Story fupi yenye mafunzo


L

Lilwayne

Member
Joined
Nov 15, 2011
Messages
50
Likes
1
Points
0
L

Lilwayne

Member
Joined Nov 15, 2011
50 1 0


Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!!
Penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha. Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya nikawa mtumwa wa ng
ono kila nikienda chumbani kwake.
Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.


Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu.
Nilipenda tututmie kinga lakini aliipinga sana. Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanya alivyotaka. Kwa mara ya kwanza nikatyoa mimba.
Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua.
Pombe kidogo na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa nawahi kulewa.
Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya lililonifanya niandike haya kwako.
Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!!
Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi.Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu.

Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo.
Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile.
Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto. Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi?Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!!
Nilijua tayari ameniacha!!!
Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima hospitali.
Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia.
Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda.
Nilipomaliza chuo akajitambulisha nyumbani na alitaka kunioa.
Akanio kweli. Maisha yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba.
Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwa hi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.
Nikaambiwa kizazi change kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa.
Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu.
Dunia haikuwa mahali pangu sahihi.
Nimekuandikia barua hii mdogo wangu. Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyika na kufanya mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi.
Wasipokusikiliza usijisikie vibaya maana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu.Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia wasichana hawa.


Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako AMENITENDA HIVI!!! TAFADHARI TAFAKARI
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Likes
1,310
Points
280
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 1,310 280
Duh,simulizi hii imeletwa hapa sijui hii ni mara ya ngapi.!
 
Asnam

Asnam

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2012
Messages
4,262
Likes
52
Points
145
Asnam

Asnam

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2012
4,262 52 145
Duh,simulizi hii imeletwa hapa sijui hii ni mara ya ngapi.!
si mbaya ikirudiwa hata mara elfu ili mradi wageni ktk nchi ya sodoma na gomora tupate kuyaona maandiko yatupe mwangaza
 
Arushaone

Arushaone

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Messages
14,637
Likes
1,115
Points
280
Arushaone

Arushaone

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2012
14,637 1,115 280
Hii kwa kiingereza inaitwa 'copy & paste'. Kuwa mbunifu na ulete kisa kipya bhana!
 
Scofied

Scofied

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2012
Messages
2,070
Likes
272
Points
180
Scofied

Scofied

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2012
2,070 272 180
si mbaya ikirudiwa hata mara elfu ili mradi wageni ktk nchi ya sodoma na gomora tupate kuyaona maandiko yatupe mwangaza
Ikirudiwa sana inabore arifu.....
 

Forum statistics

Threads 1,237,082
Members 475,401
Posts 29,277,620