwambie unaishi hapa kwa sasa mpaka baadae akakubali
Tukashinda nyumbani pale tunapika tunakula na kucheka nikiwa na maswali mengi itakuwa kama Aloyce atakuja hapa amkute atakuwa amejiharibia vibaya mno...


KUENDELEA NA HADITHI HII BONYEZA LINK HII HAPA MAHUSIANO ~ 1 – Money Star Stories

 
wallah usingenitag ningeandamana tarehe hiyo kwa ajili yako


Wengine hii story tutakapokuwa tunaigutukia ni hapo hapo maana hatujulikanagi
Hata kusoma nimeahirisha

Teh

Si ni leo tar17

Ingawa hujaniita ila nimefika

Unaanzisha story halafu humalizii. Mara unarukia kuanzisha nyingine.

Njoeni nimeletaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom